Nenda kwa yaliyomo

Akilei wa Larissa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Akilei wa Larissa

Mt. Akilei katika mozaiki
Feast

Akilei wa Larissa (pia: Achilles, Ailus, Achillas, Achilius, Achillius; kwa Kigiriki: Άγιος Αχίλλειος, Ágios Achílleios; Kapadokia, leo nchini Uturuki, karne ya 3; Larissa, Ugiriki, 330) alikuwa askofu wa mji huo katika karne ya 4.

Baada ya kupata malezi mazuri, alipofiwa wazazi wake aliwagawia maskini mali zake akaenda kuhiji Yerusalemu na Roma; kutoka huko aliinjilisha sehemu mbalimbali kwa bidii ya kitume iliyothibitishwa na maadili yote. Alipofikia mkoa wa Tessaly alichaguliwa kuwa askofu.[1].

Ni mmojawapo kati ya wale 318 walioshiriki Mtaguso wa kwanza wa Nisea (325). Anakumbukwa kwa hotuba yake ya kutetea imani sahihi na kwa muujiza alioufanya kuthibitisha kwamba mafundisho ya Ario ni uzushi[2].

Baada ya kurudi jimboni mwake alibomoa mahekalu ya Kipagani, alijenga makanisa na kufukuza pepo wabaya kwa wingi[3].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Mei[4][5].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/93009
  2. Taking up a stone, Achillius called to the Arians: 'If Christ is a creature of God, as you say, tell oil to flow from this stone.' The heretics kept silent, amazed at this demand by St. Achillius. Then the saint continued: 'And if the Son of God is equal to the Father, as we believe, then let oil flow from this stone.' And oil flowed out, to the amazement of all.
  3. "God is Wonderful in His Saints". "Our Father among the Saints Achillius, Bishop of Larissa". Orthodox Saints commemorated in May. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Februari 2007. Iliwekwa mnamo 2007-01-18.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Martyrologium Romanum
  5. (Kigiriki) Ὁ Ἅγιος Ἀχίλλιος Ἐπίσκοπος Λαρίσης. ΜΕΓΑΣ ΣΥΝΑΞΑΡΙΣΤΗΣ.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.