Cassini–Huygens

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
mchoro wa Cassini juu ya bangili za sayari Zohali

Cassini–Huygens ni chombo cha angani kilichotumwa na NASA na ESA kufanya utafiti wa sayari Zohali (Saturnus) na miezi yake hasa Titan. Chombo kina sehemu mbili:

  • Cassini ni sehemu inayoendelea kuzunguka sayari na miezi yake ikipiga picha na kupima mnururisho
  • Huygens ni chombo cha kufikia kwenye uso wa Titan.

Cassini-Huygens imepewa jina kutokana na wataalamu wawili. Hao ni wanaastronomia Mwitalia Giovanni Domenico Cassini na Mholanzi Christiaan Huygens waliokuwa watu wa kwanza kuifanyia Zohali utafiti katika historia. Chombo kilirushwa angani 15 Oktoba 1997 kikafikia obiti ya Zohali 1 Julai 2004. Sehemu ya Huygens iliachana na Cassini na kufika usoni wa Titan 14 Januari 2005 ambao iliweza kutuma data kwa dakika 72. Data hizi zilihusu hasa angahewa ya mwezi huu na machnganyiko wa elementi za kikemia ndani yake, halijoto na halihewa yake.

Cassini inaendelea kuzunguka sayari na miezi yake. Mwaka 2012 ilituma picha za kwanza za mito nje ya dunia yetu iliyotambuliwa kwenye mwezi Titan. Maziwa na mito ya Titan ni ya methani na hidrokaboni nyingine zinazotokea duniani kama gesi lakini kwenye baridi ya Titan hupatikana kama kiowevu. Cassini ilipiga picha za mto menye urefu wa kilomita 400. [1]


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]