Kondomu ya kike
Kondomu ya kike | |
---|---|
Polyurethane female condom | |
Mandharinyuma | |
Aina ya udhibiti wa kuzaa | Barrier |
Matumizi ya kwanza | 1980s |
Failure vya mimba (first year) | |
Matumizi kamili | 5% |
Matumizi ya kawaida | 21% |
Matumizi | |
Ugeuzaji | Immediate |
Vikumbusho vya mtumiaji | ? |
Manufaa na hasara | |
Ulinzi kutokana na magonjwa ya zinaa (STD) | Yes |
Manufaa | No external drugs or clinic visits required |
Kondomu ya kike ni kifaa cha plastiki kinachotumika wakati wa kufanya ngono kama kingamimba (kikifeli kwa asilimia 5-21) na kwa lengo la kupunguza hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa (kama vile Kisonono, Kaswende na Ukimwi) lakini hata katika hilo kinafeli kuliko kondomu ya kiume[1].
Kondomu ya kike ni kifuko chenye duara zinazopindika kila upande. Kabla ya ngono ya uke, duara lililo ndani ya kifuko huingizwa kwenye kina cha uke, ili kuishikilia kondomu katika uke. Uume huingizwa moja kwa moja katika ufuko kupitia upande wa duara ulio wazi, ambao hubaki nje ya uke wakati wa ngono.
Kondomu za kike zinaweza kutumika na mwanamke wakati wa kufanya ngono ya tupu ya nyuma.[2] [3]
Kondomu hiyo ilivumbuliwa na daktari wa Denmark Lasse Hessel, na huvaliwa kwa ndani na mwanamke ili kuzuia manii isiingie katika mwili wake.
Mpaka sasa kifaa hicho hakijaanza kutumika kwa wingi, tofauti na mpira wa kiume.
Aina na vifaa
[hariri | hariri chanzo]Kondomu ya kike ya kwanza ilitengenezwa kwa poliyuretheni. Aina hiyo inaitwa rasmi "Kondomu ya kike ya FC". Aina mpya zaidi imetengenezwa kwa mpira wa nitrili na inaitwa "FC2" [4] (mabadiliko haya ya vifaa yalitangazwa mnamo Septemba 2005). [5]
Kondomu za nitrili za karibuni zaidi zina uwezekano mdogo zaidi wa kutoa sauti inayotokana na kukunjika kwa kondomu na ambayo huenda ikafadhaisha watumiaji. Kuna matumaini kuwa kondomu hizo za nitrili pia zitaruhusu kupungua kwa bei. [5] Aina hiyo ya kondomu hutengenezwa na kampuni ya afya ya wanawake ya Female Health nchini Marekani.
FC1 na FC2 ndizo kondomu pekee za wanawake zinazopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kama kifaa cha ziada cha kulinda afya ya uzazi na kujamiiana. UNFPA, shirika la Umoja wa Mataifa, imeingiza kondomu ya kike katika mipango yake. [6] Kondomu hizi huuzwa chini ya chapa kadhaa ikiwa ni pamoja na Reality, Femidom, Dominique, Femy, Myfemy, Protectiv na Care.
Toleo la hivi karibuni la kondomu ya kike limetengenezwa kwa ulimbo wa mpira asili, sawa na ule unaotumika kuunda kondomu ya kiume. Kondomu hiyo haitoi sauti kama zile za plastiki. Aina hiyo ya kondomu ya kike hutengenezwa na kampuni ya Medtech Products Ltd, nchini India. Inauzwa chini ya chapa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Reddy, V Amour, L'amour, VA WOW Feminine condom na Sutra. Jaribio zaidi la kiafya linahitajika kabla ya kufikiriwa kupewa kibali cha FDA nchini Marekani. [7]
Programu ya Teknolojia Inayofaa kwa Afya (PATH), ambayo ni programu ya kimataifa ya afya isiyolenga faida, imeunda pia kondomu ya kike ya kutumika katika nchi zinazoendelea. Kondomu hiyo inatengenezwa na Shanghai Dahua Medical Apparatus nchini Uchina na kwa sasa inapitia majaribio ya kimatibabu. [8]
Gharama na "Utumiaji tena" wa (poliyuretheni) asili ya FC
[hariri | hariri chanzo]Bei ya kondomu ya kike ni ya juu kuliko ile ya kondomu ya kiume lakini kuna ushahidi unaoonyesha kwamba kondomu za kike za poliyuretheni zinaweza kuoshwa, kuuliwa viini, na kutumiwa upya.
