Beatriz wa Silva

Beatriz wa Silva, O.I.C. (jina kamili kwa Kireno: Beatriz de Menezes da Silva; Campo Maior, Ureno[1] 1424 hivi – Toledo Hispania, 9 Agosti 1492) alikuwa mwanamke wa ukoo maarufu wa Ureno, lakini alijiunga na monasteri na hatimaye akawa mwanzilishi wa masista wamonaki wa Shirika la Bikira Maria Kukingiwa Dhambi ya Asili.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 17 Agosti[2].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]
Beatriz alizaliwa Campo Maior; kati ya ndugu zake 10, mmojawapo ni mwenye heri Amadeo wa Ureno, aliyerekebisha shirika la Ndugu Wadogo.
Mwaka 1447 Beatriz alihamia katika ikulu ya Kastilia ili kumsindikiza rafiki yake Isabela aliyeolewa na mfalme wa huko.[3]
Lakini uzuri wa Beatriz ulimtia kijicho, hata akamfunga katika chumba kidogo.
Humo Beatriz alitokewa na Bikira Maria na kuelekezwa aanzishe shirika jipya kwa heshima yake.
Beatriz alipofaulu kutoroka alikimbilia monasteri ya Wadominiko wanawake (Utawa wa pili) huko Toledo, akaishi huko miaka 37 bila kujiunga nao kisheria.[3][4]
Mwaka 1484 Beatriz na wenzake kadhaa walitamalaki monasteri nyingine ya Toledo aliyopewa na malkia ili itumike kuheshimu Kukingiwa Dhambi ya Asili Bikira Maria.
Mwaka 1489, kwa ruhusa ya Papa Innocent VIII, walipokea sheria za Wasitoo,[3] wakiahidi kuadhimisha kila siku Breviari ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, wakiwa chini ya askofu mkuu wa Jimbo kuu la Toledo.

Baada ya kifo
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1501 Papa Alexander VI aliunganisha jumuia hiyo na Wabenedikto lakini chini ya Kanuni ya Mt. Klara.
Mwaka 1511 Papa Julius II aliwapa kanuni mpya ya kwao, halafu kardinali Fransisko Quiñones aliwaandikia katiba maalumu.
Kuanzia mwaka 1507 shirika lilienea Ureno, Hispania, Italia, Ufaransa na Brazil.
Beatriz wa Silva alitangazwa mwenye heri tarehe 28 Julai 1926 na Papa Pius XI, halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 3 Oktoba 1976.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Congregatio de Cultu Divino et Disciplina Sacramentorum (Kireno) - Decree from the Congregation for Divine Worship and the Discipline of the Sacraments (Vatican, 12 October 2010) which states that modern research has proven her birthplace to have been Campo Maior, in Portugal.
- ↑ Martyrologium Romanum
- ↑ 3.0 3.1 3.2 "Foley O.F.M., Leonard. "St. Beatrice of Silva", Saint of the Day, Lives, Lessons and Feast, (revised by Pat McCloskey, O.F.M.), Franciscan Media". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2014-09-03.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/91204
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Saint Beatrice of Silva Ilihifadhiwa 28 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- Saint Beatrice and the Order of the Immaculate Conception of Our Lady
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |