Nenda kwa yaliyomo

A Boy From Tandale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
A Boy From Tandale
A Boy From Tandale Cover
Studio album ya Diamond Platnumz
Imetolewa 14 Machi, 2018[1]
Imerekodiwa 2013, 2015, 2016-2017
Aina Bongo Flava, Afro-pop
Lebo Wasafi Records
Universal Music (Pty) Ltd (ZA)
Mtayarishaji Laizer Classic (Mtayarisha Mkuu)
Nahreel
Sheddy Clever
Single za kutoka katika albamu ya A Boy From Tandale
  1. "Number One Remix"
    Imetolewa: 6 Januari, 2014
  2. "Nana"
    Imetolewa: 29 Mei, 2015
  3. "Kidogo"
    Imetolewa: 12 Julai, 2016
  4. "Marry You"
    Imetolewa: 2 Februari, 2017
  5. "Fire"
    Imetolewa: 21 Juni 2017
  6. "Eneka"
    Imetolewa: 10 Julai 2017
  7. "Hallelujah"
    Imetolewa: 28 Septemba, 2017
  8. "Waka"
    Imetolewa: 7 Desemba, 2017
  9. "African Beauty"
    Imetolewa: 15 Machi, 2018
  10. "Iyena"
    Imetolewa: 31 Mei, 2018
  11. "Baila"
    Imetolewa: 12 Julai, 2018


"A Boy From Tandale" ni jina la albamu ya tatu kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Diamond Platnumz. Albamu imetoka rasmi mnamo tarehe 14 Machi, 2018, japo utangazaji wake ulianza tangu kwenye mwezi Oktoba-2017 na kutangazwa kutolewa tarehe 12 Januari, 2018 kabla ya kuruka-ruka tarehe chungumzima za kutolewa.[2][3][4] Sehemu kubwa ya albamu imetayarishwa na Laizer Classic (ambaye pia amesimama kama mtayarishaji mkuu), vilevile kuna nyimbo za awali ambazo baadhi zilitayarishwa na watayarishaji wengine. Nyimbo hizo ni pamoja na Number One, Nikuone na Marry You ambazo zilitayarishwa na Sheddy Clever - Burn Records, Nana iliyotayarishwa na Nahreel wa The Industry, Far Away iliyotayarishwa na S2kizzy na mwisho Iyena iliyotayarishwa na Abby Daddy.

Albamu imeshirikisha wasanii wengi wa ndani na nje ya nchi. Wasanii hao ni pamoja na Young Killer (wimbo wa Pamela), Morgan Heritage (wimbo wa Hallelujah, Rick Ross (wimbo wa Waka), Rayvanny (wimbo wa Iyena), Miri Ben Air (wimbo wa Baila), Omarion (African Beauty), Tiwa Savage (wimbo wa Fire), Ne-Yo (wimbo Marry You, Davido (Number One Remix), Mr. Flavour (wimbo Nana), P Square (wimbo Kidogo), Jah Prayzah (wimbo Amanda), pamoja na Vanessa Mdee kwenye wimbo wa Far Away ambao ndio wa mwisho kutoka katika albamu hii.

Albamu ilianza kutolewa kwa oda kwanza kwenye majukwaa mengi tu ya muziki mtandaoni, hasa iTunes, Songa Music na kwengineko.[5]Albamu ilizinduliwa rasmi mnamo tarehe 14 Machi nchini Kenya chini ya udhamini kamili wa Songa Music (tawi la Safaricom ya Kenya linalojihusisha na masuala mazima ya muziki). Jinsi Songa inavyofanya kazi sawa na Mkito au Mzikii ya Tanzania. Sababu hasa zilizoplekea kuizindulia Kenya ikiwa ni pamoja na kukosekana vifaa ambavyo vingeweza kuonesha mandahari mbalimbali yaliyokuwa yanaonekana nyuma ya fanani aliyekuwa anatoa burudani katika uzinduzi huo. Halkadhalika kuonesha umoja wa kweli wa Afrika Mashariki na sio unafiki. Uzinduzi ulifanyika katika ukumbi wa "Kenya National Theatre".

Diamond anaamini yeye ni mtu wa Afrika Mashariki na popote anaweza kufanya kazi zake bila pingamizi maadamu anafuata utaratibu. Hii sio mara ya kwanza kwa Diamond kufanya kazi Kenya. Mwaka 2012 alienda kufanya video yake ya kwanza ya nje ya nchini, Kesho, na Ogopa Videos na hatimaye kujenga mahusiano mazuri na kufanya video ya pili Afrika Kusini, Number One, tena chini ya Ogopa Videos.

