Maria Goretti
Maria Teresa Goretti (Corinaldo, Ancona, Italia, 16 Oktoba 1890 - Nettuno, Lazio, 6 Julai 1902) alikuwa bikira Mkristo ambaye, baada ya kupitia utoto katika ufukara akimsaidia mama yake mjane katika shughuli za nyumbani na kudumu katika sala, alikataa mfululizo kuzini na jirani yake Alessandro Serenelli, mpaka huyo akamchoma mara 14 mfululizo kwa kifaa cha chuma[1].
Akizidi kuchomwa, Maria alisisitiza msimamo wake: "Usifanye, ni dhambi!"
Kabla hajafa hospitalini, Maria alimsamehe muuaji wake kwa kumtakia awe naye mbinguni.
Baada ya miaka mitatu gerezani, Alessandro aliongoka na alipotoka alikwenda kuomba msamaha wa mama wa Maria, akakubaliwa kwa hoja kwamba, "Mwanangu amekusamehe wakati wa kufa, nami siwezi kufanya tofauti". Kesho yake walipokea ekaristi pamoja.
Halafu akaishi utawani kwa Wakapuchini wa Macerata hadi alipofariki mwaka 1970.
Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 27 Aprili 1947 na kuwa mtakatifu tarehe 24 Juni 1950, wakihudhuria mama yake na muuaji vilevile.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe ya kifodini chake, 6 Julai ya kila mwaka[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Filamu juu yake
[hariri | hariri chanzo]- Cielo sulla palude, kwa ajili ya sinema, iliongozwa na Augusto Genina, Italia 1949
- Maria Goretti, kwa ajili ya televisheni, iliongozwa na Giulio Base, Italia 2002
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Beatificationis seu declarationis martyrii Mariae Goretti, Roma, 1938-1939 (nyaraka za kesi ya kumtangaza mwenye heri).
- Compendium vitae virtutum ac miracolorum Beatae Mariae Theresiae Goretti, Typis Polyglottis Vaticani, 1950 (nyaraka za kesi ya kumtangaza mtakatifu).
- A proposito di Maria Goretti: santità e canonizzazioni: atti della Commissione di studio istituita dalla Congregazione per le cause dei santi il 5 febbraio 1985, Città del Vaticano, Libreria Editrice Vaticana, 1986.
- Giovanni Alberti, Maria Goretti, Città Nuova Editrice, 1980. ISBN 88-8386-150-7.
- Giordano Bruno Guerri, Povera santa, povero assassino. La vera storia di Maria Goretti, Mondadori, Milano, 1985 - toleo jipya lililorekebishwa na kuongezewa Bompiani, Milano, 2008.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Friends of Maria Goretti
- Saint Maria Goretti Ilihifadhiwa 12 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
- Pontificia Basilica Madonna delle Grazie e Santa Maria Goretti di Nettuno Ilihifadhiwa 2 Novemba 2012 kwenye Wayback Machine.
- Sito del santuario di Corinaldo
- Messaggio di Giovanni Paolo II in occasione del centenario della morte, 6 luglio 2002
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |