Nenda kwa yaliyomo

Aina ya damu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kielelezo cha aina za damu.

Aina ya damu (pia huitwa kikundi cha damu) ni uainishaji wa damu kwa kuzingatia kuwepo au kutokuwepo kwa dutu za antijeni za kurithiwa kwenye uso wa chembechembe nyekundu za damu (RBCs).

Antijeni hizo zinaweza kuwa protini, kabohaidreti, glikoprotini au glikolipidi, kutegemeana na mfumo wa aina ya damu.

Baadhi ya antijeni hizo pia zinapatikana kwenye uso wa aina nyingine za seli za tishu mbalimbali. Baadhi ya hizi antijeni za juu za chembechembe nyekundu za damu zinazotoka kwenye aleli moja (au jeni zinazohusiana), kwa pamoja huunda mfumo wa aina ya damu. [1] Aina za damu hurithiwa na huwakilisha michango kutoka kwa wazazi wote wawili. Jumla ya mifumo 30 ya aina ya damu ya binadamu inatambuliwa na Shirika la Kimataifa la Utoaji wa Damu (ISBT) hadi sasa. [2]

Wanawake wengi wajawazito hubeba mimba yenye aina ya damu tofauti na yao, na mama huweza kutengeneza kingamwili dhidi ya chembechembe nyekundu za damu za mimba. Wakati mwingine kingamwili hizi za mama ni IgG, imunoglobulini ndogo, ambayo inaweza kuvuka kondo na kusababisha hemolosia ya chembechembe nyekundu za damu, ambayo kwa upande mwingine inaweza kusababisha ugonjwa wa hemolitiki wa mtoto mchanga, ugonjwa wa hesabu ya chini ya damu ya mimba unaoweza kuwa hafifu au kali. [3]

Mifumo ya aina ya damu[hariri | hariri chanzo]

[2] Aina ya damu kamili ni seti ya dutu 30 kwenye uso wa chembechembe nyekundu za damu, na aina ya damu ya mtu ni mojawapo ya miungano iwezekanayo ya antijeni za aina ya damu. Katika aina hizo 30 za damu, zaidi ya antijeni 600 tofauti za aina ya damu zimepatikana, [4] lakini nyingi kati ya hizi ni za nadra sana au kwa kiasi kikubwa hupatikana katika makabila fulani tu.

Karibu kila mara, mtu ana aina moja ya damu maisha yake yote, lakini mara chache sana aina hubadilika kwa sababu ya mtu kuongezewa damu au kwa ukandamizaji wa antijeni katika maambukizi, donda ndugu, au ugonjwa kingamwilinafsi. [5] [6] [7] [8] Mfano wa jambo hili nadra ni kesi ya Demi-Lee Brennan, raia wa Australia, ambaye aina yake ya damu ilibadilika baada ya kuatikwa ini. [9] [10] Sababu nyingine ya kawaida ya mabadiliko ya aina ya damu ni uatikwaji wa uboho ambao hutekelezwa kwa lukemia na limfoma, miongoni mwa magonjwa mengine. Mtu akipokea uboho kutoka kwa mtu ambaye ana aina tofauti ya ABO (k.m. mgonjwa wa aina A anapokea uboho wa aina O), hatimaye damu ya mgonjwa itabadilika kuwa ya aina ya changizi.

Aina nyingine za damu uhusishwa na urithi wa magonjwa; kwa mfano, antijeni ya Kell mara nyingine huhusishwa na ugonjwa wa McLeod. [11] Baadhi ya aina za damu zinaweza kuathiri wepesi wa maambukizo, mfano ukiwa upinzani kwa aina maalum za malaria zinazoonekana katika watu wenye ukosefu wa antijeni ya Duffy. [12] Antijeni ya Duffy, inakisiwa kwa sababu ya uteuzi asilia, si ya kawaida katika makabila kutoka maeneo yenye matukio mengi ya malaria. [13]

Mfumo wa aina ya damu wa ABO[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa aina ya damu wa ABO: mchoro unaonyesha minyororo ya kabohaidreti ambayo huamua kikundi cha damu cha ABO

Mfumo wa ABO ni mfumo muhimu zaidi wa aina ya damu katika kuongezewa damu kwa binadamu. Kingamwili kinza-A na kingamwili kinza-B zinazohusika kwa kawaida ni kingamwili za Imunoglobulini M, inayofupishwa IgM. Kingamwili za ABO IgM hutengenezwa katika miaka ya kwanza ya maisha kwa wepesi wa kuhisi dutu za mazingira kama vile chakula, bakteria na virusi. O kwenye ABO mara nyingi huitwa 0 (sifuri au kapa) katika lugha nyingine. [14]

Fenotaipu Aina-jeni
A. AA au AO
B BB au BO
AB AB
O OO

Mfumo wa aina ya damu wa Rh[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa Rh ni mfumo wa pili muhimu zaidi wa aina ya damu katika kuongezewa damu kwa binadamu ukiwa na antijeni 50 kwa sasa. Antijeni ya Rh iliyo muhimu zaidi ni ile ya D kwa sababu huenda ikachochea mkarara wa mfumo wa kinga wa Antigeni tano kuu za Rh. Ni kawaida kwa watu wenye D-hasi kutokuwa na kingamwili kinza-D IgG au IgM, kwa sababu kwa kawaida, kingamwili kinza-D hazitengenezwi kwa wepesi wa kuhisi dhidi ya dutu za mazingira. Hata hivyo, watu wenye D-hasi wanaweza kutengeneza kingamwili kinza-D za IgG kufuatia tukio la uhamasishaji: labda kupewa damu kutoka kwa kijusi hadi kwa mama wakati wa ujauzito au mara chache kupewa damu na chembechembe nyekundu za damu [15]za D chanya. Ugonjwa wa Rh unaweza kutokea katika hali hizi. [16] Aina za damu zenye Rh hasi ni chache kwa uwiano wa idadi ya watu wa Asia (0.3%) kuliko zilivyo kwenye idadi ya watu weupe (15%). [17] Katika jedwali lililo hapa chini, kuwepo au kutokuwepo kwa antijeni za Rh kunaashiriwa kwa ishara ya + au - , ili kwa mfano aina ya A- haina antijeni zozote za Rh.

