Mabel Dove Danquah
Mabel Dove Danquah (alizaliwa mwaka 1905 [1] mji wa Accra nchini Ghana) alikuwa mwandishi wa habari kutoka mji wa Gold Coast mwanzoni mwa mwaka 1984, pia alikuwa mwanaharakati wa kisiasa[2] na mwandishi mbunifu,ni miongoni wa wanawake wa mwanzo katika Afrika Magharibi kufanya kazi katika nyanja hizi.[3]Kama vile Francis Elsbend Kofigah anavyosema kuhusiana na waanzilishi huyu wa fasihi kutoka Ghana, "kabla ya kuibuka kwa watetezi hodari wa ufeministi wa kifasihi kama Efua Sutherland na Ama Ata Aidoo, kulikuwa na Mabel Dove Danquah, mwanzilishi wa ufeministi mkali." [4]
Alitumia njia mbalimbali za kutetea Haki za Wanawake, kama majina bandia katika uandishi wake kwa magazeti ya miaka ya 1930, "Marjorie Mensah" katika gazeti The Times of West Africa; "Dama Dumas" katika andiko la African Morning; "Ebun Alakija" katika gazeti la Daily Times la Nigeria na "Akosua Dzatsui" katika gazeti Accra Evening News.[3] Aliingia katika siasa katika miaka ya 1950 kabla ya uhuru wa Ghana. Alikuwa ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa mshiriki wa bunge lla nchi yake ya Ghana, lakini pia alikuwa ni mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuingia bunge la Afrika.[5] Mwanandishi huyo alihamasisha ufahamu na uhitaji wa kujitawala kupitia kazi zake.[6]
Elimu na historia yake kwa Ufupi
[hariri | hariri chanzo]Mabel Ellen Dove alizaliwa katika jiji la Accra Mama yake alifahamika kwa jina la Eva Buckman na alikuwa ni Mfanyabiashara mwanamke kutoka miji wa Osu, na Baba yake bwana Francis (Frans) Dove (1869-1949),[7] ambaye alikuwa Mwanasheria kutoka nchini Sierra Leone ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa Gold Coast Bar.[3]Akiwa na Dada zake, Mabel akiwa na umri wa miaka sita walipelekwa katika Shule ya Kumbukumbu ya Annie Walsh huko Freetown, nchini Sierra Leone,[8]na baadaye kupelekwa huko nchini Uingereza kupata Elimu zaidi katika Convent ya Anglikani huko Bury St. Edmunds na Chuo cha St. Michael Hurstpierpoint,[9] ambapo alichukua kozi ya ukatibu, kinyume na matakwa ya Baba yake.[10][11]
Alirudishwa Freetown na akiwa huko alisaidia kuanzisha timu ya kriketi ya wanawake,[12] alishiriki katika jumuiya ya michezo ya ndani ya eneo hilo na kusoma sana, kabla ya kurudi tena Gold Coast akiwa na umri wa miaka 21.[9] Alipata kazi kama mtaalamu wa kuandika kwa kutumia kinakirishi (taipisti) na Elder Dempster na kufanya kazi hiyo kwa miaka minane, baadaye akahamishwa hadi G. B. Olivant kabla ya kwenda kufanya kazi kama Meneja katika kampuni ya biashara ya A. G. Leventis.[9]
Uandishi wa habari
[hariri | hariri chanzo]Alianza kazi ya uandishi kwa kuliandikia gazeti la The Times of West Africa, gazeti la kwanza la kila siku la Ghana, ambalo lilianzishwa na kumilikiwa na Dkt J. B. Danquah kwa lengola kutetea kwa nguvu haki msingi za binadamu huku likikemea utawala wa kigeni.[13] Kupitia safu ya "Ladies Corner [Kona ya Wanawake] na Marjorie Mensah" kati ya mwaka (1931-34),[3] makala zake zilimletea umaarufu mkubwa nchini kote,"aliwashauri wanawake kuthubutu na kujivunia jinsia ya kike, kupata msukumo kutoka kwa wapingaji, kukemea ubeberu, na kupigania haki zao."[3][14] Pia alishinda kupongezwa na mmiliki wa makala hiyo, ambaye hatimaye alimuoa mnamo 1933.[1] Mnamo 1939, alitoa hotuba za redio ili kuunga mkono juhudi za vita.[15]
Baada ya The Times of West Africa kukoma kufanya kazi, aliendelea kuandikia Magazeti ya African Morning Post mnamo miaka ya (1935–40) na Daily Times ya Nigeria mnamo mwaka (1936–37), Accra Evening News manamo miaka ya (1950–1960) na Daily Graphic mwaka ( 1952). Mnamo 1951 alikuwa mhariri wa gazeti la Accra Evening News – akihariri Makalaya Convention People's Party (CPP), iliyoanzishwa mwaka wa 1948[16], alikuwa mwanamke wa pili kuwahi kuhariri gazeti nchini Ghana. Ingawa uteuzi huo uliisha baada ya miezi mitano kwa sababu ya kutokubaliana na kiongozi wa CPP Kwame Nkrumah kuhusu mbinu za uhariri,[10] alibaki mwaminifu kwa Nkrumah na chama chake.[17]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Heroes Of Our Time — Ms Mabel Ellen Dove". Modern Ghana (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-14.
