Riali ya Zanzibar
Riali ya Zanzibar ilikuwa fedha halali iliyotolewa na Usultani wa Zanzibar kuanzia mwaka 1882 (1299 AH). Amri ya kuanzisha pesa hii ilitolewa na Sultani Barghash ibn Said ibn Sultan.
Ilipatikana kwa sarafu za riali 5, 2 1/2, 1, nusu na robo riali. Iligawiwa katika paisa 136.
Pamoja na riali, matumizi ya rupia ya Uhindi na Dolar ya Maria Theresia yalikuwa kawaida.
Mwaka 1908 Usultani (wakati ule ulikuwa tayari nchi lindwa chini ya Uingereza) uliacha riali na kutumia fedha ya rupia sawa na majirani kwenye bara yaani Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na Afrika ya Mashariki ya Kiingereza.
Sarafu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1882 (AH 1299) sarafu za paisa 1 na riali ¼, ½, 1, 2½ na 5 zilipelekwa nchini. Paisa ilikuwa sarafu ya shaba. Riali ndogo zilikuwa za fedha na sarafu za riali 2½ na 5 za dhahabu.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Coin Catalogue - picha
- Uchumi wa zanzibar - maelezo
- History of Zanzibar Archived 23 Oktoba 2004 at the Wayback Machine.