Prospa wa Akwitania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Prospa wa Aquitania (kwa Kilatini Prosper Aquitanus; 390 hivi – Roma, Italia, 463 hivi), alikuwa mfuasi wa Augustino wa Hippo, mwandishi wa vitabu vya Kikristo, na mwendelezaji wa kwanza wa kitabu Chronicon cha Jeromu hadi mwaka 455.

Ingawa alikuwa mlei, alijitosa katika mabishano kuhusu imani sahihi ya Kanisa Katoliki na kumtetea Augustino dhidi ya wapinzani wake, hasa Wapelaji.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 25 Juni[1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Prospa alizaliwa mkoani Aquitaine (labda Limoges, leo nchini Ufaransa)[2] na inadhaniwa alipata malezi mjini Marseille.

Mwaka 429 aliandikiana barua na Augustino.

Mwaka 431 alifika Roma ili kumuuliza Papa Selestini I kuhusu mafundisho ya Augustino.

Mwaka 440, alipochaguliwa Papa Leo I, Prospa akawa karani katika ofisi zake. Inasemekana kwamba ndiye aliyeandika barua maarufu ya Papa huyo kwa Eutike.

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Prospa ni muhimu kwa maandishi yake kuliko kwa maisha yake[3]. Vitabu vyake ni kama ifuatavyo:

De vocatione omnium gentium (Calling of All Nations)
Epitoma Chronicon
Capitulla
Sententia and Epigrammata
Liber contra Collatorem
Carmen de Providentia Divina (Poem on Divine Providence)

Matoleo yaliyopo[hariri | hariri chanzo]

 • Yanapatikana yote katika Patrologia Latina ya Migne, gombo la 51.
 • Epitoma Chronicon ilitolewa na Theodor Mommsen katika Chronica minora ya Monumenta Germaniae Historica (1892). Tafsiri ya Kiingereza inapatikana katika From Roman to Merovingian Gaul: A Reader ed. & trans. A. C Murray (Ontario, 2003) kur. 62–76.
 • Tazama pia Saint Prosper of Aquitaine, the Call of All Nations, iliyotolewa na P. De Letter, S.J. (Series Ancient Christian writers 14) 1952.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

 1. Martyrologium Romanum
 2. He is called Prosper Tiro in several manuscripts of his Epitoma Chronicon. (Steven Muhlberger, "Prosper's Epitoma Chronicon: was there an edition of 443?" Classical Philology 81.3 (July 1986), pp. 240-244).
 3. Muhlberger, 48

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 • Arturo Elberti, Prospero d'Aquitania: Teologo e Discepolo (Rome, 1999).
 • Mark Humphries. "Chronicle and Chronology: Prosper of Aquitaine, his methods and the development of early medieval chronography." Early Medieval Europe 5 (1996) 155–175.
 • Steven Muhlberger, The Fifth Century Chroniclers (Great Britain: Redwood Press, 1990) pp. 48–60.
 • Alexander Hwang. Intrepid Lover of Perfect Grace: The Life and Thought of Prosper of Aquitaine. Washington: Catholic University of America Press, 2009.
 • Caroline White, Early Christian Latin Poets (New York, 2000) pp. 113–118.
 • The Fathers of the Church (New York: The Catholic University of America, 1949) pp. 335–343.
 • L. Valentin, St. Prosper d'Aquitaine: Étude sur la littérature écclésiastique au cinqième siècle en Gaule (Paris, 1900). This work offers a complete list of previous writings on Prosper and is still the main reference.
 • August Potthast, Bibliotheca historica (1896).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.