Nenda kwa yaliyomo

Lukemia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Seli za mtu mwenye lukemia
Seli za mtu mwenye lukemia

Lukemia ni kansa ya seli nyeupe za damu na uboho wa mfupa. Kama mtu akiwa na lukemia, mwili huunda seli nyingi nyeupe za damu (kwa Kiingereza leukocytes) .

Kuna aina nyingi za lukemia. Lukemia ni mojawapo ya magonjwa makubwa ya damu (kwa Kiingereza hematological neoplasms). Lukemia inaweza kusababisha kifo ndani ya wiki, miezi, au miaka kama isipotibiwa. Maisha ya mtu hutegemeana na aina ya lukemia.

Mwaka wa 2000, watoto na watu wazima 256,000 duniani kote walipata aina fulani ya lukemia, na 209,000 walikufa kutokana na hiyo aina, wengine waliendelea kuishi. Takribani asilimia 90 ya lukemia zote huonekana kwa watu wazima.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lukemia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.