Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:MBENAWILL

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

LUGHA

JE KUNA LUGHA BORA KULIKO NYINGINE ?

Lugha ni nini ? Neno lugha linaelezwa kwa maneno tofauti na wataalamu mbalimbali. Yafuatayo ni maelezo tofauti kuhusu maana ya lugha: Lugha nimfumo wa sauti za nasibu zenye kutoa wazo au mawazo kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Pia kunamaana nyingine ya lugha isemayo kwamba lugha ni mkusanyiko wa alama za nasibu ambazo zinapangwa kwa kufuatakanuni fulani. Uchaguzi wa hizialama pamoja na kanuni za matumizi hukubaliwa na jamii husika inayotumia lugha hiyo. Pia kuna maelezo ya lugha kama sauti za nasibu zinazowezesha watu wote ya jamii fulani au wengine wasio wa jamii hiyo waliojifunzamfumo wa utamaduni huo kuweza kuwasiliana. Ukiangalia maana hizi na nyinginezo zilitolewa na wataalamu mbalimbali unaweza kujifunza kwamba licha ya maneno tofauti yaliyotumika kueleza maana ya lugha yapo maneno ya msingi yanayopatikanatakribani katika maana zote. Maneno hayo ni yafuatayo:mfumo, nasibu, sauti,alama,jamii ya watu watumiaji na mengine. Neno mfumo linaweza kuelezwa kwa kifupi kama hali ya vitu tofauti kufanya kazi kwa kuhusiana kuhusu jambo kuu moja, kwa mfano, mfumo wa kusukuma damu kwenye mwili wa binadamu unajumuisha viungo kadhaa kama vile moyo,mishipa ya damu na damu yenyewe.Hivyo moyo, mishipa na damu yenyewe vyote vinahusika kukamilisha mzunguko wa damu mwilini. Mfano huu unashabiana na jinsi lugha inavyoundwa kwani ndani yake kuna sarufi,sauti,uumbaji wa maneno,na mengine ambayo yote yanategemeana kufanya ukamilfu wa lugha.Maelezo haya yanathibitisha kabisa kwamba lugha ni mfumo kama ilivyo mifumo mengine mbalimbali. Kwa upande wa nasibu tunapata maana kwamba lugha inachukua alama inazotumia kuwakilisha vitu au dhana mbalimbali za yaliyopo duniani kwa bahati tu bila kuwepo uhusiano ulio dhahiri. Alama ni kitu ambacho uwakilisha kitu kingine,kwa mfano, rangi nyekundu inaweza kutumika kuwakilisha hatari.Vivo hivyo kwa upande wa lugha kwa kuwa maneno tutamkayo au kuandika si vitu, maumbo au dhana zenyewe halisi bali uwakilisha tu. Ukisema muhogo ni neno ambalo ni alama tu yenye kuwakilisha mzizi husika ambao ni chakula, neno lenyewe si huo muhogo.Pia lugha kwa utamaduni wa asili ni ya kutamkwa au kuongewa, kwa maana binadamu wa mwanzo walitumia alama za mawasiliano kwa sauti za kutoka midomoni mwao.Kwa maneno rahisi ni kusema kwamba lugha yamdomo au kuongea ndiko kulianza kabla ya kuandika au maandishi.Alama za lugha za maandishi zilitumika miaka mingi baadaye baada ya ufumbuzi wa alama za maandishi ambazo pia zilitumika kuwakilisha vitamkwa vya mdomoni.Hivyo basimaneno yatumikayo yanaweza kuwekwa katikamakundi makuu mawili ya alama yaani alama za kutamkwa mdomoni(za sauti) na alama za kuandikwa.Sifa nyingine ya lugha inaibainisha lugha kuwa chombo cha binadamu pekee.Hii ina maana kwamba nibinadamu pekee ndiye aliyepewa uwezo wa kumiliki na kutumia lugha, viumbe wengine hawana lugha isipokuwa wanawezapia kuwasiliana.Kwa hiyo tofauti hapa ni kwamba binadamu anatumia lugha kwa mawasiliano lakini viumbe wengine wanawasiliana bila ya kutumia [[lugha[[.Hali hii inaweza kupewa tafsiri kwamba ilikuwa ni mpango wa Mungu wa kumpatia binadamu chombo cha mawasiliano kilicho tofauti na mtindo wa mawasiliano wa viumbe wengine.Hii pia inathibitishwa na nadharia mojawapo inayojadili asili ya lugha ambayo ni nadharia ya maumbile ya binadamu. Wapo watu wanaodhani kwamba kuna lugha fulani ni bora kuliko nyingine. Kundi hili lina hoja au madai kadhaa wanayotumia kutetea upande wao. Baadhi ya madai hayo ni haya: kwanza wanasema kuna baaadhi ya lugha zina maneno machache,sarufi rahisi au nyepesi na sauti chache. Kwa madai haya wanafikiri kwamba lugha zenye maneno mengi sarufi ngumu na sauti nyingi ni bora kuliko nyingine. Pia wanasema lugha zilizosanifishwa ni bora kuliko zile zisizofanyiwa usanifishaji. Kwa mfano,kwa madai haya Kiingereza kwa kuwa ni lugha iliyosanifishwa ni bora kuliko Kitindiga cha Watindiga wa Tanzania.Madai mengine