ABO na uenezi wa Rh nchi kwa nchi[hariri | hariri chanzo]

ABO na uenezaji wa aina ya damu wa Rh kwa taifa (wastani ya idadi ya watu)
Nchi Idadi ya Watu[18]  O +  A+  B + AB +  O-  A-  B- AB-
Australia [19] 21,262,641 40% 31% 8% 2% 9% 7% 2% 1%
Austria [20] 8,210,281 30% 33% 12% 6% 7% 8% 3% 1%
Ubelgiji [21] 10,414,336 38% 34% 8.5% 4.1% 7% 6% 1.5% 0.8%
Brazil [22] 198,739,269 36% 34% 8% 2.5% 9% 8% 2% 0.5%
Kanada [23] 33,487,208 39% 36% 7.6% 2.5% 7% 6% 1.4% 0.5%
Denmaki 5,500,510 35% 37% 8% 4% 6% 7% 2% 1%
Estonia [24] 1,299,371 30% 31% 20% 6% 4.5% 4.5% 3% 1%
Ufini [25] 5,250,275 27% 38% 15% 7% 4% 6% 2% 1%
Ufaransa [26] 62,150,775 36% 37% 9% 3% 6% 7% 1% 1%
Ujerumani [27] 82,329,758 35% 37% 9% 4% 6% 6% 2% 1%
Hong Kong SAR 7,055,071 10% 26% 27% 7% 0.31% 0.19% 0.14% 0.05%
Aisilandi [28] 306,694 47.6% 26.4% 9.3% 1.6% 8.4% 4.6% 1.7% 0.4%
India [29] 1,166,079,217 36.5% 22.1% 30.9% 6.4% 2.0% 0.8% 1.1% 0.2%
Ayalandi [30] 4,203,200 47% 26% 9% 2% 8% 5% 2% 1%
Israeli [31] 7,233,701 32% 34% 17% 7% 3% 4% 2% 1%
Uholanzi [32] 16,715,999 39.5% 35% 6.7% 2.5% 7.5% 7% 1.3% 0.5%
New Zealand [33] 4,213,418 38% 32% 9% 3% 9% 6% 2% 1%
Norwe [34] 4,660,539 34% 42.5% 6.8% 3.4% 6% 7.5% 1.2% 0.6%
Polandi [35] 38,482,919 31% 32% 15% 7% 6% 6% 2% 1%
Ureno [36] 10,707,924 36.2% 39.8% 6.6% 2.9% 6.0% 6.6% 1.1% 0.5%
Saudi Arabia [37] 28,686,633 48% 24% 17% 4% 4% 2% 1% 0.23%
Afrika Kusini [38] 49,320,000 39% 32% 12% 3% 7% 5% 2% 1%
Hispania [39] 40,525,002 36% 34% 8% 2.5% 9% 8% 2% 0.5%
Uswidi [40] 9,059,651 32% 37% 10% 5% 6% 7% 2% 1%
Taiwan [41] 24,000,000 43.9% 25.9% 23.9% 6.0% 0.1% 0.1% 0.01% 0.02%
Uturuki [42] 76,805,524 29.8% 37.8% 14.2% 7.2% 3.9% 4.7% 1.6% 0.8%
Uingereza [43] 61,113,205 37% 35% 8% 3% 7% 7% 2% 1%
Marekani [44] 307,212,123 37.4% 35.7% 8.5% 3.4% 6.6% 6.3% 1.5% 0.6%
Wastani wa idadi ya watu (Jumla ya idadi ya watu = 2,261,025,244) 36.44% 28.27% 20.59% 5.06% 4.33% 3.52% 1.39% 0.45%

(| Darasa = "jedwali la wiki linaloweza kuporomoka kuporomoka"! Usambazaji wa ABO kirangi na kikabila (bila RH) damu aina [45]
(meza hii ina ingizo zaidi kuliko meza iliyo juu lakini haitofautishi kati ya aina za Rh <). / ndogo > | - | (| darasa = "jedwali la wiki lililopangika" | -! upana = 200 | Watu kundi! upana = 70 | O (%)! width = 70 | A% ()! upana= 70 | B (%)! upana = 70 | AB (%) | -

Waaborijini 61 39 0 0


Wahabeshi 43 27 25 5
Ainu (Japani) 17 32
32 18
Waalbania 38
43 13 6
Waandamania Wakuu 9 60 23 9
Waarabu 34 31 29 6
Waamenia 31 50 13 6
Wa-Asia (Marekani - kwa jumla) 40 28 27 5
Wa-Austria 36 44 13 6
Wabantu 46 30 19 5
Wabaski 51 44 4 1
Wabelgiji 47 42 8 3
Blackfoot (Wahindi wa Amerika Kaskazini) 17 82 0 1
Wabororo (Brazil) 100 0 0 0
Wabrazili 47 41 9 3


Wabulgaria 32 44 15 8
Wabama 36 24
33 7
Waburyat (Saiberia) 33
21 38 8
Bushmen
56 34 9 2
Wakantoni wa Kichina
46 23 25 6
Wapeking wa Kichina
29 27 32 13
Wachuvashi
30 29 33 7
Wacheki
30 44 18 9
Wadeni
41 44 11 4
Waholanzi
45 43 9 3
Wamisri
33 36 24 8
Waingereza
47 42 9 3
Waeskimo (Alaska)
38 44 13 5
Waeskimo (Grinlandi)
54 [47] 23 8
Waestonia
34 36 23 8
Wafiji
44 34 17 6
Wafini
34 41 18 7
Wafaransa
43 47 7 3
Wajojia
46 37 12 4
Wajerumani
41 43 11 5
Wagiriki
40 42 14 5
Wajipsi (Hungaria)
29 27 35 10
Wahawaii
37 61 2 1
Wahindi (Bombay) 32 29 28 11
Wahungaria 36 43 16 5


Waaisilandi 56 32 10
3
Wahindi (India-jumla) 37 22
33 7
Wahindi (Marekani-jumla) 79
16 4 1
Waayalandi
52 35 10 3
Waitaliano (Milan)
46 41 11 3
Wajapani
30 38 22 10
Wayahudi (Ujerumani)
42 41 12 5
Wayahudi (Polandi)
33 41 18 8
Wakalmuk
26 23 41 11
Wakikuyu (Kenya)
60 19 20 1
Wakorea 28 32 31 10


Walapp 29 63 4
4
Walatvia 32 37
24 7
Walitwania 40
34 20 6
Wamalesia
62 18 20 0
Wamaori
46 54 1 0
Wamaya
98 1 1 1
Wamoro
64 16 20 0
Mnavajo (Mhindi wa Amerika Kaskazini)
73 27 0 0
Mnikoba (Wanikoba) 
74 9 15 1
Wanorwe
39 50 8 4
Wapapua (Guinea Mpya)
41 27 23 9
Waajemi
38 33 22 7
Peru (Wahindi)
100 0 0 0
Wafilipino
45 22 27 6
Wapoli
33 39 20 9
Wareno
35 53 8 4
Waromania
34 41 19 6
Warusi
33 36 23 8
Wasardini
50 26 19 5
Waskoti
51 34 12 3
Waserbia
38 42 16 5
Shompeni (Wanikoba)
100 0 0 0
Slovaks
42 37 16 5
Waafrika Kusini
45 40 11 4
Wahispania
38 47 10 5
Wasudani
62 16 21 0
Waswidi
38 47 10 5
Waswisi
40 50 7 3
Watata
28 30 29 13
Watai
37 22 33 8
Waturuki
43 34 18 6
Wayukraini
37 40 18 6
Marekani (Wamarekani weusi)
49 27 20 4
Marekani (Wamarekani wazungu)
45 40 11 4
Wavietnamu 42 22 30 5
Wastani 43.91 34.80 16.55 5.14
Mchepuko wa kiwango 16.87 13.80 9.97 3.41


|)

Damu ya aina B inapatikana zaidi Kaskazini mwa India na Asia ya Kati, na hupungua kuelekea magharibi na mashariki hadi kufikia asilimia za tarakimu moja tu nchini Hispania. [46] [47] Inaaminika kuwa haikuwepo kabisa katika wakazi asili wa Amerika na wa Australia kabla ya kufika kwa Wazungu katika maeneo hayo. [47] [48]

Damu ya aina A inarudiarudia Ulaya, hasa katika nchi za Skandinavia na Ulaya ya Kati, ingawa marudio ya juu zaidi hutokea katika wakazi asili wa Australia na Waindio Blackfoot wa Montana. [49] [50]

Mifumo mingine ya aina ya damu[hariri | hariri chanzo]

Shirika la Kimataifa la Utoaji Damu sasa linatambua mifumo 30 ya aina ya damu (ikiwa ni pamoja na mifumo ya ABO na Rh). [2] Hivyo, pamoja na antijeni ya ABO na antijeni ya Rh, antijeni nyingine nyingi zinaonyeshwa kwenye utando wa uso wa chembechembe nyekundu za damu. Kwa mfano, mtu anaweza kuwa AB, D chanya, na wakati huo huo M na N chanya (mfumo wa MNS), K chanya (mfumo wa Kell), Le a au Le b hasi (mfumo wa Lewis), na kadhalika, kuwa chanya au hasi kwa antijeni ya kila mfumo wa aina ya damu. Mifumo mingi ya aina ya damu ilipewa majina ya wagonjwa waliopatikana na kingamwili inayotangamana kwanza.

Umuhimu wa kimatibabu[hariri | hariri chanzo]

Kuongezewa damu[hariri | hariri chanzo]

Matibabu ya kuongeza damu ni tawi maalumu la hematolojia linalohusu masomo ya aina za damu, pamoja na kazi ya hifadhi ya damu kutoa huduma ya kuongezewa damu na bidhaa nyingine za damu. Duniani kote, bidhaa za damu ni lazima ziagizwe na daktari au daktari mpasuaji mwenye leseni kwa hali sawa kama dawa.

Dalili kuu ya mmenyuko hatari wa hemolitiki kutokana na damu zisizoambatana. Hitilafu ya kutaja: Closing </ref> missing for <ref> tag

Kazi nyingi ya kawaida ya hifadhi ya damu inahusisha kupima damu kutoka kwa watoaji damu na wapokeaji kuhakikisha kuwa kila mpokeaji anapewa damu iliyo patanifu na salama iwezekanavyo. Ikiwa kiasi cha damu isiyowiana inabadilishwa baina ya mtoaji damu na mpokeaji, mmenyuko mkali na hatari wa hemolitiki kwa hemolosia (uharibifu wa chembechembe nyekundu za damu), mafigo kushindwa kufanya kazi na mshtuko huenda yakatokea, na kifo kinawezekana. Kingamwili zinaweza kuwa hai sana na zinaweza kushambulia chembechembe nyekundu za damu na kugandisha vipengele vya mfumo saidishi na kusababisha hemolosia nyingi ya damu iliyoongezwa.

Ni bora kwa wagonjwa kupokea damu yao wenyewe au bidhaa za damu maalum za aina yao kupunguza nafasi za mmenyuko wa kuongezewa damu. Hatari inaweza kupunguzwa zaidi kwa ulinganisho wa pamoja wa damu, lakini hii inaweza kurukwa wakati damu inahitajika kwa dharura. Ulinganisho wa pamoja huhusisha kuchanganya sampuli ya majimaji ya damu ya mpokeaji na sampuli ya chembechembe nyekundu za damu ya mtoaji damu na kuangalia ikiwa mchanganyiko unashikamana, au unaunda mafungu. Ikiwa kushikamana si dhahiri kwa kuangalia moja kwa moja, mafundi wa hifadhi ya damu huangalia kushikamana kwa hadubini. Kushikamana kukitokea, damu ya mtoaji damu hiyo haiwezi kuongezwa kwa mpokeaji husika. Katika hifadhi ya damu ni muhimu kutambua sampuli zote za damu kwa usahihi, kwa hiyo utambulisho umesanifishwa kwa kutumia mfumo wa msimbo mkuo unaojulikana kama ISBT (Kipimo cha jumla cha utambulisho na utengenezaji wa taarifa za bidhaa za damu, tishu na viungo vya binadamu) 128.

