Benknoti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Benknoti za kwanza kutoka China

Benknoti (kutoka Kiitalia banca + nota kupitia Kiingereza "banknote") kwa kawaida ni kipande cha karatasi (pia: plastiki) kinachochapishwa na kuonyesha namba fulani na jina la pesa ya nchi fulani. Inakubaliwa kama njia ya malipo kabisa pamoja na pamoja na sarafu ni pesa taslim ya nchi fulani.

Kwa kawaida vipande vya sarafu au pesa taslim metalia huwa na viwango vidogo zaidi na benknoti huwa na viwango vikubwa zaidi.

Usalama wa benknoti[hariri | hariri chanzo]

Tangu kutolewa kwa benknoti wahalifu walijaribu kutengeneza benknoti bandia wakiiga zile zinazotolewa na benki rasmi. Kwa sababu hiyo benki kuu na serikali zinajitahidi kutoa benknoti ambazo ni vigumu kuiga. Hapa wanatumia karatasi za pekee zisizopatikana madukani, wanachapisha kwa rangi zisizosomeka na mashine ya fotokopi, wanaingiza nyuzi za metali ndani ya karatasi na kadhalika.

Tangu mwisho wa karne ya 20 nchi kadhaa zimeanza kutoa benknoti za plastiki badala ya karatasi. Hizi zina gharama kubwa zaidi ya kuzitengeneza lakini hadi sasa usalama ni kubwa zaidi ni vigumu sana za kuiga pia hazichakai haraka kama vile noti za karatasi.

Historia ya benknoti[hariri | hariri chanzo]

Chanzo cha historia ya benknoti ni barua zinazoahidi kulipa kiasi fulani cha pesa kwa mtu yeyote anayeshika barua ile. Kwa hiyo benknoti zilikuwa sawa na hundi za leo.

Barua badala ya sarafu nzito[hariri | hariri chanzo]

Kiasili vipande vya metali adili kama dhahabu au fedha vilitumiwa kama pesa vikipimwa kuwa na uzito fulani kwa mfano "pound" ya Uingereza ilikuwa sawa na uzito wa "pauni" au ratili moja ya fedha.

Wakati uchumi uliongezeka watu walianza kutumia viasi vikubwa vya pesa na hii ilikuwa kazi ngumu kutokana na uzito wa sarafu nyingi. Hapo wafanyabiashara waliacha sarafu zao kwa mtu aliyeaminiwa na kushika barua kutoka kwake iliyothebitisha ya kwamba alishika kiasi fulani kwa niaba ya mwingine. Pale ambako watu waliaminiana waliweza kutumia barua hizi kama malipo badala ya sarafu yenyewe.

China[hariri | hariri chanzo]

Serikali ya kwanza ya kutoa benknoti ilikuwa nasaba ya Song nchini China mnamo mwaka 960. Benknoti hizi zilikuwa na maandishi zilizomwahidi mwenye kuishika ya kwamba atapewa kiasi fulani cha fedha akiipeleka benknoti kwa idara ya fedha ya serikali. Kimsingi hii ilibaki muundo wa benknoti hadi karne ya 20 yaani zilikuwa ahadi za serikali au za benki kubwa kumpatia mwenye noti kiasi fulani cha dhahabu au fedha.

Tatizo la benknoti tangu mwanzo ilikuwa ya kwamba serikali yenye matatizo iliweza kuendelea kuchapisha benknoti mpya kata kama haikuwa na dhahabu au fedha ya kutosha. Hii haikuwa tatizo mara moja kwa sababu hali halisi benknoti zilifanya kazi zao kama thamani ya benknoti zote ililingana na thamani ya bidhaa zilizopatikana katika nchi fulani. Lakini kama serikali iliendelea kuchapisha pesa hovyo watu walianza kuona ya kwamba pesa haina thamani tena na bei zilianza kupanda haraka sana.

Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Katika Ulaya benknoti za kwanza zilizotolewa na serikali au kwa niaba ya serikali zilianza kupatikana tangu karne 16 katika Uholanzi na Ufaransa. Mara kwa mara majaribio haya ya kwanza yalivurugika kutokana na kuchapisha benknoti nyingi mno na kushuka kwa thamani ya pesa hii.

Benknoti zilianza kuwa kawaida hata kwa watu wa kawaida wakati wa karne ya 19. Mwnazoni benki kuu ya kila nchi kisheria ilipaswa kuwa na akiba ya dhahabu au fedha iliyolingana ama na benknoti zote au angalau na sehemu kubwa zao. Masharti haya yalifutwa polepole kwa sababu ilionekana ya kwamba kama kiasi cha benknoti haizidi thamani ya bidhaa nchini uchumi unaendelea bila mvurugo. Tena baada ya kupatikana kwa mawasiliano ya kisasa kama simu na intaneti kiasi kikubwa cha ahadi za kulipana inazunguka katika uchumi na hizi ahadi zinafanya kazi kama pesa hata kama si pesa taslim.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Picha z benknoti za dunia
Benknoti za plastiki
Vyama vya watu wanaokusanya aina nyingi a benknoti
Wachapishaji
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: