Charles de Foucauld

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Charles de Foucald)
Picha halisi ya Foucauld mwaka 1907 hivi.
Nyumba ya Charles de Foucauld, iliyojengwa mwaka 1911, juu ya Assekrem (mita 2780 juu ya usawa wa bahari).

Charles Eugène de Foucauld (Strasbourg, 15 Septemba 1858Tamanrasset, 1 Desemba 1916) alikuwa mmonaki na padri Mkatoliki kutoka Ufaransa aliyekwenda kuishi peke yake kati ya Watuareg wa Sahara katika nchi ya Algeria ya leo hadi alipouawa.

Papa Benedikto XVI alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Novemba 2005, Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 15 Mei 2022.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Desemba.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya uongofu wake mwishoni mwa Oktoba 1886, Charles alikuwa ofisa wa Jeshi la Ufaransa huko Moroko, alipoanza kuguswa na mambo ya dini.[1]

Mwaka 1890 alijiunga na Watrapisti lakini aliwaacha mwaka 1897 ili kufuata wito mwingine wa pekee zaidi.

Baada ya kuishi peke yake karibu na Waklara wa Nazareti, mwaka 1901 alipata upadirisho akaenda kuishi jangwani.

Aliuawa mwaka 1916 nje ya ngome aliyojenga ili kulinda Watuareg na anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mfiadini.

Ingawa akiwa hai hakupata wafuasi, mfano na maandishi yake vilichangia uanzishaji wa mashirika na vyama kadhaa duniani kote, kama vile Ndugu Wadogo wa Yesu, Dada Wadogo wa Yesu na Ndugu Wadogo wa Injili.


Maandishi[hariri | hariri chanzo]

  • Reconnaissance au Maroc, 1883-1884. 4 vols. Paris: Challamel, 1888.
  • Dictionnaire Touareg–Français, Dialecte de l'Ahaggar. 4 vols. Paris: Imprimerie nationale de France, 1951-1952.
  • Poésies Touarègues. Dialecte de l'Ahaggar. 2 vols. Paris: Leroux, 1925-1930.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Vicar. "Visitor information". Retrieved on 22 May 2013. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.