Euro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka )
Jump to navigation Jump to search
Ishara ya Euro
Euro sign.svg

Euro ni sarafu ya pamoja katika baadhi ya nchi za Ulaya. Wakazi wake 343,000,000 wanatumia kwa kawaida pesa hiyo. Watu wengine 240,000,000 wanatumia pesa zilizoungwa na euro, hasa barani Afrika.

Tangu mwaka 2002 nchi 13 za EU zilifuta sarafu ya kitaifa ili kutumia Euro tu. Siku hizi ni 19.

Euro moja imegawanyika katika senti 100.

Kuna benknoti za € 5 (kijivu), € 10 (nyekundu), € 20 (buluu], € 50 (machungwa), € 100 (kijani), € 200 (njano), € 500 (nyekundu).

Kuna sarafu za metali 8 za € 0,01, € 0,02, € 0,05, € 0,10, € 0,20, € 0,50, € 1, € 2.

Pesa ya karatasi inatolewa na benki kuu ya Ulaya na ni sawa kote.

Sarafu zinatolewa na nchi wanachama na zinatofautiana upande mmoja, lakini sarafu zote hutumika kote.

Ishara ya Euro[hariri | hariri chanzo]

Ishara ya Euro ni herufi ya Kigiriki epsilon (E) yenye mistari miwili ya kulala: .

Nchi wanachama wa Euro[hariri | hariri chanzo]

Euro
Panotên Euro
Euro
Panotên Euro
 1. Austria
 2. Ubelgiji
 3. Ufini
 4. Ufaransa
 5. Ujerumani
 6. Ugiriki
 7. Ueire
 8. Italia
 9. Latvia
 10. Luxemburg
 11. Ureno
 12. Hispania
 13. Uholanzi
 14. Slovakia
 15. Slovenia
 16. Kupro
 17. Malta
 18. Estonia
 19. Lithuania


Nchi zifuatazo hutumia pia Euro kama pesa pekee bila kuwa sehemu za mapatano:

Pesa za nchi zifuatazo zimeungwa na Euro:

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Euro kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.