- ↑ Kwasi Gyamfi Asiedu. "Africa has forgotten the women leaders of its independence struggle". Quartz (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-14.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Benson, Eugene; Conolly, L. W. (2004-11-30). Encyclopedia of Post-Colonial Literatures in English (kwa Kiingereza). Routledge. ISBN 978-1-134-46848-5.
- ↑ Kofigah, Francis Elsbend, "The Writing of Mabel Dove Danquah" (thesis) Archived 2016-03-05 at the Wayback Machine, Kwame Nkrumah University of Science and Technology, Kumasi, 1996.
- ↑ Margaret Busby, "Mabel Dove-Danquah", in Daughters of Africa: An International Anthology of Words and Writings by Women of African Descent (1992), 1993, p. 223.
- ↑ B. I. Contributor (2020-08-04). "Here are 7 women who played a role in Ghana's independence struggle". Business Insider Africa (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-03-14.
{{cite web}}
:|author=
has generic name (help) - ↑ https://thejournalofsierraleonestudies.com/downloads/Version6.pdf
- ↑ Cornwall, Andrea (2005). Readings in Gender in Africa (kwa Kiingereza). Indiana University Press. ISBN 978-0-253-34517-2.
- ↑ 9.0 9.1 9.2 Cornwall, Andrea (2005). Readings in Gender in Africa (kwa Kiingereza). Indiana University Press. ISBN 978-0-253-34517-2.
- ↑ 10.0 10.1 Sheldon, Kathleen E. (2005). Historical Dictionary of Women in Sub-Saharan Africa (kwa Kiingereza). Scarecrow Press. ISBN 978-0-8108-5331-7.
- ↑ News Ghana. "Mabel Dove-Danquah was an exceptional lady | News Ghana". https://newsghana.com.gh/ (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-03-14.
{{cite web}}
: External link in
(help)|work=
- ↑ Cornwall, Andrea (2005). Readings in Gender in Africa (kwa Kiingereza). Indiana University Press. ISBN 978-0-253-34517-2.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-02. Iliwekwa mnamo 2022-03-14.
- ↑ Moynagh, Maureen; Forestell, Nancy (2012-01-14). Documenting First Wave Feminisms: Volume 1: Transnational Collaborations and Crosscurrents (kwa Kiingereza). University of Toronto Press. ISBN 978-1-4426-6410-4.
- ↑ Wendell P. Holbrook, "British Propaganda and the Mobilization of the Gold Coast War Effort, 1939–1945", Journal of African History 26, 4, World War II and Africa (1985), p. 354.
- ↑ Company, Johnson Publishing (1972-07). Black World/Negro Digest (kwa Kiingereza). Johnson Publishing Company.
{{cite book}}
: Check date values in:|date=
(help) - ↑ Cornwall, Andrea (2005). Readings in Gender in Africa (kwa Kiingereza). Indiana University Press. ISBN 978-0-253-34517-2.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mabel Dove Danquah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |