Andalusia
Andalusia (kwa Kihispania: Andalucía) ni jimbo la kujitawala (Kihisp.: comunidade autónoma) la Hispania katika kusini ya rasi ya Iberia. Mji mkuu ni Sevilla. Katika historia ni sehemu ya Hispania iliyowahi kutwaliwa na iliyotawaliwa kwa karne nyingi zaidi na Waarabu Waislamu.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Imepakana na majimbo ya Hispania ya Extremadura, Castilla-La Mancha na Murcia. Upande wa magharibi iko Ureno na upande wa kusini kuna pwani ya Mediteranea, Mlango wa Gibraltar pamoja na eneo la Kiingereza la Gibraltar na pwani ya Atlantiki.
Andalusia ina eneo la km² 87,268 (17,2 % ya Hispania yote) ambalo linakaliwa na watu milioni 8.
Mto mkubwa ni Guadalquivir na mlima mrefu ni Mulhacen (m 3,479).
Miji muhimu ni (idadi ya wakazi kwa mabano): Sevilla (705,000), Malaga (560,000), Cordoba, Granada, Almeria, Cadiz, Jaen, Huelva, Jerez na Marbella.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Andalusia ni eneo la pekee kutokana na historia yake. Iliwahi kutawaliwa na nchi za nje tangu zama za kale. Wafinisia walikuwa na koloni hapa, Waroma wa Kale waliingiza eneo lote katika Dola la Roma wakifuatwa na Wavandali halafu na Wavisigothi waliojenga hapa ufalme wao.
Mwaka 711 Waarabu na Waberber Waislamu walivamia Hispania kwa kuvuka mlango wa Gibraltar na kuanzisha utawala wao katika sehemu kubwa za rasi ya Iberia uliokwisha mwaka 1492. Kati ya maeneo yote ya Hispania ni Andalusia iliyokaa muda mrefu chini ya utawala wa Kiislamu. Eneo lote chini ya utawala wa Kiislamu likaitwa "Al-Andalus" na Andalusia ya leo ilikuwa kiini chake.
Utamaduni wa Andalusia uliathiriwa sana na karne hizo chini ya Uislamu. Cordoba ikawa kwa sehemu kubwa ya wakati ule mji mkuu wa utawala wa nchi ikawa mji mkubwa wa Ulaya. Vyuo vikuu vya Andalusia vikawa vitovu vya elimu ambako wataalamu wa Ulaya, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi walikutana. Hata uchumi ulistawi.
Kati ya mabaki ya kipindi hicho ni majengo kama Alhambra wa Granada, majina ya kijiografia kama mto Guadalquivir (kutoka Kiarabu الوادي الكبير "wadi al kabir" yaani mto mkubwa) na muziki wa Andalusia.
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Jimbo la Andalusia huwa na mikoa 8. Mahakama hufanya kazi kwenye msingi wa maeneo ya korti kwa jumla ni 125 katika Andalusia.
Jimbo | Makao makuu | Wakazi | Densiti | Idadi ya manisipaa | Maeneo ya korti |
---|---|---|---|---|---|
Almería | Almeria | ||||
Cádiz | Cádiz | ||||
Córdoba | Cordoba | ||||
Granada | Granada | ||||
Huelva | Huelva | ||||
Jaén | Jaén | ||||
Málaga | Málaga | ||||
Seville | Seville |
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Andalusia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |