Nenda kwa yaliyomo

Felicien Kabuga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Faili:Félicien Kabuga.jpg
Felicien Kabuga.

Felicien Kabuga (amezaliwa 19 Julai 1935) ni mfanyabiashara wa Rwanda, anayeshtumiwa kwa kugharamia na kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994. [1]

Maisha ya zamani[hariri | hariri chanzo]

Kabuga alizaliwa Muniga, katika tarafa ya Mukarange, mkoa wa Byumba, Rwanda ya leo. Kabuga alijenga utajiri wake kwa kumiliki mashamba ya chai kaskazini mwa Rwanda, miongoni mwa shughuli nyingine za kibiashara. [2] Alifikia kumiliki mali ya milioni nyingi [3] na kuwa na uhusiano wa karibu na chama cha MRND cha Juvénal Habyarimana na kundi la Akazu, kikundi kisicho rasmi cha Wahutu wenye msimamo mkali kutoka Rwanda kaskazini ambao walichangia kwa nguvu mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Kabuga amemwoa Josephine Mukazitoni. Binti zao wawili wameolewa na wana wawili wa Habyarimana. [4]

Kabuga alishiriki katika kuanzisha, kugharamia na kusimamia Redio Mille Collines (RTLM; kwa maana "vilima 1000") na jarida la Kangura.[2] [5] Mnamo 1993, katika mkutano wa kutafuta fedha wa RTLM ulioandaliwa na MRND, Félicien Kabuga aliripotiwa kufafanua hadharani madhumuni ya RTLM kuwa utetezi wa "Nguvu ya Hutu". [6] Wakati wa kesi ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR) kuhusu vyombo vya habari vya Rwanda, mtangazaji wa zamani wa RTLM Georges Ruggiu alimtaja Kabuga kama "Mkurugenzi Mkuu wa kituo" mwenye majukumu kama "kusimamia RTLM" na "kuwakilisha RTLM." [7]

Kutoka Januari 1993 hadi Machi 1994, jumla ya mapanga 500,000 yaliingizwa katika Rwanda. Kabuga ametajwa kama mmoja wa waingizaji wakuu wa mapanga haya. [2]

Wakati wa Juni 1994, Kabuga na wengine waliripotiwa kushiriki katika mkutano mjini Gisenyi. Katika mkutano huo, wana MRND wanasemekana kutoa orodha ya Watutsi na Wahutu wasiochukia Watutsi waliowahi kukimbilia Kisenyi kutoka maeneo mengine. Hapa wanasemekana kutunga orodha ya watu waliopaswa kuuawa iliyokabidhiwa kwa wanamgambo wa Interahamwe[8].

Kushtakiwa na ICTR[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 29 Agosti 1998, mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda (ICTR) Carla Del Ponte, alimshtaki Kabuga. Katika mashtaka yaliyorekebishwa tarehe 1 Oktoba 2004, mwendesha mashtaka Hassan Jallow alimshtaki Kabuga kuwa:

 • alifanya njama za kutekeleza mauaji ya kimbari
 • alihusika katika mauaji ya kimbari
 • alichochea moja kwa moja na hadharani kutekeleza mauaji ya kimbari
 • alihusika katika jinai dhidi ya ubinadamu.

Mkimbizi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Juni 1994, wakati Rwanda ilivamiwa na jeshi la RPF, Kabuga alikimbia nchi. Kwanza alijaribu kuingia Uswisi, lakini aliamriwa kuondoka tena. Alienda Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na baadaye aliaminika kuwa akiishi Nairobi, Kenya.

Mnamo Septemba 1995, kabla ya mashtaka yoyote na kabla ya kutajwa kama mpangaji wa tuhuma za mauaji, Kabuga alisajili na kuendesha biashara inayoitwa 'Nshikabem Agency' jijini Nairobi, iliyokuwa na ofisi katika eneo la Kilimani lililopo kando ya barabara ya Lenana ya Nairobi. [9] [10]

Mnamo 2003, mfanyabiashara Mkenya aliyewahi kuwasaidia maafisa kutoka Ofisi ya Upelelezi ya Marinai (FBI) kumfuatilia Kabuga aliuawa.[11]

Katika hotuba iliyotolewa mnamo Agosti 28, 2006 wakati wa ziara yake nchini Kenya, aliyekuwa wakati ule seneta wa Marekani Barack Obama alishtumu Kenya kwa "kumruhusu Kabuga kununua kimbilio chake." [12] Serikali ya Kenya ilikana madai hayo na kuelezea madai ya Obama kuhusu Kabuga yalionyesha "dharau kwa wananchi".

