Jumatano ya Majivu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
A priest marks a cross of ashes on a worshipper's forehead.
Mkristo akipakwa majivu siku hiyo.
Mwaka wa liturujia
Magharibi
Mashariki

Jumatano ya Majivu, katika kalenda ya mwaka wa Kanisa la Magharibi, ni siku ya kwanza ya kwaresima, walau kwa madhehebu mengi (katika liturujia ya Milano Kwaresima inaanza Jumapili inayofuata, hivyo majivu yanapakwa siku hiyo, si Jumatano).

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina linatokana na desturi katika Kanisa Katoliki ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka.

Mfungo[hariri | hariri chanzo]

Kwa kawaida siku hiyo unaanza mfungo wa siku 40 kabla ya sikukuu ya Pasaka. Kipindi hicho kinatunza kumbukumbu ya Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

Tarehe[hariri | hariri chanzo]

Tarehe ya Jumatano ya Majivu hutegemea ile ya Pasaka. Ni siku ya kufunga ya 40 kabla ya Pasaka; ilhali katika desturi hii siku za Jumapili hakuna kufunga, ni siku ya 46 kabla ya sikukuu, maana kuna Jumapili 6 ndani ya Kwaresima.

Tarehe ya mapema inayowezekana ni 4 Februari, tarehe ya mwisho inayoweza kutokea ni 10 Machi.

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jumatano ya Majivu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.