Chama cha Jamhuri cha Marekani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Chama_cha_Jamhuri_cha_Marekani
Chama_cha_Jamhuri_cha_Marekani

Chama cha Jamhuri cha Marekani (kwa Kiingereza “Republican Party” au "Grand Old Party") ni chama cha kisiasa nchini Marekani.

Kilianzishwa mwaka wa 1854 na tangu pale kikawa chama chenye nguvu kikigombeana na Chama cha Kidemokrasia.

Kulikuwa na Marais kumi na wanane kutoka Chama cha Jamhuri, kuanzia Abraham Lincoln (1861-1865) hadi George W. Bush (2001-2009).

Kuanzia tarehe 20 Januari 2017, Donald Trump atakuwa rais wa 19 kutoka chama hicho.