Meningitis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Tando zinazofunika na kulinda seli ya neva zinaitwa "Meniges"; zukishambuliwa na virusi au bakteria zinaweza kuwaka na kusababisha mvurugo mkali kwenye neva.

Meningitisi ni uvimbe wa tando za uti wa mgongo na ubongo.[1] Kuvimba huku husababishwa na virusi, bakteria au hata kutumia dawa fulani.

Meningitis ni maradhi yanayoweza kuua, kwa kuwa uvimbe huo hufanyika karibu na ubongo; kwa hiyo ugonjwa huu ni hatari inayodai umwone daktari.

Dalili kuu za ugonjwa huu ni kuumwa na kichwa na shingo, pamoja na homa na kuchanganyikiwa kwa akili, kutapika na kutoweza kustahimili mwangaza na kelele.

Dalili[hariri | hariri chanzo]

  • Kichwa kuuma sana.
  • Kutokuwa na akili timamu, hii hutokea kwa takriban asilimia 44 ya wagonjwa.[2]
  • Kutoweza kustahimili mwangaza na kelele.
  • Uvimbe juu ya kichwa hutokea kwa watoto wa umri wa chini ya miezi sita.
  • Dalili zingine zinazopatikana kwa watoto ni kuumwa kwa miguu, kuhisi baridi kali na ngozi kugeuka rangi.[3]
Mgonjwa mahututi wa Meningitis

Sababu[hariri | hariri chanzo]

Kwa watoto wenye umri wa chini ya miezi mitatu, ugonjwa huu husababishwa na group B streptococcus. Wengine ambao hukaa kwenye matumbo ya binadamu ni kama Escherichia coli

Virusi[hariri | hariri chanzo]

Virusi vinavyosababisha Meningitis ni kama enterovirus, herpes simplex virus type 2, varicella zoster virus, herpes zoster, mumps, HIV, na Lymphocytic choriomeningitis.

Meningitis pia huweza kusababishwa na kuenea kwa saratani hadi kwenye ubongo.[4]

Kukinga[hariri | hariri chanzo]

Meningitis hukingwa kwa kutumia chanjo. Katika nchi nyingi, watoto wengi hupewa chanjo ya kuzuia Haemophilus influenzae ambayo huondoa bakteria hizo kwa miili ya watoto. Hata hivyo, chanjo hii ni ghali.

Chanjo ya Bacillus Calmette-Guérin imeonyesha kupunguza kiwango cha ugonjwa huu kuenea.

Dawa zinazotumika kuzuia ni kama rifampicin, ciprofloxacin au ceftriaxone.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Sáez-Llorens X, McCracken GH (Juni 2003). "Bacterial meningitis in children". Lancet 361 (9375): 2139–48. doi:10.1016/S0140-6736(03)13693-8 . PMID 12826449 .
  2. Attia J, Hatala R, Cook DJ, Wong JG (Julai 1999). "The rational clinical examination. Does this adult patient have acute meningitis?". JAMA 282 (2): 175–81. doi:10.1001/jama.282.2.175 . PMID 10411200 .
  3. Theilen U, Wilson L, Wilson G, Beattie JO, Qureshi S, Simpson D (Juni 2008). "Management of invasive meningococcal disease in children and young people: Summary of SIGN guidelines". BMJ (Clinical research ed.) 336 (7657): 1367–70. doi:10.1136/bmj.a129 . PMC 2427067 . PMID 18556318 . Full guideline page
  4. Chamberlain MC (Mei 2005). "Neoplastic meningitis". Journal of Clinical Oncology: official journal of the American Society of Clinical Oncology 23 (15): 3605–13. doi:10.1200/JCO.2005.01.131 . PMID 15908671 .
Rod of Asclepius2.svg Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Meningitis kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.