ni kuwa baadhi ya lugha zinatumika kwenye ibada au huduma na mawasiliano na Mungu hivyo basi wanadai kwamba lugha hizo ni bora kuliko nyingine. Mifano ya lugha hizo ni Kilatini, Kiarabu na Kihebrania.Watu wa kundi hili vilevile wanatoa madai ya kwamba lugha fulani ni bora kuliko nyingine kwa kuwa ni kongwe. Yaani kuwa na umri mkubwa tu kuna ipa lugha ubora. Hapa kuna mfano wa Kigiriki.Kigezo kingine wanachotoa wale wenye mawazo ya ubora wa lugha fulani kupita nyingine ni nafasi ya lugha kimataifa. Wanaona kwamba lugha yenye nafasi ya matumizi kimataifa ni bora kuliko nyingine.Kwa mantiki hii wanazipa nafasi lugha za kimataifa za Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, na nyinginezo. Je, madai haya yana mantiki ya kitaalamu kuhusu ubora au umuhimu wa lugha ? Kimsingi ni kweli kwamba lugha hazifanani kwa vigezo vinavyotolewa na watu wa kundi hili lakini swali muhimu la kujiuliza ni je, hivi ni vigezo sahihi vya kutumia kuamua kuhusu umuhimu wa lugha ? Kundi lingine la watu linasema kwamba hapana kwani vigezo sahihi vya kupima ubora wa lugha inabidi viegemee kwenye kazi kuu ya lugha pamoja na sifa kuu za kipekee za lugha zote duniani.Hivyo basi kundi hili linasema kwamba kazi kuu ya lugha zote duniani ni mawasiliano.Kwa kuzingatia kazi hii, inaonekana kwamba lughazote duniani zinawawezesha watumiaji wa lugha hizo kuwasiliana kati yao.Hakuna lugha hatamoja duniani ambayo watumiaji wake hawawezi kuwasiliana kwa lugha yao hiyo.Kimsingi hili haliwezi kutokea duniani ikiwa hivyo maana yake hiyo si lugha yao hivyohaiwezekani kusema watu hao wanashindwa kuwasiliana kwa lugha yao.Kwa upande wa sifa za kipekee za lugha kuna mambo kama :uwezo wa lugha kuzalisha vitu vipya kwa mfano msamiati mpya, tungo mpya, maana mpya na kadhalika; kuna dhana ya unasibu yaani lugha zote duniani ni matunda ya unasibu kwa maana kwamba alama na maana havina uhusiano wa moja kwa moja]]; uwezo wa lugha kutoa nafasi ya kubadilishana majukumu baina ya watumiaji wa lugha kwa maana muongeaji na msikilizaji huwa wanabadilishana nasafi zao; umaalumu wa maneno katika matumizi kwa maana yapo maneno yenye maana maalumuyenye kutofautisha kwa mfano jinsia. Kwa mfano binti ni neno linalomlenga mtu kijana wa jinsi ya kiume na kijana lina maana ya mtu kijana wa jinsi ya kiume; uwezo wa lugha kueleza kuhusu vitu vya mbali na vya dhahania, kwa mfano, lugha inampa mtumiaji nafasi ya kuweza kuongea kuhusu mtu ambaye yupo mbali na wala hawaonani na mwenyewe hata hajui kwamba kuna mtu upande mwingine wa dunia anaongea kuhusu yeye. Vivo hivyo mtumiaji wa lugha anaweza kuongea kuhusu vitu visivoonekana, visivyogusika, visivyoonjeka, visivyonusika na visivyogusika. Kwa mfano, upendo ni neno la dhahania. Kwa kuzingatia kazi kuu ya lugha na sifa za kipekee za lugha ni rahisi mwingine anayezingatia haya kupinga mawazo kwamba kuna lugha bora kuliko nyingine kwani lugha zote ni sawa kwa kuwa zinafanya kazi ile kuu ya mawasiliano na pia zote zina sifa sawa sawa za kipekee licha ya ukweli kwamba kuna lugha zina maneno machache, sio lugha za ibada, sio kongwe, sio za kimataifa na hazikusanifiwa Kwa mfano, lugha yenye maneno machache ipo hivyo kulingana na kiwango cha maendeleo cha watumiaji wake na watumiaji hao hawapungukiwi mawasiliano kwani maneno [[]]waliyonayo yanawiana na kiwango chao cha mahitaji ya mawasiliano hivyo hakuna upungufu wa kueleza yale yaliyopo kwenye kiwango chao cha maendeleo kiutamaduni kiuchumi, kisiasa, kijamii na kadhalika. Kama kuna dhana mpya kutoka nje ya kiwango chao basi lugha ina uwezo wa kuja ma msamiati mpya kwa kuunda kutokandani ya jamii na utamaduni wao na jinsi wanavyolipokea jambo hilo jipya au la lugha itakopa dhana pamoja na msamiati kutoka [[nje linakotoka jambo hilo jipya. Ukopaji si ishara ya uduni wa lugha bali ni sifa chanya ya ukuaji wa lugha yoyote ile. Kwa mfano, ukichukua lugha ya Kiingereza ambayo baadhi ya watu wanafikiri ni lugha bora kuliko nyingine inasemekana imekopa kwa takribani asilimia sabini ya msamiati wake na kati hizo kuna asilimia takribani arobaini kutoka lugha ya Kifaransa.