Wilaya ya Mbulu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Mbulu (kijani) katika mkoa wa Manyara.
Wilaya ya Mbulu ni wilaya moja ya Mkoa wa Manyara. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Mbulu ilihesabiwa kuwa 237,882 [1].
Mbulu imepakana na Mkoa wa Arusha pamoja na ziwa Eyasi upande wa kaskazini, wilaya ya Babati upande wa mashariki, wilaya ya Hanang upande wa kusini na mkoa wa Singida kwa magharibi.
Wenyeji asilia ni hasa Wairaqw (Wambulu).
Makao makuu yapo Mbulu mjini na mji huu ulianzishwa wakati wa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa jina la Neu-Trier.
| Kata za Wilaya ya Mbulu - Mkoa wa Manyara - Tanzania | ||
|---|---|---|
|
Bargish (Mbulu) | Bashay | Daudi (Mbulu) | Dongobesh | Gehandu | Haidom | Kainam | Maghang | Maretadu | Masieda | Mbulu mjini | Murray (Mbulu) | Sanu | Tlawi | Tumati | Yaeda Chini |
||
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Manyara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Mbulu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |