Fransisko wa Fatima

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha halisi ya Lusia Santos (kushoto) na binamu zake Fransisco na Yasinta Marto, mwaka 1917.
Mahali pa Fatima nchini Ureno.
Sanamu iliyotiwa taji ya Bikira Maria ya Fatima katika kikanisa kilichopo mahali pa njozi.

Fransisko Marto wa Fatima (11 Juni 1908 - 4 Aprili 1919), ni jina la mmojawapo kati ya watoto watatu waliotokewa na malaika wa amani (1916), halafu na Bikira Maria (1917) kwao Fatima, Ureno, pamoja na binamu yake Lusia Santos na dada yake Yasinta Marto.

Njozi hizo zilithibitishwa na Kanisa Katoliki kuwa za kuaminika[1], hata ikaanzishwa kumbukumbu ya Bikira Maria wa Fatima katika liturujia kila tarehe ya njozi ya kwanza, 13 Mei.

Fransisko, pamoja na dada yake mdogo Yasinta, alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 13 Mei 2000, halafu na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 13 Mei 2017, miaka 100 kamili tangu tukio la kwanza.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Papa Pius XII, Papa Paulo VI, Papa Yohane Paulo II, Papa Benedikto XVI na Papa Fransisko walikubali asili ya Kimungu ya njozi za Fatima.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fransisko wa Fatima kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.