Wamuawiya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nasaba ya Wamuawiya)
Uenezi wa utawala wa Kiislamu chini ya makhalifa wa kwanza na Waumawiya:      Uenezaji wakati wa Mtume Muhamad 622-632      Uenezaji wakati wa makhalifa rashidun 632-661      Uenezaji wakati wa Wamuawiya, 661-750

Wamuawiya (Kar. ‏الأمويون‎ al-umawiyyūn) ni jina la nasaba ya makhalifa waliotawala milki kubwa ya Kiislamu kati ya 661 bis 750 BK. Mfululizo huo ulianzishwa na Muawiya ibn Abu Sufyan aliyekuwa gavana Mwislamu mjini Dameski alipoasi dhidi ya khalifa Ali ibn Abi Talib mnamo mwaka 660. Wamuawiya walikuwa nasaba ya kwanza ya Kiislamu ya kutawala. Waliwafuata makhalifa wanne wa kwanza wakafuatwa na nasaba ya Waabbasi. Mkono mmoja wa familia hii iliendelea kutawala huko Hispania hata baada ya mwaka 750.

Mji mkuu wa Wamuawiya ulikuwa Dameski katika Shamu.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Familia ya Wamuawiya walikuwa sehemu ya kabila ya Waquraishi wa Makka sawa na Mtume Muhamad aliyezaliwa katika familia ya Wahashemi lakini si ndugu wa karibu na mtume. Jina la Wamuawiya lilianzishwa na Muawiya babau yake Muawiya ibn Abu Sufyan.

Geti ya ukumbi wa sala za masjid ya Wamuawiya mjini Dameski iliyojengwa na khalifa Al-Walid I.

Wamuawiya na Wahashemi walishindana kati yao The Umayyads and the Hashimites were bitter rivals. Sababu yake ilikuwa upinzani wa Abu Sufyan (baba wa khalifa wa kwanza wa Wamuawiya) dhidi ya Uislamu na Mahamad. Baadaye Abu Sufyan na wanawe walijiunga na imani mpya na Muawiya alikuwa karani ya mtume.

Uthman na utawala wa Muawiya[hariri | hariri chanzo]

Khalifa wa kwanza kutoka familia ya Muawiya alikuwa Uthman ibn Affan aliyewchaguliwa kama khalifa wa tatu. Lakini huyu hakuanzisha nasaba maana hajuamteua mrithi wowote.

Chanzo cha nasaba kiko katika fitina kuhusu kifo cha Uthman mwaka 656. Aliuawa Makka na waasi Waislamu kutoka Misri. Baada ya kifo chake Ali ibn Abi Talib (aliyekuwa Mhashemi) aliteuliwa kuwa khalifa wa nne. Ukoo wa Uthman ulidai utafiti mkali kuhusu kuuawa kwake wakamshtaki Ali ya kwamba alikataa kuwaadhibu wauaji wengine walimshtaki kuwa alihusika katika uuaji.

Muawiya ibn Abu Sufyan alikuwa gavana Mwislamu wa Shamu huko Dameski. Alikuwa mkuu wa jeshi kubwa na baada ya kusikia habari kutoka Makka alikataa kumkubali Ali kama khalifa mpya akadai haki kwa kifo cha Uthman.

Mwaka 657 jeshi lake lilikutana na jeshi la Ali kwenye mapigano ya Siffin. Hapo Ali alisita kummaliza Muawiya akakubali kusimamisha mapigano na kuondoa fitina kwa njia ya majadiliano. Majadiliano hayakutekelezwa kwa hiyo Muawiya alibaki katika nafasi yake kama mkuu wa Shamu hadi kifo cha Ali mwaka 661.

Hapo alikuwa mwenye nguvu kati ya wote waliotafuta ukhalifa akajitangaza khalifa na wapinzani walimkubali. Hata Hasan ibn Ali mwana wa Ali alikubali mapatano naye.

Utawala wa Muawiya[hariri | hariri chanzo]

Muawiya aliendelea kukaa Dameski iliyokuwa sasa mji mkuu wa ukhalifa. Kipaumbele wa Madina kilikwisha. Muawiya mwenyewe aliweza kuimarisha utawala wake juu ya maeneo yote yaliyotawaliwa na Waislamu. Aliteua watu aliowasadiki kama magavana wa Misri na Iraq. Alitumia muundo wa utawala wa Bizanti na Uajemi uliokuwepo katika sehemu mbalimbali zilizotwaliwa na Waislamu kutoka milki hizi akawapa pia Wakristo vyeo katika idara mbalimbali za utawala wake; wanaojulikana hasa ni familia ya mwalimu Mkristo Yohane wa Dameski.


Muawiya alifaulu kukubaliwa kwa mwanawe Yazid kuwa mfuasi wake katika ukhalifa ingawa kwa kumtangaza alivunja mapatano yake na Hasan ibn Ali.

Chini ya serikali ya Muawiya eneo la Waislamu likaendlea kupanuliwa katika Maghreb na pia Uajemi ya Mashariki. Lakini alishindwa kuteka Bizanti ingawa jeshi lake lilishambulia Konstantinopoli mara mbili.

Muawiya I aliaga dunia mjini Dameski tarehe 18 Aprili 680.

Watawala Waumawiya katika mji mkuu Dameski
661–750
Name kuanzia hadi
Mu'awiya I 661 680
Yazid I 680 683
Mu'awiya II 683 684
Marwan I 684 685
Abd al-Malik 685 705
al-Walid I 705 715
Sulayman 715 717
Umar Ibn Abd al-Aziz 717 720
Yazid II 720 724
Hischam 724 743
al-Walid II 743 744
Yazid III 744
Ibrahim 744
Marwan II 744 750


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamuawiya kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.