Kanivali ya Karibi
Kanivali ya Karibi ni sherehe inayoadhimishwa kila mwaka katika Visiwa vya Karibi na kule ambako watu wa Karibi walihamia kama Marekani, Amerika Kusini, Kanada, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani.
Asili yake ilikuwa katika desturi za kanivali ya Wafaransa Wakatoliki na utamaduni uliotokea Trinidad na Tobago hasa baada ya uhuru wa watumwa kuanzia miaka ya 1840. Majira yake ni siku zilizopo kabla ya Jumatano ya Majivu na kipindi cha Kwaresima.
Kanivali ya Karibi hujulikana hasa kwa maandamano makubwa ambako watu hucheza barabarani wakisikiliza muziki wa Reggae au Calypso, na kuvaa mavazi mazuri na manyoya na mapambo sana.
Usuli
[hariri | hariri chanzo]Mamia ya miaka iliyopita, watu ambao walifuata dini ya Kikatoliki katika nchi ya Italia walianza desturi ya kwenda tamashani, kuvaa mavazi maalumu na ya ajabu, na kula na kunywa sana kabla ya Jumatano ya Majivu ambaye ni siku ya kuanza saumu ya Kikristo katika Kwaresima. Kwa sababu Wakatoliki hawakula nyama wakati wa Kwaresima waliita sherehe hizo kwa Kiitalia "carne vale" – ambayo inamaanisha “kwaheri nyama.” Kadiri muda ulivyopita, kanivali katika Italia ikawa maarufu, na mila ikaenea Ufaransa, Uhispania, na nchi zote za Kikatoliki katika Ulaya. Mwishowe, jinsi Wafaransa, Wahispania, na Wareno walivyoanza kutawala nchi katika Amerika, na mahali pengine duniani, walileta desturi zao kwa kuadhimisha kanivali.
Historia ya kiuchumi na kisiasa ya Kariba ilisaidia kuanzisha tamasha la kanivali kiasi kwamba hata sisi tunajua leo katika dayaspora ya Kiafrika na Kariba. Baada ya Kristoforo Kolumbus kusafiri bahari ya Karibi, mamilioni ya watumwa waliletwa katika visiwa vya.
Ushawishi juu ya Kanivali
[hariri | hariri chanzo]Kitu muhimu kwa tamasha la kanivali ni desturi kongwe ya Kiafrika ya kusanyika na kutembea kwa miduara kupita kijiji hadi kijiji wakati wamevaa mavazi na vinyago. Watu wengi walisema kwamba kuzunguka vijijini huleta bahati nzuri, huponya matatizo, na hutuliza wazee wenye hasira ambao walitangulia katika ulimwengu ujao. Utamaduni wa kanivali pia unatokana na mila ya Kiafrika ya kuunganisha vitu ya asili (kama vile, mifupa, majani, shanga, magamba ya bahari, vitambaa) kuumba vinyago, au mavazi – na kila kitu au muungano wa vitu ambavyo viliwakilisha wazo fulani au nguvu ya kiroho.
Manyoya yalikuwa yanatumika kwa Waafrika katika vinyago na vifuniko vya kichwa kama ishara ya uwezo za binadamu kushinda matatizo, maumivu, huzuni nyingi, magonjwa – kuhamia ulimwengu mwingine na kufufuka na kukua kiroho. Leo, manyoya hutumika katika namna nyingi kwa kutengenezea mavazi.
Pia, vibaraka wengi, wapiganaji fimbo, na wachezaji wa “stilt” walianza kuonekana katika matukio ya kanivali. Desturi ya dansi na muziki wa Kiafrika pia iligeuza mapema tamasha la kanivali katika Marekani ya kaskazini na kusini. Mahadhi ya ngoma za Kiafrika yaliathiri utengenezaji wa muziki, kama vile soca na calypso.
Maeneo
[hariri | hariri chanzo]Katika mahali tofauti duniani, ambapo Wakatoliki wa Ulaya walianzisha biashara ya watumwa na makoloni mapya, kanivali ilianza pia. Brazil ni maarufu sana kwa kanivali yake na ni moja ya kanivali kubwa katika eneo la Marekani Kusini. Kanivali huliadhimishwa pia katika: Barbados, Jamaika, Grenada, Dominika, Haiti, Kuba, St. Thomas, St. Maarten; katika Marekani katikati na kusini katika Belize, Panama, Brazil; katika maeneo ya Ulaya katika Uingereza, Uswizi, Ujerumani, na miji mikubwa katika Marekani ambapo watu wa Kariba waliishi, kama vile Brooklyn, Miami, Atlanta, Houston, Washington D.C., Baltimore, Hollywood na Toronto.
Hata hivyo, kanivali kubwa na maarufu zaidi hutokea katika visiwa cha Trinidad na Tobago. Kila mwaka mamia ya maelfu ya watu hukutana katika visiwa vidogo kuadhimisha siku ya kanivali, na kuna sikukuu, kama vile “J’ouvert,” ambayo ni sherehe ya asubuhi mapema kabla ya siku ya kanivali.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Baynes, M. E. (2021, October 5). Carnival: A Caribbean Tradition with Historical Roots. The Odyssey Online. Retrieved November 13, 2021, from https://www.theodysseyonline.com/experience-carnival-life.