Abraham Lincoln

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Abrahamlincoln.jpg

Abraham Lincoln (12 Februari 180915 Aprili 1865) alikuwa Rais wa 16 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1861 hadi 1865. Alikuwa na Kaimu Rais wawili: kwanza Hannibal Hamlin, halafu Andrew Johnson aliyemfuata kama Rais Lincoln alipouawa.

Lincoln amejulikana kama rais upande wa kaskazini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani kati ya majimbo ya kaskazini dhidi ya shirikisho la kusini na kuunganisha taifa tena. Kwa hiyo hukumbukwa kama rais aliyeleta mwisho wa utumwa na uhuru kwa watumwa wa Marekani.