Aina ya damu inaweza kujumuishwa kwenye tagi za utambulishaji au kwenye michoro inayovaliwa na wafanyakazi wa kijeshi, ikiwa watahitaji kuongezwa damu kwa dharura. Mjerumani wa mstari wa mbele Waffen-SS alikuwa na michoro yenye aina ya damu wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Aina za damu za nadra zinaweza kusababisha matatizo ya upatikanaji kwa hifadhi za damu na hospitali. Kwa mfano damu ya Duffy-hasi hupatikana zaidi katika watu wa asili ya Kiafrika, [51] na uadimifu wa aina hii ya damu katika watu wengine unaweza kusababisha upungufu wa damu ya Duffy-hasi kwa wagonjwa Waafrika. Vilevile kwa watu wenye RhD hasi, kuna hatari inayohuhusishwa na kusafiri hadi sehemu za dunia ambapo upatikanaji wa damu ya RhD hasi ni nadra, hasa Asia ya Mashariki, ambapo huduma za damu zinaweza kujitahidi kuhimiza wenyeji wa magharibi kuchangia damu. [52]

Ugonjwa wa hemolitiki wa watoto wachanga (HDN)[hariri | hariri chanzo]

Mwanamke mjamzito anaweza kutengeneza kingamwili za aina ya damu ya IgG ikiwa mimba yake ina antijeni ya damu ambayo yeye hana. Hii inaweza kutokea ikiwa baadhi ya seli za damu za mimba zitaingia katika mzunguko wa damu ya mama yake (kwa mfano kutokwa damu kidogo kati ya mimba na mama wakati wa kujifungua au kuingiliwa kwa ukunga), au mara nyingine baada ya kuongezewa damu. Hii inaweza kusababisha maradhi ya Rh au aina nyingine ya ugonjwa wa hemolitiki wa watoto wachanga (HDN) katika mimba ya sasa na / au zile zitakazofuata. Ikiwa mjamzito anajulikana kuwa na kingamwili za kinza-D, aina ya damu ya Rh ya mimba inaweza kupimwa kwa uchambuzi wa DNA katika plazma ya mama kutathmini hatari ya ugonjwa wa Rh kwa mimba. [53] Moja kati ya maendeleo makubwa ya udaktari wa karne ya 20 ilikuwa kuzuia ugonjwa huu kwa kusimamisha uundaji kingamwili za kinza-D na mama wenye D hasi kwa kutumia dawa ya sindano inayoitwa Rho (D) globulini ya kinga. [54] [55] Kingamwili zinazohusishwa na baadhi ya vikundi vya damu zinaweza kusababisha HDN kali, nyingine zinaweza kusababisha HDN pole na nyingine hazisababishi HDN. [3]

Bidhaa za damu[hariri | hariri chanzo]

Kutoa faida ya juu zaidi kwa kila uchangiaji wa damu na kuhakikisha haitaharibika, hifadhi za damu hugawanya damu fulani nzima katika bidhaa kadhaa. Bidhaa za kawaida ni chembechembe nyekundu za damu, plazma, chembe za kugandisha damu, bidhaa ya damu iliyoganda inayotengenezwa kutoka kwa plazma, na plazma-bichi iliyoganda (FFP). FFP inagandishwa haraka kuhifadhi vigandiza damu vya V na VIII vya kukubali mabadiliko, ambavyo kwa kawaida hutolewa kwa wagonjwa ambao wana uwezekano wa tatizo hatari la kuganda damu linalosababishwa na hali kama vile ugonjwa wa kuzidi kuharibika kwa ini, kuzidisha kiasi cha kinza-mgando damu, au mgando wa damu unaosambazwa (DIC)

Vitengo vya chembechembe nyekundu zilizowekwa pamoja vinatengenezwa kwa kuondoa plazma nyingi iwezekanavyo kutoka kwenye vitengo vya damu nzima.

Vigandiza damu vilivyosanisiwa na mbinu za kisasa za seli zilizoungana tenasasa zinatumika kwa kawaida katika matibabu ya hemofilia, kwa sababu hatari za kuambukiza maambukizi zinazotokana na bidhaa za damu zilizowekwa pamoja huepukwa.

Upatanifu wa chembechembe nyekundu za damu[hariri | hariri chanzo]

 • Watu wenye damu ya aina ya AB wana antijeni zote mbili za A na B kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu, na majimaji yao ya damu hayana kingamwili zozote dhidi ya antijeni A au B. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya AB anaweza kupokea damu aina yoyote (aina ya AB inapendekezwa), lakini anaweza kutoa damu kwa mtu mwingine mwenye aina ya AB pekee.
 • Watu wenye damu ya aina ya A wana antijeni ya A kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu, na majimaji yao ya damu yana kingamwili za IgM dhidi ya antijeni ya B. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya A anaweza kupokea damu kutoka kwa watu wenye aina ya A au O pekee (aina ya A ikipendekezwa), na anaweza kutoa damu kwa watu wengine wenye aina ya A au AB.
 • Watu wenye damu ya aina ya B wana antijeni ya B kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu, na majimaji yao ya damu yana kingamwili za IgM dhidi ya antijeni ya A. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya B anaweza kupokea damu kutoka kwa watu wenye aina ya B au O (aina ya B ikipendekezwa), na wanaweza kutoa damu kwa watu wenye aina ya B au AB.
 • Watu wenye damu ya aina ya O (au kikundi cha damu cha sifuri katika nchi kadhaa) watu hawana antijeni A au B kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu, lakini majimaji yao ya damu yana kingamwili kinza-A na kingamwili kinza-B za IgM dhidi ya antijeni za aina ya damu za A na B. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya O anaweza tu kupokea damu kutoka kwa mtu mwenye aina ya O, lakini anaweza kutoa damu kwa watu wa aina yoyote ya ABO (yaani A, B, O au AB). Ikiwa mtu anahitaji kuongezewa damu kwa dharura sana, na kama muda utakaochukuliwa kuikagua damu ya mpokeaji utasababisha kuchelewa kwenye madhara, damu ya O Hasi inaweza kutolewa.
Cheti cha Upatanifu wa chembechembe nyekundu za damu. Mbali na kuchangia kwa kikundi kimoja cha damu; watoaji damu wa aina ya O wanaweza kuwatolea wale wa A, B na AB; watoaji damu wa aina ya A na B wanaweza kuwatolea wale wa AB.
Jedwali la upatanifu wa chembechembe nyekundu za damu
[56][57]
Mpokeaji [1] Mtoaji damu [1]
O- O + A- A+ B- B + AB- AB +
O- Green tickY style = "width: 3em"
O + Green tickY Green tickY
A- Green tickY Green tickY
A+ Green tickY Green tickY Green tickY Green tickY
B- Green tickY Green tickY
B + Green tickY Green tickY Green tickY Green tickY
AB- Green tickY Green tickY Green tickY Green tickY
AB + Green tickY Green tickY Green tickY Green tickY Green tickY Green tickY Green tickY Green tickY

Muhtasari wa jedwali
1. Linaamini ukosefu wa kingamwili zisizo za kawaida ambazo zingesababisha kutokaribiana kati ya mtoaji damu na mpokezi, kama ilivyo kawaida kwa damu iliyochaguliwa kwa ulinganisho wa pamoja.

Mgonjwa mwenye Rh ya D-hasi ambaye hana kingamwili zozote za kinza-D (hajawahi kamwe kuhamasishwa kwa chembechembe nyekundu za damu za D chanya) anaweza kuongezewa damu ya D-chanya mara moja, lakini hii itasababisha wepesi wa kuhisi kwa antijeni ya D, na mwanamke mgonjwa atakuwa katika hatari ya ugonjwa wa hemolitiki wa mtoto mchanga. Ikiwa mgonjwa mwenye D-hasi amekuza kingamwili za kinza-D, mfichuo wa baadaye kwa damu ya D-chanya unaweza kusababisha mmenyuko unaoweza kuwa hatari wa kuongezewa damu. Damu ya Rh D-chanya kamwe haifai kutolewa kwa wanawake wenye umri wa kuzaa au kwa wagonjwa wenye kingamwili za D, kwa hivyo hifadhi za damu zinafaa kuhifadhi damu ya Rh-hasi kwa wagonjwa hawa. Katika hali zilizokithiri, kama vile kutokwa na damu nyingi wakati akiba ya vitengo vya damu ya D-hasi damu ni ndogo sana katika benki ya damu, damu ya D-chanya inaweza kutolewa kwa wanawake wenye D-hasi waliozidi umri wa kuzaa watoto au wanaume wenye Rh-hasi, ikiwa hawakuwa na kingamwili za kinza-D, kuhifadhi akiba ya damu ya D-hasi katika benki ya damu. Kinyume chake si kweli; wagonjwa wenye Rh D-chanya hawaathiriwi na damu ya D hasi. Ulinganisho sawa unafanywa kwa antijeni zingine za mfumo wa Rh kama vile C, c, E na e na kwa mifumo miingine ya aina ya damu iliyo na hatari inayojulikana kwa kupewa kingamaradhi kama vile mfumo wa Kell hasa kwa wanawake wenye umri wa kuzaa watoto au wagonjwa wenye haja inayojulikana ya kuongezewa damu mara nyingi.

Upatanifu wa Plazma[hariri | hariri chanzo]

Faili:Plasma-donation.svg
Cheti cha Upatanifu wa plazma. Mbali na kuchangia kwa kikundi kimoja cha damu; plazma kutoka kwa damu ya aina ya AB inaweza tolewa kwa wale wa A, B na O; plazma kutoka kwa damu ya aina za A na B inaweza kutolewa kwa wale wa aina ya O.

Wapokeaji wanaweza kupokea plazma za aina moja ya damu, lakini vinginevyo upatanifu wa mtoaji damu-mpokeaji kwa plazma ya damu ni kinyume cha ule wa chembechembe nyekundu za damu: plazma iliyoondolewa katika aina ya damu ya AB inaweza kuongezwa kwa watu wenye aina yoyote ya damu; watu wenye aina ya damu O wanaweza kupokea plazma kutoka kwa aina yoyote ya damu; na plazma ya aina ya O inaweza kutumiwa na wapokeaji wenye aina ya O pekee.

Jedwali la upatanifu wa plazma
[57]
Mpokeaji Mtoaji damu [1]

! mtindo = "upana: 3em" | O ! mtindo = "upana: 3em" | A ! mtindo = "upana: 3em" | B ! mtindo = "upana: 3em" | AB | - ! O | Green tickY | Green tickY | Green tickY | Green tickY | - ! A | | Green tickY | | Green tickY | - ! B | | | Green tickY | Green tickY | - ! AB | | | | Green tickY |)

Ukumbusho wa jedwali
1. Linaamini ukosefu wa kingamwili kali zisizo za kawaida katika plazma ya mtoaji damu

Kingamwili za Rh D sio za kawaida, kwa hivyo kwa ujumla wala damu ya D hasi au ya D chanya ina kingamwili za kinza-D. Ikiwa mtoaji damu atapatikana kuwa na kingamwili za kinza-D au kingamwili yoyote kali ya aina ya damu isiyo ya kawaida kwa uchunguzi wa kingamwili katika hifadhi ya damu, hatakubaliwa kama mtoaji damu (au katika hifadhi zingine damu itatolewa lakini bidhaa itahitajika kutambulishwa ipasavyo); kwa hivyo, plazma ya damu ya mtoaji damu inayotolewa na hifadhi ya damu inaweza kuchaguliwa ili isiwe na kingamwili za D na isiwe na kingamwili zingine zisizo za kawaida, na plazma kama hii ya mtoaji damu ilyotolewa na hifadhi ya damu inaweza kufaa kwa mpokeaji anayeweza kuwa D chanya au D hasi, mradi plazma ya damu na mpokeaji wana upatanifu wa ABO. [onesha uthibitisho]

Watoaji damu bia na wapokeaji damu bia[hariri | hariri chanzo]

Msaidizi wa hospitali aliye na Kikundi cha Utoaji Damu kutoka Portsmouth Naval Hospital anachukua sampuli za damu kutoka kwa watoaji kwa ajili ya kupima

Kuhusu kuongezewa damu nzima au chembechembe nyekundu za damu zilizowekwa pamoja, watu wenye damu ya aina ya O Rh D hasi mara nyingi huitwa watoaji damu bia, na wale walio na aina ya damu ya AB Rh D chanya huitwa wapokeaji damu bia; hata hivyo, masharti haya ni kweli kwa kawaida kuhusu mmenyuko wa kingamwili za kinza-A na kinza-B za mpokeaji kwa chembechembe nyekundu za damu zilizoongezwa, na pia uwezekano wa wepesi wa kuhisi kwa antijeni za Rh D. Kikundi kimoja kisichokuwa cha kawaida ni watu walio na mfumo wa antijeni wa HH (pia unajulikana kama aina ya damu ya Bombay) ambao wanaweza tu kupokea damu salama kutoka kwa watoaji damu wa hh, kwa sababu wanaunda kingamwili dhidi ya dutu ya H. [58] [59]

Watoaji damu wenye kingamwili kali za kinza-A, kinza-B au aina yoyote ya damu isiokawaida hutengwa kutoka kwa uchangiaji wa damu. Mimenyuko inayowezekana ya kingamwili za kinza-A na kinza-B zinazopatikana katika damu iliyoongezwa kwa chembechembe nyekundu za damu za mpokeaji lazima isizingatiwe, kwa sababu kiasi kidogo cha plazma iliyo na kingamwili inaongezwa.

