Ignas wa Loyola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ignas wa Loyola alivyochorwa na Peter Paul Rubens.

Ignas wa Loyola (kwa Kieuskara Inigo Loiolakoa, kwa Kihispania Ignacio de Loyola; Loyola, Guipúzcoa, leo nchini Hispania, 1491 - Roma, Italia, 31 Julai 1556) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki maarufu hasa kama mwanzilishi wa Shirika la Yesu na wa mtindo wa mazoezi ya kiroho.

Alitangazwa na Papa Paulo V kuwa mwenye heri tarehe 27 Julai 1609, halafu Papa Gregori XV alimtangaza mtakatifu tarehe 12 Machi 1622.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Patakatifu pake huko Loyola, palipojengwa mahali alipozaliwa.
Ignas katika deraya yake kama askari.
Njozi za Ignas.
Ignas kama mkuu wa shirika.
Sanamu yake huko Belo Horizonte, Brazil.

Sala yake[hariri | hariri chanzo]

Pokea, Bwana, hiari yangu yote.

Pokea kumbukumbu, akili na utashi wote.

Vyovyote nilivyonavyo au kuvimiliki nimejaliwa na wewe: nakurudishia vyote na kuukabidhi utashi wako uvitawale.

Unijalie tu upendo wako na neema yako, nami nitakuwa tajiri kutosha, nisitamani kitu kingine chochote.

Maono ya Ignas wa Loyola aliyoonyeshwa Mungu Baba na Mwana.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo ya Kiswahili[hariri | hariri chanzo]

  • A. JOU, S.J., Kazaliwa Kupigana Vita, Simulizi juu ya Mt. Inyasi wa Loyola kwa ajili ya Vijana (hasa wa kiume) – tafsiri ya Ofisi ya Taifa ya Utume wa Sala, Tanzania – ed. Ofisi ya Taifa ya Utume wa Sala, Tanzania – Dodoma 2001 – ISBN 0856-5589

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

Muhimu zaidi

Mengine

Maandishi[hariri | hariri chanzo]

Historia ya maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.