Michelle Obama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Michelle Obama.

Michelle LaVaughn Obama (jina la kuzaliwa ni Michelle LaVaughn Robinson), amezaliwa mnamo tar. 17 Januari 1964) ni Mwanasheria wa Kimarekani na ndiyo mke wa Rais wa Marekani Bw. Barack Obama.[1] Huyu ndiye Mwafrika-Mwamerika wa kwanza kuwa Mwanamke wa Kwanza wa Marekani.

Michelle alizaliwa na kukulia kitongoji South Side ya Chicago na kusoma hadi kuelekea katika Chuo Kikuu cha Princeton halafu baadaye katika Kitivo cha Sheria cha Harvard.

Baada ya kumaliza elimu yake hiyo, alirudi Chicago na kukubali kuchukua nafasi ya kazi katika kampuni ya Sidley Austin, halafu baadaye akaja kuwa kama mmoja kati ya wafanyakazi wa meya wa Chicago Bw. Richard M. Daley, halafu baadaye akafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Chicago na Hospitali za Chuo Kikuu cha Chicago.

Michelle Obama ni dada wa Craig Robinson, kocha wa mpira wa kikapu wa Oregon State University. Alikutana na Barack pale alipojiunga na Sidley Austin. Pale Barack Obama alipochaguliwa kuwa kama Seneta, familia ya Obama ikachagua kuishi mjini Chicago South Side kuliko kuishi mjini Washington, D.C.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Frederick, Don. "Barack Obama, 44th president of the United States", Los Angeles Times, 4 Novemba 2008. Retrieved on 2008-11-04. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Orodha ya Wake wa Marais wa Marekani Seal Of The President Of The United States Of America.svg
M. Washington · A. Adams · M. Jefferson Randolph · D. Madison · E. Monroe · L. Adams · E. Donelson · S. Jackson · A. Van Buren · A. Harrison · J. Harrison · L. Tyler · P. Tyler · J. Tyler · S. Polk · M. Taylor · A. Fillmore · J. Pierce · H. Lane · M. Lincoln · E. Johnson · J. Grant · L. Hayes · L. Garfield · M. McElroy · R. Cleveland · F. Cleveland · C. Harrison · M. McKee · F. Cleveland · I. McKinley · Edith Roosevelt · H. Taft · Ellen Wilson · Edith Wilson · F. Harding · G. Coolidge · L. Hoover · E. Roosevelt · B. Truman · M. Eisenhower · J. Kennedy · C. Johnson · P. Nixon · B. Ford · R. Carter · N. Reagan · B. Bush · H. Clinton · L. Bush · M. Obama

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Crystal personal.svg Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Michelle Obama kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.