Kiriako mkaapweke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Kiriako.

Kiriako mkaapweke (kwa Kigiriki: Ὅσιος Κυριάκος ὁ Ἀναχωρητής, Hosios Kyriakos ho Anachōrētēs[1]
; Korintho, Ugiriki, 9 Januari 449 - Pango la Mt. Chariton, Palestina, 557) alikuwa mmonaki kwa muda wa miaka 90 hivi.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Septemba[2] au 10 Novemba.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mtoto wa padri Yohane, na ndugu wa askofu Petro wa Korintho, alifanywa mapema msomaji kanisani.

Akisoma Biblia alitamani kuishi kwa utakatifu, hivyo kabla ya kufikia umri wa miaka 18, alijiondokea akahiji Yerusalemu.

Baadaye alijiunga na monasteri akapata uongozi wa kiroho wa watakatifu Eutimi Mkuu na Gerasimo wa Yordani.

Baadaye tena aliishi peke yake akakaa kimya kabisa miaka 10.

Alipofikia miaka 37 alipewa daraja takatifu ya ushemasi, na miaka kadhaa baadaye ile ya upadri.

Kisha kuishi miaka 30 tena monasterini akarudi jangwani ili aishi upwekeni lakini watu walianza kumtafuta ili wapate miujiza kwa maombezi yake. Ndiyo sababu alihamahama hadi kifo chake[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]