Kulingana na ripoti ya Juni 2008 na mwanablogi nchini Norwei aliyejiita "African Press International (API)", Kabuga alikuwa mafichoni huko Oslo. Serikali ya Norwei ilitupilia mbali madai hayo kama si kweli. [13] [14]

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza ahadi ya zawadi ya dola milioni 5 kwa atakayetoa habari inayosababisha kukamatwa kwa Kabuga. [15] Mtandao wa habari wa KTN nchini Kenya uliripoti mnamo Juni 14, 2008 kwamba Kabuga alikamatwa na Polisi Kenya na alikuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Gigiri jijini Nairobi. Baadaye, mtuhumiwa aligunduliwa kuwa mhadhiri wa chuo kikuu, si Kabuga jinsi ilivyodhaniwa hapo awali akaachiliwa. Kulikuwa na habari kuwa Kabuga aliishi Kenya, [16] akiaminika alianya biashara na kupata ulinzi ama kutoka kwa serikali ya Kenya au watu wenye athira ndani ya nchi.

Kukamatwa[hariri | hariri chanzo]

Akiwa na umri wa miaka 84, Kabuga alikamatwa huko Asnières-sur-Seine, karibu na Paris, Ufaransa, mnamo Mei 16 2020 baada ya kuishi miaka 26 kama mkimbizi. Serikali ya Ufaransa imeelezea nia ya kumuona katika mahakama kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa dhidi ya Watutsi wa Rwanda. Alikamatwa na polisi wa Ufaransa kama matokeo ya uchunguzi wa pamoja na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa IRMCT, [17] aliyesaidiwa na Interpol na polisi nchini Rwanda, Ubelgiji, na Marikani . [15]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "Top 10 Most Wanted Criminals in the World 2018". Improb (kwa American English). 2017-12-18. Iliwekwa mnamo 2019-11-21.
 2. 2.0 2.1 2.2 "YouTube". www.youtube.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-06-25.
 3. How the mighty are falling, The Economist, 5 July 2007. Accessed online 17 July 2007.
 4. US Goes To Social Media Hunting For Hardcore Genocide Fugitives chronicles.rw, retrieved 12 August 2019
 5. "Felicien Kabuga - TRIAL International". Retrieved on 2020-05-31. (en-US) Archived from the original on 2019-10-27. 
 6. ICTR Case No. 99-52-T; The Prosecutor against Jean-Bosco Barayagwiza, Amended Indictment, pg. 19, 6.4; Tribunal Pénal International pour le Rwanda; International Criminal Tribunal for Rwanda PDF 5-12-2003
 7. ICTR-99-52-T Prosecution Exhibit P 91B; "A DOCUMENT TITLED RTLM ORGANIZATIONAL STRUCTURE RUGGIUS REPRESENTATION.PDF"
 8. Felicien Kabuga Archived 27 Oktoba 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya trialinternational.org ya tar. 07.06.2016, iliangaliwa Mei 2020
 9. "International Criminal Tribunal For Rwanda: Delayed Justice". International Crisis Group (kwa Kiingereza). 7 Juni 2001. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-25. Iliwekwa mnamo 2020-05-31.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 10. "YouTube". www.youtube.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-06-25.
 11. "How hit squad killed man who laid trap for Kabuga". Daily Nation. Iliwekwa mnamo 17 Mei 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 12. Mathenge, Oliver. "Tough speech that kicked off diplomatic feud", The Daily Nation, 3 November 2008. 
 13. "Rwandan war criminal reportedly in Oslo", Aftenposten, 2 June 2008. 
 14. "- Etterlyst krigsforbryter oppholder seg i Norge", Aftenposten, 1 June 2008. (no) 
 15. 15.0 15.1 Rwanda's Most-Wanted Fugitive, Félicien Kabuga, Arrested For War Crimes
 16. "Risking Irrelevance: The Threat of Impunity to the African Union". Retrieved on 15 June 2018. 
 17. "IRMCT Press release". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-05-17.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]