Shirika la Yesu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kanisa la Saint Pierre de Montmartre Paris (Ufaransa).
Mchoro wa ukutani wa Johann Christoph Handke kuhusu Papa Paulo III kupitisha sheria za shirika.

Shirika la Yesu (kwa Kilatini Societas Iesu, kifupi S.J. au S.I. au SJ au SI) ni shirika kubwa la watawa wanaume 19,216 katika Kanisa Katoliki, lililoenea katika nchi 112 za kontinenti 6.

Wanashirika wanaitwa Wajesuiti na ni maarufu pia kwa elimu yao ya juu katika fani mbalimbali, za kidunia na za kidini.

Mwanzilishi wake ni Ignas wa Loyola ambaye, kisha kuacha jeshi, alifuata kwa juhudi zote maisha ya kiroho na kutunga Mazoezi ya Kiroho ili kuongoza watu wamfuate Yesu Kristo.

Mwaka 1534, Ignas alikusanya vijana sita wakaweka nadhiri za ufukara, useja mtakatifu na utiifu, halafu ile ya kumtii daima Papa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Mafundisho ya Papa Benedikto XVI[hariri | hariri chanzo]

Hati za Wajesuiti[hariri | hariri chanzo]

Tovuti za Wajesuiti sehemu mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Afrika[hariri | hariri chanzo]

Asia-Oceania[hariri | hariri chanzo]

Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Amerika Kaskazini[hariri | hariri chanzo]

Amerika Kusini[hariri | hariri chanzo]

Vyombo vya habari[hariri | hariri chanzo]

Kigezo:Tasafiri