Kwa mfano: tukizingatia kuongezwa kwa damu ya O Rh D hasi(damu ya mtoaji damu kwa watu wote) kwa mpokeaji wa aina ya damu ya A Rh D chanya, athari za kinga kati ya kingamwili za anti-B za mpokeaji na chembechembe nyekundu za damu zilizoongezwa hazitarajiwi. Hata hivyo, kiasi kidogo cha plazma katika damu iliyoongezwa ina kingamwili za kinza-A, ambazo zinaweza kuathiriana na antijeni A kwenye uso wa chembechembe nyekundu za damu ya mpokeaji, lakini mmenyuko mkubwa hauna uwezekano wa kuwepo kwa sababu ya sababu za mzimuo. Wepesi wa kuhisi Rh D hautarajiwi.

Zaidi ya hayo, antijeni za uso wa chembechembe nyekundu za damu isipokuwa A, B na Rh D, zinaweza kusababisha athari mbaya na wepesi wa kuhisi, ikiwa zinaweza kufunga kingamwili zinazolingana kusababisha mwitikio wa kinga. Kuongezewa damu kuna changamano kwa sababu chembe za kugandisha damu na chembechembe nyeupe za damu (WBCs) zina mifumo yao ya antijeni za uso, na wepesi wa kuhisi wa antijeni za chembe za kugandisha damu au WBC unaweza kutokea kutokana na kuongezewa damu.

Kuhusu kuongezewa plazma, kinyume cha hali hii hutokea. Plazma ya aina ya O, iliyo na kingamwili zote za kinza-A ns kinza-B, inaweza kutolewa kwa wapokeaji wa O pekee yao. Kingamwili zitashambulia antijeni za aina nyingine yoyote ya damu. Kinyume chake, plazma ya AB inaweza kutolewa kwa wagonjwa wenye aina yoyote ya damu ya ABO kwa sababu haina kingamwili zozote za kinza-A au kinza-B.

Kuainisha jeni za vikundi damu[hariri | hariri chanzo]

Mbali na desturi ya sasa ya majaribio ya serolojia ya aina za damu, maendeleo katika kutambua ugonjwa kwa molekiuli yanaruhusu uongezeko wa matumizi ya kuainisha jeni za vikundi damu. Tofauti na majaribio ya serolijia yanayoripoti fenotaipu ya moja kwa moja ya aina ya damu, kutambua aina-jeni kunaruhusu utabiri wa fenotaipu kutokana na maarifa ya msingi wa molekiuli ya antijeni zinazojulikana kwa sasa. Hii inaruhusu uamuzi wa kina wa aina ya damu na kwa hivyo ulinganisho bora wa kuongezewa damu, jambo ambalo linaweza kuwa muhimu hasa kwa wagonjwa wenye mahitaji ya kuongezewa damu mara nyingi kuzuia kingamaradhi ya allo. [60] [61]

Ugeuzaji[hariri | hariri chanzo]

Mwezi Aprili 2007 uligunduliwa utaratibu wa kugeuza aina za damu A, B, na AB kuwa O kwa kutumia kimeng'enya. Utaratibu huu bado ni wa majaribio na damu inayopatikana bado haijafanyiwa majaribio kwa binadamu. [62] [63] Utaratibu huu hasa huondoa au kubadilisha antijeni kwenye chembechembe nyekundu za damu, ili antijeni na kingamwili zingine zisalie. Hii haisaidii upatanifu wa plazma, lakini hili ni jambo dogo kwa sababu plazma ina manufaa finyu zaidi katika kuongezewa damu na ni rahisi zaidi kuihifadhi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mifumo miwili ya aina za damu iliyo muhimu zaidi iligunduliwa na Karl Landsteiner wakati wa majaribio ya kwanza ya kuongezea damu: aina ya ABO mwaka wa 1901 [64] na kwa ushirikiano na Alexander S. Wiener aina ya Rhesus mwaka wa 1937. [65] Uvumbuzi wa jaribio la Coombs mwaka wa 1945, [66] majilio ya udaktari wa kuongezewa damu, na ufahamu wa ugonjwa wa hemolitiki ya mtoto mchanga kuliongoza kwa ugunduzi wa aina zaidi za damu, na sasa mifumo 30 ya vikundi vya damu ya binadamu vinatambuliwa na Shirika la Kimataifa la Utoaji damu (ISBT), [2] na ndani vikundi 30 vya damu, zaidi ya antijeni 600 tofauti za vikundi vya damu zimepatikana, [4] nyingi kati ya hizi ni za nadra sana au zinapatikana katika makabila mengine. Aina za damu zimetumika katika sayansi ya kuchunguza na katika kupima ubaba, lakini nafasi ya matumizi haya mawili inachukuliwa na uchukuaji kijeni wa alama za vidole ambao hutoa uhakika zaidi. [67]

Imani za kitamaduni na madai mengine[hariri | hariri chanzo]

Imani maarufu nchini Japani ni kwamba aina ya damu ya ABO ya mtu inaweza kutabiri tabia yao, nafsi yao, na upatanifu wao na wengine. Imani hiyo imeenea Korea Kusini. [68]

Kutokana na mawazo ya kisayansi ya ubaguzi wa rangi wa kihistoria, nadharia hii ilifika Japani mwaka wa 1927 katika ripoti ya mwanasaikolojia, na serikali ya kijeshi ya wakati huo ikaagiza utafiti kwa lengo la kuadilisha askari bora. [68]

