Hillary Rodham Clinton

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Hillary Clinton)
Hillary Clinton, mnamo 2016.
Hillary Clinton, Manchester, New Hampshire, 2016

Hillary Rodham Clinton (jina la kuzaliwa ni: Hillary Diane Rodham 26 Oktoba 1947) ni seneta kutoka katika jimbo la New York, Marekani. Hilary vilevile ni mwanasheria.

Ameolewa na rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton. Wakati mumewe alipokuwa rais, Hilary alipewa jina la Mwanamke wa Kwanza au Mke wa rais wa Marekani. Alikuwa Mwanamke wa Kwanza wa Arkansas kabla ya kuwa Mwanamke wa Kwanza wa Marekani.

Ameanza kufanya kazi kama Seneta mnamo tarehe 3 Januari ya mwaka wa 2001. Hillary Clinton alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa seneta wa New York. Aliendelea kuwania tena kiti hicho cha Useneta katika uchaguzi wa mwaka 2006, ambapo pia aliibuka mshindi.

Maisha ya awali na elimu[hariri | hariri chanzo]

Hillary Diane Rodham alizaliwa mjini Chicago, Illinois. Jina la babake ni Hugh Rodham, Sr., na jina la mamake ni Dorothy Emma Howell Rodham. Pia ana ndugu wa kiume wawili, Hugh na Tony.

Alipata elimu yake katika shule ya Maine East High School na Maine South High School. Alimaliza elimu yake ya awali kunako mwaka wa 1965, na baada ya hapo akaenda kujiandikisha katika chuo cha Wellesley, karibu na mji wa Boston.

Mnamo mwaka wa 1969, Rodham alielekea Chuo cha Sheria, kilichokuwa kinamilikiwa na Yale. Baada ya hapo akapata digrii yake ya ualimu wa sheria katika Chuo Kikuu cha Yale mnamo mwaka wa 1973. Kisha akawa anafanya kazi ya kujitolea katika Kutuo cha Kufundishia Watoto cha Yale, kilichokuwa kinajulikana kwa jina la Yale Child Study Center.

Ndoa na familia[hariri | hariri chanzo]

Wakati anafanya kazi kama mwanachama wa kitengo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Arkansas, akaolewa na Bill Clinton ambaye naye alikuwa akifanya kazi hiyohiyo aliyokuwa anafanya mkewe katika Chuo Kukuu hicho. Wote walifahamiana wakati wanasoma katika Chuo cha Sheria cha Yale. Kwa pamoja wamebarikiwa kupata mtoto mmoja pekee aitwaye Chelsea Clinton, aliyezaliwa tarehe 27 Februari 1980.

Kuwa Mwanamke wa Kwanza[hariri | hariri chanzo]

Wakati alipokuwa Mwanamke wa Kwanza, alijaribu kubadilisha mfumo wa huduma ya afya. Kuna baadhi ya watu wakawa wanapinga suala hilo kwa-kuwa mikutano mingi ya mpango huo ilikuwa ikifanyika kwa siri, si katika hadhara. Mwishowe watu wengi wakawa hawataki badiliko lolote lile katika sekta hiyo, hivyo suala likafeli.

Jambo lingine ambalo limetokea wakati ni Mwanamke wa Kwanza ni pale jamii ilipogundua kwamba Bill Clinton alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamke mwingine nje, Monica Lewinsky. Kulikuwa na mzozo mkubwa katika ndoa hiyo na Clinton alipelekwa mahakamani lakini kesi ilisitishwa.

Useneta[hariri | hariri chanzo]

Alipoamua kutaka kuwa Seneta, akachagua kuwa kuwa Seneta wa New York japokuwa haishi huko. Baadhi walimlaumu kwa hilo. Alielekea huko akashinda katika uchaguzi wa awali na wa pili pia, uliofanyika mwaka 2006.

Wakati vita vya Iraki vinataka kuanza, alipigia kura vita hivyohivyo. Baadaye akageuka na kutaka vikosi vya Jeshi la Marekani viache kupigana huko nchini Iraki.

Kampeni za Urais[hariri | hariri chanzo]

Hilary pia ni mmoja kati ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2008. Aligombea kupitia Chama cha Demokrasia (kwa Kiingereza Democratic Party).

Hillary Clinton alitumia fedha nyingi kuliko mtu yeyote yule katika uchaguzi mkuu wa rais na alifikiriwa na vyombo vya habari vingi na baadhi ya wanasiasa kuwa na nafasi kubwa ya ushindi lakini chama chake kilimchagua Barack Obama kama mgombea.

Mwaka 2016 alifaulu kuchaguliwa na chama chake kuwa mgombea urais, lakini katika uchaguzi mkuu wananchi walimpa ushindi Donald Trump.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Orodha ya Wake wa Marais wa Marekani
M. Washington · A. Adams · M. Jefferson Randolph · D. Madison · E. Monroe · L. Adams · E. Donelson · S. Jackson · A. Van Buren · A. Harrison · J. Harrison · L. Tyler · P. Tyler · J. Tyler · S. Polk · M. Taylor · A. Fillmore · J. Pierce · H. Lane · M. Lincoln · E. Johnson · J. Grant · L. Hayes · L. Garfield · M. McElroy · R. Cleveland · F. Cleveland · C. Harrison · M. McKee · F. Cleveland · I. McKinley · Edith Roosevelt · H. Taft · Ellen Wilson · Edith Wilson · F. Harding · G. Coolidge · L. Hoover · E. Roosevelt · B. Truman · M. Eisenhower · J. Kennedy · C. Johnson · P. Nixon · B. Ford · R. Carter · N. Reagan · B. Bush · H. Clinton · L. Bush · M. Obama