Mji mdogo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mji mdogo ni hadhi ambayo baadhi ya vijiji vinapewa na serikali ya nchi kisha kutimiza vigezo vya sheria husika.

Nchini Tanzania Mamlaka ya Mji Mdogo (Township Authority) ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyopo kwenye Mamlaka za Wilaya. Mamlaka hizo zinaanzishwa pale ambapo palikuwa na Kijiji ambacho kimeanza kuendelezwa na kuwa na mazingira ya kimji.

Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa amepewa madaraka ya kutangaza Kijiji au Vijiji vilivyofikia sifa zilizowekwa kuwa Mamlaka za Miji Midogo, ambazo ni:

  1. Kuwe idadi ya watu wasiopungua elfu kumi (10,000);
  2. Kuwe na huduma za jamii zifuatazo: Shule ya Sekondari, Kituo cha Afya na Mahakama ya Mwanzo;
  3. Kuwe na Soko pamoja na Maduka ya rejareja yasiyopungua matano (5);
  4. Eneo liwe ni Makao Makuu ya Kata au Tarafa.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mji mdogo kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.