Sarafu (mfumo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bao la ofisi ya kubadilisha sarafu

Sarafu (ing.: currency) kwa maana ya kisasa ni utaratibu uliopo katika nchi fulani au jumuiya ya nchi zenye pesa ya pamoja unaotawala utoaji na matumizi ya sarafu na benknoti katika eneo hili.

Sarafu na pesa[hariri | hariri chanzo]

Kiasili neno sarafu lamaanisha vipande vya metali vinavyokubaliwa kama pesa kwa matumizi ya malipo ya bidhaa na huduma.

Zamani sarafu mbalimbali zilitumiwa pamoja kwa mfano katika Afrika ya Mashariki kabla ya ukoloni au katika miaka ya kwanza ya ukoloni kulikuwa na Riali ya Zanzibar, Rupia, Dolar ya Maria Theresia na pesa za Kiarabu kandokando. Thamani yao ililinganishwa kutokana na kiasi cha fedha halisi ndani ya kila sarafu.

Katika dunia ya kisasa kulingana na maendeleo ya uchumi kila nchi imeweka utaratibu rasmi wa kukubali aina moja ya pesa katika eneo lake. Kama pesa ya nchi au sarafu kwa maana hiyo ni dhaifu sana kuna pia matumizi ya sarafu mbalimbali kandokando hadi leo.

Nchi kadhaa zimeendelea kuunda sarafu ya pamoja na mfano bora ni Euro kwa ajili ya nchi nyingi za Ulaya iliyochukua nafasi ya sarafu za kitaifa tangu mwaka .

Soko la sarafu[hariri | hariri chanzo]

Sarafu nyingi za dunia zafanyiwa biashara kwenye masoko ya sarafu ambako fedha za kigeni zanunuliwa na kuuzwa. Hapa kunatokea kima cha mabadilishano ya fedha. Sarafu inayotumiwa zaidi kimataifa kwa ajili ya biashara kati ya nchi mbalimbali ni Dolar ya Marekani (US-Dollar) na mengine ni hasa Euro ya Ulaya na Pauni ya Uingereza. Kwa jumla kuna takriban sarafu rasmi 160 duniani.

Kama sarafu inakubalika kwenye masoko ya sarafu huitwa fedha (au sarafu) ya kusafifika (ing. convertible currency). Nchi kadhaa zina sheria zinazolenga kuzuia kusafifika kwa pesa yao. Kwa mfano Won wa Korea Kaskazini, Peso ya Kuba au Rubel ya Transnistria haibadilishwa kwa fedha ya kigeni isipokuwa kwa watu na makampuni chache ndani ya nchi na kutopokelewa nje ya nchi hizi. Lakini kwa kawaida kuna soko la siri kwa ajili sarafu hizi hata kama ni marufuku ndani ya nchi na hapo thamani ni chini sana na kiwango rasmi inayotangaziwa rasmi.

Utawala wa sarafu[hariri | hariri chanzo]

Usimamizi wa sarafu uko mkononi mwa waziri wa fedha au benki kuu ya nchi mbalimbali. Katika nchi zinazofuata mfumo wa soko huria mara nyingi benki kuu ina kiwango kikubwa cha uhuru mbele ya serikali. Zamani za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ya kwanza sarafu ya shilingi ya Afrika ya Mashariki ilisimamiwa na Bodi ya Sarafu ya Afrika ya Mashariki iliyovunjika mwaka 1966.

Zamani yaani hadi mwanzo au katikati ya karne ya 20 sarafu nyingi ziliunganishwa na dhahabu. Maana yake kila dolar, pauni, mark, rupia au shilingi iliwakilisha kiasi fulani cha dhahabu au pia fedha halisi. Benki kuu zilikuwa na akiba kubwa ya metali hizi zilizotakiwa kuwa sawa na jumla ya benknoti zilizotolewa na benki kuu.

Lakini mfumo huu uliachwa. Siku hizi jumla ya pesa iliyotolewa inatakiwa kiulingana na nguvu ya uchumi wa nchi au eneo. Kama benki kuu inaendelea kuchapisha benknoti zaidi kunatokea mfumko wa bei yaani thamani ya pesa inashuka.

Matumizi ya Dolar na Eruo duniani:      Marekani      Nchi za nje zinazotumia Dolar ya Marekani      Nchi zinazofunga pesa yao kwa Dolar moja kwa moja      Nchi zinazofunga pesa yao kwa Dolar kwa kuacha nafasi kidogo      Nchi za Euro      Nchi za nje zinazotumia Euro      Nchi zinazofunga pesa yao kwa Euro moja kwa moja      Nchi zinazofunga pesa yao kwa Euro kwa kuacha nafasi kidogo

Nchi kadhaa zimefunga kima cha mabadilishano ya pesa yao kwa sarafu muhimu kama dolar au Euro. Faida yake ni ya kwamba shirika na watu katika nchi hizi -ambazo mara nyingi ni ndogo- zina uhakika kuhusu thamani ya pesa yao. Kwa mafanyikio wa mfumo huu ni lazima ya kwamba benki kuu ina pesa ya kigeni ya kutosha ili iweze ila wakati kubadilisha pesa ya nchi kwa kima cha soko huru na kwa kima rasmi kwa sarafu inakofungwa. Mfano ni nchi nyingi za Afrika ya Magharibi zilizotumia zamani pesa ya Ufaransa kama sarafu yao na sasa zimefunga pesa ya kitaifa kwa Euro.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]