Mkoa wa Manyara
Mkoa wa Manyara ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 27000. Umepakana na mikoa ya Arusha na Kilimanjaro upande wa kaskazini, Mkoa wa Tanga upande wa mashariki, Mkoa wa Dodoma upande wa kusini na mikoa ya Singida na Shinyanga upande wa magharibi.
Mkoa wa Manyara umetengwa na Mkoa wa Arusha mwaka 2002 kwa azimio la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukiwa na eneo la km² 46,359.
Babati ndiyo makao makuu ya mkoa.
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Jumla ya wakazi mkoani ilikuwa 1,892,502 katika sensa ya mwaka 2022 [1].
Idadi hiyo imepatikana katika wilaya 7 zifuatazo (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022): Babati Vijijini (375,200), Babati Mjini (129,572), Hanang (367,391), Mbulu Vijijini (238,272), Mbulu Mjini (138.593), Simanjiro (291,169) na Kiteto (352,305).
Sensa zinaonyesha kwamba ni kati ya mikoa ya Tanzania yenye ongezeko kubwa la wakazi. Pia ni kati ya mikoa yenye maambukizi machache zaidi ya Ukimwi.
Wenyeji wa mkoa huu ni pamoja na Wairaqw, Wamasai, Wambugwe, Wagorowa na Wabarbaig wakijihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji kama njia ya kuingiza kipato chao cha kila siku.
Majimbo ya bunge
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi 7 yafuatayo:
- Babati Mjini : mbunge ni Pauline Gekuli (CCM)
- Babati Vijijini : mbunge ni Jitu Vrajilal Soni (CCM)
- Hanang’ : mbunge ni Samwel Hhayuma (CCM)
- Kiteto : mbunge ni Emmanuel Papiani (CCM)
- Mbulu Mjini : mbunge ni Zacharia Paulo Issaay (CCM)
- Mbulu Vijijini : mbunge ni Flatei Massay (CCM)
- Simanjiro : mbunge ni James Kinyasi Ole Millya (CCM)
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- (Kiswahili) Tovuti ya Mkoa wa Manyara
- Manyara Matokeo ya sensa ya 2002* Serikali ya TanzaniaIlihifadhiwa 15 Desemba 2003 kwenye Wayback Machine.
- Ijue mikoa ya Tanzania Ilihifadhiwa 21 Februari 2006 kwenye Wayback Machine.
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Manyara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
|