Jumamosi kuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Sanamu maarufu ya Pietà ya Michelangelo iliyochongwa katika marumaru kuonyesha Bikira Maria akipakata maiti ya mwanae Yesu mara baada ya kifo chake.

Jumamosi kuu ni siku ya Juma kuu inayoadhimisha hasa pumziko la mwili wa Yesu Kristo kaburini kabla ya kufufuka mtukufu usiku wa Pasaka.

Tarehe yake inabadilikabadilika kila mwaka na hata mwaka uleule ni tofauti katika madhehebu ya Ukristo, hasa yanayofuata mapokeo ya mashariki na yale yanayofuata mapokeo ya magharibi.

Siku hiyo wafuasi wa Yesu wanatulia kimya wakitafakari matukio ya Ijumaa kuu na kujiandaa washangilie ufufuko wake kuanzia kesha la Pasaka hadi Jumapili ya Pentekoste siku 50 baadaye.

Majina katika lugha mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Jumamosi kuu inaitwa kwa namna tofauti katika lugha mbalimbali. Baadhi ya mifano ni kama ifuatavyo:

Lugha Jina Tafsiri
Kicheki Bílá sobota Jumamosi nyeupe
Kifaransa Samedi saint Jumamosi takatifu
Kihispania Sábado Santo Jumamosi takatifu
Kiholanzi Stille Zaterdag Jumamosi ya kimya
Kihungaria Nagyszombat Jumamosi kuu
Kiingereza Holy Saturday Jumamosi takatifu
Kiitalia Sabato Santo Jumamosi takatifu
Kijapani 聖土曜日 (Sei Doyoobi) Jumamosi takatifu
Kijerumani Karsamstag Jumamosi ya ombolezo
Kipolandi Wielka Sobota Jumamosi kuu
Kislovakia Biela sobota Jumamosi nyeupe