Kalisto (mwezi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kallisto (Mshtarii))
Upande wa Kalisto usiotazama Mshtarii.

Kalisto ni mwezi unaozunguka Mshtarii (Jupiter). Ni mwezi mkubwa wa pili baada ya Ganimedi unaozunguka sayari hiyo. Kipenyo chake kinalingana na kile cha sayari Utaridi (Mercury). Kati ya miezi minne mikubwa ya Mshtarii, Kalisto iko mbali zaidi na sayari hiyo ukiwa na umbali wa wastani wa km 1,889,999.

Kalisto ilitambuliwa mwaka 1610 na Galileo Galilei wakati huyu alipokuwa mtu wa kwanza kutumia darubini akiangalia nyota. [1]

Sawa na mwezi wa Dunia, mzunguko wa Kalisto kwenye mhimili wake unashikamana kabisa na muda wa obiti yake ("tidally locked"); kwa hiyo ni upande uleule unaoangalia sayari yake. [2]

Kalisto inafanywa kwa kiwango sawa na mwamba na barafu, na densiti ya wastani ni karibu 1.83   g / cm³. Kikemia kampaundi kwenye uso ni pamoja na barafu ya maji, dioksidi kabonia, silika, na kampaundi ogania. Kipimaanga "Galileo" kilipita karibu kikafanya uchunguzi wa mwezi, na kufunua kuwa Kalisto inaweza kuwa na kiini kidogo cha silika na labda pia tabaka la maji ya kiowevu lenye unene wa zaidi ya km 100. [3] [4]

Uso wa Kalisto umejaa kasoko zilizosababishwa na mapigo ya asteroidi. Hakuna dalili za michakato inayotokea chini ya uso kama vile matetemeko ya ardhi au volkeno. [5]

Kalisto imezungukwa na angahewa nyembamba sana inayofanywa na dioksidi kabonia na pengine molekuli chache za oksijeni. Kuna pia tabaka la ioni (ionosphere). [6]

Vipimaanga mbalimbali vimepita Kalisto, kuanzia "Pioneer 10" hadi "Galileo" na Cassini − Huygens vikapima mwezi huo. Kalisto inatazamwa kuwa mahali panapofaa kwa kuanzisha kituo kama wanadamu wanataka kufanya uchunguzi wa baadaye wa mfumo wa Mshtarii. [7]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Galilei, G.; Sidereus Nuncius Archived 23 Agosti 2009 at the Wayback Machine. (March 13, 1610)
  2. Cooper, John F. (2001). Johnson, Robert E.; Mauk, Barry H.; et al.. "Energetic ion and electron irradiation of the icy Galilean satellites". Icarus 139: 133–159. doi:10.1006/icar.2000.6498. Archived from the original on 2009-02-25. Retrieved 2019-12-18. 
  3. Kuskov, O.L.; Kronrod, V.A. (2005). "Internal structure of Europa and Callisto". Icarus 177: 550–369. doi:10.1016/j.icarus.2005.04.014. 
  4. Showman, Adam P.; Malhotra, Renu (1999). "The Galilean Satellites". Science 286. doi:10.1126/science.286.5437.77. Archived from the original on 2011-05-14. Retrieved 2019-12-18. 
  5. Greeley, R. (2000). Klemaszewski J.E.; Wagne, L. et al.. "Galileo views of the geology of Callisto". Planetary and Space Science 48: 829–853. 
  6. Kliore, A.J. (2002). Anabtawi, A; Herrera, R. G.; et al.. "Ionosphere of Callisto from Galileo radio occultation observations". Journal of Geophysics Research 107: 1407. doi:10.1029/2002JA009365. 
  7. Trautman (2003). Revolutionary concepts for human outer planet exploration (HOPE). Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-01-19. Iliwekwa mnamo 2019-12-18.

Maelezo ya chini