Imani hiyo ilififia katika miaka ya 1930 kutokana na msingi wake ambao haukuwa wa kisayansi. Nadharia hii ilikataliwa na wanasayansi muda mrefu uliopita, lakini ilifufuliwa katika miaka ya 1970 na Masahiko Nomi, mtangazaji ambaye hakuwa na ujuzi wowote wa uuguzi. [68]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Maton, Anthea (1993). Human Biology and Health. Englewood Cliffs, New Jersey, USA: Prentice Hall. ISBN 0-13-981176-1. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
 2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Table of blood group systems". International Society of Blood Transfusion. 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-16. Iliwekwa mnamo 2008-09-12. {{cite web}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
 3. 3.0 3.1 E.A. Letsky (2000). "Chapter 12: Rhesus and other haemolytic diseases". Antenatal & neonatal screening (toleo la Second). Oxford University Press. ISBN 0-19-262827-7. {{cite book}}: Check |isbn= value: checksum (help); Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
 4. 4.0 4.1 "American Red Cross Blood Services, New England Region, Maine, Massachusetts, New Hampshire, Vermont". American Red Cross Blood Services - New England Region. 2001. Iliwekwa mnamo 2008-07-15. there are more than 600 known antigens besides A and B that characterize the proteins found on a person's red cells
 5. Dean, Laura. "The ABO blood group". Blood Groups and Red Cell Antigens. online: NCBI. A number of illnesses may alter a person's ABO phenotype {{cite book}}: Cite has empty unknown parameters: |origdate= na |origmonth= (help); External link in |chapterurl= (help); Unknown parameter |chapterurl= ignored (|chapter-url= suggested) (help)
 6. Stayboldt C, Rearden A, Lane TA (1987). "B antigen acquired by normal A1 red cells exposed to a patient's serum". Transfusion. 27 (1): 41–4. doi:10.1046/j.1537-2995.1987.27187121471.x. PMID 3810822.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 7. Matsushita S, Imamura T, Mizuta T, Hanada M (1983). "Acquired B antigen and polyagglutination in a patient with gastric cancer". The Japanese Journal of Surgery. 13 (6): 540–2. doi:10.1007/BF02469500. PMID 6672386. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 8. Kremer Hovinga I, Koopmans M, de Heer E, Bruijn J, Bajema I (2007). "Change in blood group in systemic lupus erythematosus". Lancet. 369 (9557): 186–7, author reply 187. doi:10.1016/S0140-6736(07)60099-3. PMID 17240276.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 9. [17] ^ Demi-Lee Brennan amebadilisha aina za damu na mfumo wa kinga Kate Sikora, The Daily Telegraph, 25 Januari 2008
 10. Madaktari wa Australia wanasifia 'muujiza' wa kupandikiza wa chipukizi Sean Rubinsztein-Dunlop, ABC News (Australia), 24 Januari 2008
 11. Chown B., Lewis M., Kaita K. (1957). "A new Kell blood-group phenotype". Nature. 180 (4588): 711. doi:10.1038/180711a0. PMID 13477267. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 12. Miller LH, Mason SJ, Clyde DF, McGinniss MH (1976). "The resistance factor to Plasmodium vivax in blacks. The Duffy-blood-group genotype, FyFy". The New England Journal of Medicine. 295 (6): 302–4. doi:10.1056/NEJM197608052950602. PMID 778616. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 13. Kwiatkowski DP (2005). "How malaria has affected the human genome and what human genetics can teach us about malaria". American Journal of Human Genetics. 77 (2): 171–92. doi:10.1086/432519. PMC 1224522. PMID 16001361. The different geographic distributions of α thalassemia, G6PD deficiency, ovalocytosis, and the Duffy-negative blood group are further examples of the general principle that different populations have evolved different genetic variants to protect against malaria {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
 14. "Your blood – a textbook about blood and blood donation" (PDF). uk. 63. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2006-08-27. Iliwekwa mnamo 2008-07-15.
 15. Talaro, Kathleen P. (2005). Foundations in microbiology (toleo la 5th). New York: McGraw-Hill. ku. 510–1. ISBN 0-07-111203-0.
 16. Moise KJ (2008). "Management of rhesus alloimmunization in pregnancy". Obstetrics and Gynecology. 112 (1): 164–76. doi:10.1097/AOG.0b013e31817d453c. PMID 18591322. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
 17. "Rh血型的由來". Hospital.kingnet.com.tw. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-11. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 18. [https: / / www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/fields/2119.html CIA World Factbook]
 19. "Blood Types - What Are They?, Australian Red Cross". Giveblood.redcross.org.au. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 20. "Austrian Red Cross - Blood Donor Information". Old.roteskreuz.at. 2006-03-21. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-09. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 21. "Rode Kruis Wielsbeke - Blood Donor information material". Rodekruiswielsbeke.be. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-11-26. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 22. "Tipos Sanguíneos". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-03-09. Iliwekwa mnamo 2010-12-16.
 23. Canadian Blood Services - Société canadienne du sang. "Types & Rh System, Canadian Blood Services". Bloodservices.ca. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-04. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 24. "Veregruppide esinemissagedus Eestis". Kliinikum.ee. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-05-27. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 25. "Suomalaisten veriryhmäjakauma". Veripalvelu.fi. 2009-08-21. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-05-30. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 26. "Les groupes sanguins (système ABO)". Centre Hospitalier Princesse Grace - Monaco (kwa French). C.H.P.G. MONACO. 2005. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-25. Iliwekwa mnamo 2008-07-15.{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
 27. Häufigkeit der Blutgruppen (Kijerumani)
 28. "Blóðflokkar". Landspitali.is. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-19. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 29. "Indian Journal for the Practising Doctor". Indmedica.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-16. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 30. "Irish Blood Transfusion Service - Irish Blood Group Type Frequency Distribution". Irish Blood Transfusion Service. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-28. Iliwekwa mnamo 2009-11-07.
 31. "The national rescue service in Israel". Mdais.org. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 32. "Voorraad Erytrocytenconcentraten Bij Sanquin" (kwa Dutch). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-26. Iliwekwa mnamo 2009-03-27.{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
 33. "What are Blood Groups?". NZ Blood. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 34. [69] ^ [https: / / www.giblod.no/Modules/Page/viewPage.asp?modid=7324&level=7324 Shirika la Kinorwe la Watoaji Damu]
 35. "Regionalne Centrum Krwiodawstwa i Krwiolecznictwa we Wroclawiu". Rckik.wroclaw.pl. 2010-07-20. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 36. [72] ^ Taasisi ya Kireno ya damu (tukiamini kuwa antijeni za Rh na AB zinajitegemea)
