Kila mtu anaweza kuhariri makala yoyote, kutoa makosa ya lugha, kutohoa maneno na kuendeleza na kukuza makala, kwa kuandika kwa ufupi au kwa urefu. Tunakushauri ujiandikishe na kufungua akaunti. Angalia Wikipedia:Mwongozo ili ujifunze unavyoweza kuhariri au kusanifisha ukurasa. Usisite kushiriki; kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano, na hautaisha kamwe. Kamusi elezo itaimarika vizuri zaidi kila wakati. Angalia ukurasa wa jumuia, ukurasa wa jamii, na ule wa makala za msingi za kamusi elezo ili kung'amua unaweza kufanya kazi zipi ili kuboresha Wikipedia.
Vimondo (pia: meteori au meteoridi) ni magimba madogo ya angani yanayozunguka jua. Yanaweza kuangukia duniani yakionekana kama moto angani. Ukubwa wa kimondo ni kuanzia punje ya mchanga hadi kufikia kipenyo cha mita kadhaa. Hivyo kimondo ni kidogo kuliko asteoridi na kikubwa kushinda vumbi la angani. Obiti ya kimondo inaweza kuingiliana na obiti ya dunia au sayari nyingine. Kimondo kikilikaribia gimba la angani kubwa zaidi kinavutwa nalo.
Kikikaribia mno dunia yetu kinaingia katika angahewa na kuanguka chini kwa kasi kubwa sana. Njiani kinapashwa moto kutokana na shindikizo la hewa dhidi yake. Kiasi cha joto kinatosha kuchoma kabisa kimondo kidogo hewani. Hii inaonekana kwa macho matupu kama mstari wa moto angani. Kama kimondo ni kikubwa zaidi ni sehemu zake za nje tu zinazochomwa na kiini kinagonga uso wa dunia.
Kati ya vimondo kumi vikubwa kabisa duniani ambavyo mabaki yake yanaonekana, kimojawapo ni Kimondo cha Mbozi nchini Tanzania. ►Soma zaidi
Picha nzuri ya wiki
TANGAZO LA KIFO cha Ingo Koll au Kipala kilichotokea tarehe 10, Julai, 2023 nchini Ujerumani. Kipala alikuwa mchangiaji mashuhuri wa Wikipedia kuanzia Disemba 2005 hadi Juni 28, 2023. Siku kumi na mbili mbele tangu kuhariri Wikipedia yetu kwa mara ya mwisho, Mola Jalali Muumba wa mbingu na ardhi, alitwaa kiumbe chake. Kipala atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuhariri Wikipedia hii. Kwanza akiwa kama msimamizi (admin) baadaye mrasimu (bureaucrat) ambaye ametoa haki za usimamizi kwa wakabidhi ama wasimamizi wengine kama Muddyb, Antoni na wengine wengi tu. Miaka kumi na nane ya kusimamia na kutunga makala mbalimbali itakumbukwa hadi mwisho wa dunia ya Wikipedia. Kipala amechangia makala za aina mbalimbali ikiwemo, muziki, filamu, tiba, elimu ya nyota, dini, siasa, demografia, jiografia, sayansi, na mengine mengi. Amepata kuwa msaada mkubwa kwa wachangiaji wapya kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Alianzisha Jenga Wikipedia ya Kiswahili kwa lengo la kuboresha makala mbalimbali na kutoa mafunzo kwa watu wapya. Pengo lake halitazibika. Sisi wanajumuia ya Wikipedia ya Kiswahili tunasikitika kutangaza kifo chake!
Takwimu ya Wikipedia ya Kiswahili
Idadi ya makala: 78,763
Idadi ya kurasa zote: 169,610 (pamoja na kurasa za watumiaji, majadiliano, msaada n.k.)
Katika mwezi wa Agosti 2020 wikipedia ya Kiswahili iliangaliwa mara milioni 1.73 hivi, ambayo ni sawa na mara 55,800 kwa siku au mara 2,326 kila saa. Asilimia 52 za wasomaji wetu wako Tanzania, asilimia 13 wako Kenya, asilimia 18 wako Marekani na mnamo asilimia 10 wako Ulaya.
(fungua anwani kwa browser yako, ondoa majina yaliyopo na ingiza jina la makala (hadi makala 10) unayopenda. Unaweza kubadilisha kipindi cha taarifa utakachoona; takwimu kabla ya 2015 hapa)
na makala 100 zilizotazamiwa zaidi "Topviews" kwa kipindi fulani.
(unachagua kati ya makala 100 kwa mwezi au kwa siku)
Kamusi elezo ya Wiki ni kamusi elezo huru iliyo chini ya Shirika Lisilo la Kiserikali la Wikimedia Foundation, ambalo linasimamia miradi mingine mbalimbali ambayo imeorodheshwa hapo chini. Mpaka sasa miradi inayopatikana Kiswahili ni Wikipedia na Wikamusi. Wikitabu imewekwa Kiswahili lakini bado ni tupu. Mengine inapatikana Kiingereza pamoja na lugha tofauti.