Utumiaji upya wa kondomu za kike za poliyuretheni hauchukuliwi kuwa salama ukilinganishwa na kutumia kondomu mpya. Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani linasema, "bechi za kondomu mpya za wanawake ambazo zilikuwa bado hazijatumika zilipitishwa kwa duru saba za kuua viini, kuosha, kukausha na ulainishaji upya, kulingana na utaratibu wa rasimu ya protokali, lakini viwango vya juu zaidi vya dawa ya klorini hutumika na kwa muda mrefu zaidi. Bechi zote za kondomu ya kike zilifuata kanuni kamili za kukadiria ubora wa utengenezaji kuhusu ukakika wa miundo baada ya vipindi kadhaa za majaribio. ... Kuua viini, uoshaji, kukausha, ulainishaji upya na utumiaji upya wa kifaa hiki hakuhusishwa na kutoa shahawa, dalili za mwasho kwenye uke au matokeo mabaya ya utafiti wa uke na mlango wa uzazi kati ya waliojitolea kufanyiwa utafiti". [9]
Wasilisho katika mkutano wa kimataifa kuhusu UKIMWI mwaka 1998 ulithibitisha kuwa "kuosha, kukausha na kutia tena mafuta kwenye kondomu ya kike hadi mara kumi hakubadili sana uhakika wa muundo wa kifaa hicho. Majaribio zaidi ya kimikrobiolojia na kivirolojia vinahitajika kabla ya kupendekeza utumiaji upya wa kondomu hiyo ya kike." [10]
Ulainishaji
[hariri | hariri chanzo]Kama ilivyo na kingamimba zote zinazozuia shahawa kuingia kwenye uterasi, maji au mafuta ya kulainisha yaliyotengenezwa kwa silikoni ni salama yakitumiwa katika kondomu ya kike. Mafuta huharibu ulimbo wa mpira na hayapaswi kutumiwa na kondomu ya kike iliyoundwa kwa ulimbo huo. Mafuta hayapaswi kuathiri moja kwa moja kondomu za kike zisizo za ulimbo wa mpira lakini yanaweza kufanya usafishaji na uuaji wa viini katika kondomu hizi bila kuzidhoofisha zaidi uwe mgumu na unaweza kusababisha matatizo ya kiafya ambayo yanaweza kudhoofisha kinga-mwili za mtu kutokana na maradhi ya zinaa yaliyo mabaya.
Faida
[hariri | hariri chanzo]Faida ya kondomu za kike za plastiki ni kuwa zinapatana na mafuta ya kulainisha tofauti na yaliyofanywa kwa mpira. [11] Sehemu nyeti za nje za aliyevaa kondomu na sehemu ya chini ya uume wa mpenzi anayeingiza zinaweza kulindwa zaidi kuliko pale ambapo kondomu ya kiume inatumika. Hata hivyo, tazama tafiti hapa chini. Kuingiza kondomu ya kike hakuhitaji usimikaji wa uume. [12]
Hoja dhidi yake
[hariri | hariri chanzo]Inapotumika vizuri, kondomu ya kike inafeli kwa asilimia 5, la sivyo kwa asilimia 21 katika kuzuia mimba.[13]
Sababu zinaweza kuwa: kuwa na matundu, kuchanika, kuvikwa baada ya uume kugusa uke, kumwagika kwa shahawa wakati wa kuivua.[14]
Pamoja na kufeli kiasi hicho, watu wengi hawapendi kutumia kondomu hiyo kwa sababu inaweza:[15]
- ikatoa sauti isiyopendeza
- ikasababisha mwasho wa uke, uume au mkundu
- ikateleza ndani ya uke au mkundu
- ikapunguza ashiki[16]
Tena, wengine wanaona plastiki kama ukuta unaozuia umoja wa dhati kati ya wawili na kitu cha kigeni katika ulimwengu wa mapenzi, hivyo nafsi zao zinaikataa.
Wapo pia wanaopinga matumizi yake kwa misingi ya maadili na dini. Kwa mfano Wakatoliki wanatarajiwa kufanya tendo la ndoa katika ndoa tu, yaani katika muungano wa kudumu kati ya mwanamume na mwanamke, tena walifanye kwa namna isiyokwepa uzazi kwa kutumia teknolojia, ila sayansi (Uzazi wa mpango kwa njia asilia).
Uenezi kote duniani
[hariri | hariri chanzo]Mauzo ya kondomu za kike yamekuwa ya kutoridhisha katika nchi zilizoendelea, ingawa nchi hizo zinazidi kuzitumia ili kutimiza taratibu zilizopo za mpango wa uzazi na dhidi ya VVU / UKIMWI. [17]
Sababu ambazo huenda zinasababisha mauzo ya chini ni kuwa kuvaa kondomu ya kike ni ujuzi ambao mtu anapaswa kujifunza, na kondomu za kike ni ghali kuliko zile za kiume (bei ni mara 2 au 3 zaidi).
