Babati
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Babati | |
| Mahali pa mji wa Babati katika Tanzania | |
| Anwani ya kijiografia: 4°13′12″S 35°45′0″E / 4.22°S 35.75°E | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Mkoa | Manyara |
| Wilaya | Babati |
Babati ni wilaya na mji mdogo wa Mkoa wa Manyara huko nchini Tanzania. Mji mkuu wake wa wilaya unaitwa 'Babati Mjini' upo na pia ni kitovu cha Mkoa wa Manyara, takriban kilomita za mraba 172 kusini mwa Arusha. Wilaya hii ndiyo wilaya kuu katika Mkoa wa Manyara. Wilaya imepakana na Mkoa wa Arusha, kwa upande wa kusini-mashariki imepakana na Wilaya ya Simanjiro, kwa upande wa kusini imepakana na Mkoa wa Dodoma, kwa upande kusini-magharibi imepakana na Wilaya ya Hanang, na kwa upande wa kaskazini-magharibi Wilaya ya Mbulu.
Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2002, idadi ya wakazi ya Wilayani Babati ilikuwa 303,013. [1]
Vyanzo [hariri]
- Babati District Homepage for the 2002 Tanzania National Census
- Tanzanian Government Directory Database
Tazama pia [hariri]
- Wilaya za Tanzania
- Mkoa wa Manyara
- Wilaya ya Kiteto
- Wilaya ya Hanang
- Wilaya ya Simanjiro
- Wilaya ya Mbulu