 37. "Fequency of ABO blood groups in the eastern region of Saudi Arabia". Cat.inist.fr. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-25. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 38. "South African National Blood Service - What's Your Type?". Sanbs.org.za. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-06. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 39. "Federación Nacional de Donantes de Sangre/La sangre/Grupos". Donantesdesangre.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-01-10. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 40. "Frequency of major blood groups in the Swedish population". Geblod.nu. 2007-10-02. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-11-24. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 41. "Rh血型的由來". Hospital.kingnet.com.tw. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-12-11. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 42. "Turkey Blood Group Site". Kangrubu.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-05-29. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 43. "Frequency of major blood groups in the UK". Blood.co.uk. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-11. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 44. "Blood Types in the U.S". Bloodcenter.stanford.edu. 2008-06-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-12. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 45. ((wanaelezea web | url = http://www.bloodbook.com/world-abo.html | title = Usambazaji wa kirangi na kikabila wa damu ya aina ya ABO | mchapishaji = Bloodbook.com | tarehe = | accessdate = 2010/08/01))
 46. Blood Transfusion Division, United States Army Medical Research Laboratory (1971). Selected contributions to the literature of blood groups and immunology. 1971 v. 4. United States Army Medical Research Laboratory, Fort Knox, Kentucky. ... In northern India, in Southern and Central China and in the neighboring Central Asiatic areas, we find the highest known frequencies of B. If we leave this center, the frequency of the B gene decreases almost everywhere ...
 47. 47.0 47.1 Encyclopaedia Britannica (2002). The New Encyclopaedia Britannica. Encyclopaedia Britannica, Inc. ISBN 0852297874. ... The maximum frequency of the B gene occurs in Central Asia and northern India. The B gene was probably absent from American Indians and Australian Aborigines before racial admixture occurred with the coming of the white man ...
 48. Carol R. Ember, Melvin Ember (1973). Anthropology. Appleton-Century-Crofts. ... Blood type B is completely absent in most North and South American Indians ...
 49. Laura Dean, MD (2005). Blood Groups an Red Cell Antigens. National Center for Biotechnology Information, United States Government. ISBN 1932811052. ... Type A is common in Central and Eastern Europe. In countries such as Austria, Denmark, Norway, and Switzerland, about 45-50% of the population have this blood type, whereas about 40% of Poles and Ukrainians do so. The highest frequencies are found in small, unrelated populations. For example, about 80% of the Blackfoot Indians of Montana have blood type A ...
 50. Technical Monograph No. 2: The ABO Blood Group System and ABO Subgroups (PDF). Biotec. 2005. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2007-02-06. Iliwekwa mnamo 2010-12-16. ... The frequency of blood group A is quite high (25-55%) in Europe, especially in Scandinavia and parts of central Europe. High group A frequency is also found in the Aborigines of South Australia (up to 45%) and in certain American Indian tribes where the frequency reaches 35% ... {{cite book}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
 51. Nickel RG, Willadsen SA, Freidhoff LR; na wenz. (1999). "Determination of Duffy genotypes in three populations of African descent using PCR and sequence-specific oligonucleotides". Human Immunology. 60 (8): 738–42. doi:10.1016/S0198-8859(99)00039-7. PMID 10439320. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help); Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 52. Bruce, MG (2002). "BCF - Members - Chairman's Annual Report". The Blood Care Foundation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-04-10. Iliwekwa mnamo 2008-07-15. As Rhesus Negative blood is rare amongst local nationals, this Agreement will be of particular value to Rhesus Negative expatriates and travellers {{cite web}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
 53. Daniels G, Finning K, Martin P, Summers J (2006). "Fetal blood group genotyping: present and future". Annals of the New York Academy of Sciences. 1075: 88–95. doi:10.1196/annals.1368.011. PMID 17108196. {{cite journal}}: Unknown parameter |month= ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 54. "Use of Anti-D Immunoglobulin for Rh Prophylaxis". Royal College of Obstetricians and Gynaecologists. 2002. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-30. Iliwekwa mnamo 2010-12-16. {{cite web}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
 55. "Pregnancy - routine anti-D prophylaxis for D-negative women". NICE. 2002. {{cite web}}: Unknown parameter |month= ignored (help)
 56. "RBC compatibility table". American National Red Cross. 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-08-04. Iliwekwa mnamo 2008-07-15. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |month= ignored (help)
 57. 57.0 57.1 [117] ^ Aina za damu na upatanifu bloodbook.com
 58. Fauci, Anthony S. (1998). Harrison's Principals of Internal Medicine. New York: McGraw-Hill. uk. 719. ISBN 0-07-020291-5. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help) )
 59. "Universal acceptor and donor groups". Webmd.com. 2008-06-12. Iliwekwa mnamo 2010-08-01.
 60. Anstee DJ (2009). "Red cell genotyping and the future of pretransfusion testing". Blood. 114 (2): 248–56. doi:10.1182/blood-2008-11-146860. PMID 19411635.
 61. Avent ND (2009). "Large-scale blood group genotyping: clinical implications". Br J Haematol. 144 (1): 3–13. doi:10.1111/j.1365-2141.2008.07285.x. PMID 19016734.
 62. "Blood groups 'can be converted'", BBC News, 2007-04-02. Retrieved on 2008-07-15. 
 63. Liu Q, Sulzenbacher G, Yuan H, Bennett E, Pietz G, Saunders K, Spence J, Nudelman E, Levery S, White T, Neveu J, Lane W, Bourne Y, Olsson M, Henrissat B, Clausen H (2007). "Bacterial glycosidases for the production of universal red blood cells". Nat Biotechnol. 25 (4): 454. doi:10.1038/nbt1298. PMID 17401360.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 64. Landsteiner K. Suri Kenntnis der antifermentativen, lytischen und des agglutinierenden Wirkungen Blutserums und der Lymphe. Zentralblatt Bakteriologie 1900, 27:357-62.
 65. Landsteiner K, Wiener AS An agglutinable factor in human blood recognized by immune sera for rhesus blood. Proc Soc Exp Biol Med 1940; 43:223-224.
 66. Coombs RRA, Mourant AE, Race RR. A new test for the detection of weak and "incomplete" Rh agglutinins. Brit J Exp Path 1945; 26:255-66.
 67. Johnson P, Williams R, Martin P (2003). "Genetics and Forensics: Making the National DNA Database". Science Studies. 16 (2): 22–37. PMC 1351151. PMID 16467921.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
 68. 68.0 68.1 68.2 "Myth about Japan blood types under attack", AOL Health, 2005-05-06. Retrieved on 2007-12-29. Archived from the original on 2009-12-28. 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aina ya damu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.