Aidha, ripoti za sauti ya "mchakarisho" wakati wa ngono huwafanya baadhi ya watu ambao huenda wangeitumia, kama asiye na kujulikana ya nje pete ambayo bado nje ya uke. [12]
Mnamo Novemba 2005, YWCA ulimwenguni ulitoa wito kwa wizara ya afya za kitaifa na wahisani wa kimataifa wakubali kununua kondomu za kike milioni 180 za kusambazwa kote duniani katika mwaka 2006, ikisema kuwa "kondomu za kike bado ndiyo chombo cha pekee cha kuzuia Virusi Vya UKIMWI (VVU) ambayo wanawake wanaweza kuanzisha na kudhibiti wenyewe", lakini bado wanawake katika nchi zinazoendelea hawazipati kwa urahisi kutokana na gharama kubwa ya 72¢ kwa kila moja. Ikiwa kondomu milioni 180 za kike zingeagizwa, bei ya kondomu ingetarajiwa kupungua hadi 22¢. [18]
Katika mwaka 2005, kondomu za kike milioni 12 zilisambazwa kwa wanawake katika nchi zinazoendelea. Kwa kulinganisha, kati ya kondomu bilioni 6 na 9 za kiume zilisambazwa mwaka huo. [18] Ni wazi kwamba biashara ni kubwa, kwa hiyo hata propaganda ni nyingi.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/004002.htm
- ↑ "Kondomu za kike kwa ngono ya tupu ya nyuma". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-08-30. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
- ↑ "Jinsi ya kuvaa kondomu ya kike (Kwa ngono ya tupu ya nyuma)" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-09-05. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
- ↑ "Bidhaa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2005-09-03. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
- ↑ 5.0 5.1 (PDF) Female Health Company Announces International Availability of Second - Generation Female Condom at Significantly Lower Price (Press release). Female Health Company. 29 Septemba 2005. Archived from the original on 2006-08-18. https://web.archive.org/web/20060818044051/http://www.femalehealth.com/InvestorRelations/investor_pressreleases/press_2005_09_21_2ndGenerationFC_Announcement.pdf. Retrieved 2006-08-03. (PDF)
- ↑ http://www.unfpa.org/hiv/female.htm
- ↑ Kondomu ya Kike
- ↑ "Kondomu ya kike ya PATH". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-01-22. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
- ↑ Habari za karibuni zaidi kutoka kwa WHO: Vya kuzingatiwa kuhusu utumiaji-upya wa kondomu ya kike
- ↑ "Utumiaji upya wa kondomu ya kike: kutathmini uadilifu wa miundo baada ya awamu nyingi za kusafisha, kukausha na kulainisha tena". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-29. Iliwekwa mnamo 2010-11-30.
- ↑ "The Product". FC & FC2 Female Condom. Female Health Company. 2005. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2005-09-03. Iliwekwa mnamo 2006-08-03.
- ↑ 12.0 12.1 Boston Women's Health Book Collective (2008). Our Bodies, Ourselves : A New Edition for a New Era. New York, NY: Touchstone. ISBN 0-7432-5611-5.
- ↑ "How Effective Are Female Condoms?". Planned Parenthood. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-11. Iliwekwa mnamo 2013-06-24.
- ↑ www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/004002.htm
- ↑ "What Are the Disadvantages of Female Condoms?". Planned Parenthood. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-06-11. Iliwekwa mnamo 2013-06-24.
- ↑ www.nlm.nih.gov/medlineplus/ency/article/004002.htm
- ↑ "Global Consultation on the Female Condom". Baltimore, MD: PATH. 26 to 29 Septemba 2005. Archived from the original on 2006-06-16. https://web.archive.org/web/20060616030553/http://www.path.org/projects/womans_condom_gcfc2005.php. Retrieved 2006-08-03.
- ↑ 18.0 18.1 Statement of Dr. Musimbi Kanyoro, General Secretary, World YWCA (Press release). PRNewswire. 21 Novemba 2005. http://www.prnewswire.co.uk/cgi/news/release?id=158769=. Retrieved 2006-08-03.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- "Female Condoms: Sexual Freedom Doesn't Come Free" Archived 25 Januari 2009 at the Wayback Machine.
- Mwongozo wa kina kuhusu utumiaji wa kondomu za kike Archived 30 Novemba 2010 at the Wayback Machine. Namna ya kutumia na kuondoa kondomu ya kike kwa usalama
- [1] Kuongeza upatikanaji wa Kimataifa wa kondomu za kike
- [2] Archived 19 Mei 2009 at the Wayback Machine. Kondomu za kike na jukumu la msaada kutoka Marekani kwa nchi za nje kadiri ya Kituo Cha Afya na Usawa wa Kijinsia (CHANGE)
- [3] "Vipi Femidom?" katika jarida la Guardian
- [4] Archived 22 Januari 2013 at the Wayback Machine. Kondomu ya kike ya PATH
- Namna ya kuvaa kondomu ya kike Archived 1 Februari 2009 at the Wayback Machine. Mwongozo wenye picha kutoka kwa wataalamu wa afya wa Kanada
- [5] Archived 11 Juni 2013 at the Wayback Machine. Kondomu ya kike kwa kupanga uzazi