Kizunguzungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kizunguzungu
ICD-10R42.
ICD-9780.4
DiseasesDB17771
eMedicineneuro/693
MeSHD004244

Kizunguzungu ni hali ya kupoteza utambuzi na uimara [1] inaweza kutumika kwa maana ya kuhisi kuzunguka, udhaifu wa misuli, inachukuliwa kama kutokuwa na uimara [2] au kwa hisia zisizo maalum kama vile kizunguzungu au upumbavu. [3]

Mtu anaweza kupata kizunguzungu kwa kushiriki shughuli kama za kuzunguka.

  • Kisulisuli ni neno maalumu la kimatibabu linalotumika kuelezea hisia ya kuzunguka au kuhisi vitu vya mazingira vinakuzunguka Watu wengi wamekuta kisulisuli kusumbua sana na mara nyingi inatarifiwa kuhusiana na kichefuchefu na kutapika Hii inawakilisha asilimia 25 za kesi za matukio ya kizunguzungu. [4]
  • Ukosefu wa msawazo ni hisia za kutokuwa kwenye usawa,na mara nyingi kuanguka kwa kufuata mwelekeo maalumu ni sifa yake kuu Hali hii mara nyingi haihusishwi na kichefuchefu au kutapika.
  • hali yakupoteza fahamu ni ubongo hewa, udhaifu wa misuli na hisia za kukata tamaa kinyume na kuzirai, ambayo ni kweli watazimia.
  • kizunguzungu kisicho lasimi mara nyingi ni chanzo cha magonjwa ya akili. Ni utambuzi wa kuzingatiwa kwa upekee na wakati mwingine kinaweza kusababiswa na kupumua kwa kasi. [11]

{0kiharusi{/0} ni chanzo cha kizunguzungu pekee katika 0.7% ya watu waliokuwamo kwenye chumba cha dharura. [4]

Hali zinazoendana na uuguzi (tiba)[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ndogo kwa sababu kizunguzungu ni dalili ya kawaida Ya magonjwa mengi. Hata hivyo, vipengele vya kawaida vinaweza kuhahinishw kama ifuatavyo: 40% vestiburi ya pembeni inayofanya kazi vibaya, 10%jeraha kwenye mfumo mkuu wa fahamu, 15% ugonjwa wa akili, 25% kuzirai / kukosa msawazo, na 10%kizunguzungu kisicho lasimi. [5] Hali ya matibabu ambayo mara nyingi ina'kizunguzungu' kama dalili ni pamoja na: [5] [6] [7] [8]

  • ujauzito
  • shinikizo ya damu kuwa chini (msukumo kuwa chini))
  • upungufu wa hewa safi (haipoksemia)
  • upungufu wa madini chuma mwilini(safura)
  • sukari kushuka(hypoglesia)
  • matatizo kwenye homoni (kwa mfano, ugonjwa wa tezi, hedhi, mimba)
  • tatizo la kuwa na hofu au wasiwasi
  • kupumua kwa kasi
  • wasiwasi
  • kunyongonyea au kufadhaika
  • kupoteza uwezo wa kuona , usawa, na uwezo wa kupokea matambuzi harisi
  • kupatwa tatizo la misuli
  • ugonjwa wa minere
  • vestibuli ya mishipa ya fahamu
  • uvimbe katika sikio la ndani
  • uvimbe katika sikio la
  • kupoteza hisia za kusikia
  • kuwa na mwendelezo wa magonjwa sugu
  • gonjwa linalosababishwa na mdudu anayeitwa Tolosa
  • kipanda uso
  • kushikwa na misuli

Taratibu[hariri | hariri chanzo]

hali nyingi husababisha kizunguzungu kwa sababu sehemu mbalimbali za mwili zinahitajika kutunza usawa ikiwa ni pamoja na kudumisha usawa ndani ya sikio, macho, misuli, mifupa, na mfumo wa fahamu. [7]

sababu za kawaida zinazoweza kusababisha kizunguzungu ni pamoja na:

  • damu kidogo kupelekwa kwenye ubongo kutokana na:
    • kuanguka ghafla kwa shinikizo la damu [7]
    • matatizo ya moyo au kupasuka kwa ateri[7]
  • kupoteza uwezo wa kuona vizuri[7]
  • matatizo ndani ya sikio [7]
  • katika uponyaji wa ubongo na mishipa ya fahamu kwa kutumia madawa [7]

Epidemolojia[hariri | hariri chanzo]

Kiasi cha 20-30% ya watu imeripoti kuwa wamepatwa na kizunguzungu mwakka jana [4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "dizziness" at Dorland's Medical Dictionary
  2. "Chapter 14: Evaluation of the Dizzy Patient". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-27. Iliwekwa mnamo 2009-08-06.  Unknown parameter |= ignored (help)
  3. "UpToDate Inc.". 
  4. 4.0 4.1 4.2 Neuhauser HK, Lempert T (Novemba 2009). "Vertigo: epidemiologic aspects". Semin Neurol 29 (5): 473–81. PMID 19834858. doi:10.1055/s-0029-1241043. 
  5. 5.0 5.1 Chan Y (Juni 2009). "Differential diagnosis of dizziness". Curr Opin Otolaryngol Head Neck Surg 17 (3): 200–3. PMID 19365263. doi:10.1097/MOO.0b013e32832b2594. 
  6. Tusa RJ (Machi 2009). "Dizziness". Med. Clin. North Am. 93 (2): 263–71, vii. PMID 19272508. doi:10.1016/j.mcna.2008.09.005. 
  7. 7.0 7.1 7.2 7.3 7.4 7.5 7.6 [21] ^ kizunguzungu na Msongo kwenye kazi(mwongozo) wa merk Archived 5 Julai 2018 at the Wayback Machine.
  8. Bronstein AM, Lempert T (2010). "Management of the patient with chronic dizziness". Restor. Neurol. Neurosci. 28 (1): 83–90. PMID 20086285. doi:10.3233/RNN-2010-0530. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]