Halkadhalika alikuwa katika nia ya kuitangaza Bongo Flava nje ya Tanzania kwa kumaanisha kabisa. Hii ndio albamu ya kwanza ya Bongo Flava kuzinduliwa nje ya nchi. Nyimbo mbili kutoka katika albamu zimefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa Tanzania. Nyimbo hizo ni pamoja na Waka na Hallelujah.[6]

Historia

[hariri | hariri chanzo]
Kava la kwanza la A Boy From Tandale ambalo lilipendekezwa. Lakini baada ya Universal Music ya Afrika Kusini kuona kama halito-mtambulisha vyema kwa mara ya kwanza picha ya mtoto itavuruga watu. Ndipo palipo-pendekezwa picha badala itumike kama kava.

Harakati za kutoa albamu zilianza muda mrefu. Lakini kwa sababu mbalimbali, Diamond aliona bora isuburi. Kwenye mahojiano yake aliyofanya tarehe 19 Machi, 2018 na Lil Ommy kupitia kipindi cha "The Playlist" cha Times FM, Diamond alifunguka mengi mno kuhusu albamu. Alieleza kwanini albamu ilianza kutolewa katika majukwaa ya kidijitali kabla ya kuuzwa mikononi. Kwanini Wasafi.com haijapata fursa ya kuuza albamu kidijitali kabla ya Songa Music au iTunes.[7] Chibu alifafanua ya kwamba maelewano kati ya wana hisa (Universal Music) hawajafikia sehemu ambayo Wasafi.com wangeweza kusambaza. Badala yake, Songa na iTunes zikashika hatamu. Katika mahojiano hayo na Lil Ommy, Chibu alifunguka kuhusu kusambazwa kwa nakala za CD punde. Vilevile alieleza vidokezo alivyokuwa anatoa kuhusu albamu akiwa nchini Marekani, 2017 akiwa na Rick Ross. Na ilitoka na kava la Diamond akiwa na Rommy Jones wakati yungali mtoto mdogo kabisa - Rommy katolewa (tazama juu).

Azimio la albamu lilikuja katika hamasa zao, baada ya kutoa kibao cha Marry You na kusimamiwa vyema na Universal Music, ndipo walipoona kuna umihumu wa kutoa kitu kamili. Vilevile nyuma ya kava kumeonesha haki zote na usimamizi mzima ni chini ya UMG.

Katika mahojiano hayo-hayo na Lil Ommy, Chibu alitoa la moyoni kuhusu kufingiwa nyimbo zake kwa hasira mno. Alitoa fafanuzi kali na kuonesha hisia zake dhidi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Juliana Daniel Shonza kwa kitendo cha kufikisha taarifa za kufingia nyimbo zake kupitia mitandao na vyombo vya habari bila kumpelekea taarifa zozote zile rasmi katika ofisi yake. Hata hivyo, Shonza alisema hana sababu za kujibu tuhuma na lawama za Chibu kwa vile maamuzi yale hajafanya yeye binafsi bali serikali ndio hasa iliyopendekeza. Baada ya tukio, BASATA walisikitishwa na kauli za Diamond na kumfahamisha ya kwamba, hawalazimiki kupeleka barua ofisini kwake, kama ana malalamiko, alitakiwa atumie njia sahihi kufikisha malalamiko yake badala ya kutoa maneno ya kejeli na kadhalika. Tukio hilo la kihistoria kwa Diamond kujilipua kwa niaba ya wasanii wenzake, lilipokewa kimasikitiko makubwa sana na kusema Diamond sawasawa ameitukana serikali.[8][6] Kwa wasanii walio-wengi, tukio hili waliona ni la kishujaa na hakika Chibu alikuwa anawalilia wasanii wenzake. Licha ya kutosema hadharani. Maswali waliokuwa wanaulizwa na majibu yao dhahiri walifurahia msimamo wa Chibu.

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]

Hii ni orodha ya nyimbo zinazopatikana katika albamu ya "A Boy From Tandale".

Na. Jina la wimbo Mtayarishaji Maelezo
1 Hallelujah Laizer Classic Kawashirikisha Morgan Heritage
2 Waka Laizer Classic Akiwa na Rick Ross
3 Baikoko Laizer Classic
4 Pamela Laizer Classic Akiwa na Young Killer
5 Iyena Abby Daddy Akiwa na Rayvanny. Huu huenda ukawa wimbo uliosababisha Abby Dad na Ali Kiba kuacha kufanya kazi pamoja baada ya Diamond kwenda kwa Abby na kuanza kufanya kazi pamoja.
6 Kosa Langu Laizer Classic
7 Nikuone Sheddy Clever Awali ilifanywa na Marco Chali, halafu Tudd Thomas, ikatokea majanga, kisha kajakumalizia na Sheddy ndio ikawa mpango mzima.
8 Baila Kamshirikisha Miri Ben-Ari - ambaye amepiga violin kwa hisia kali.
9 Sijaona Laizer Classic Katunga na Richie Mavoko
10 African Beauty Krizbeatz biti, Laizer Akiwa na Omarion. Laizer kaingiza sauti tu, biti imetengenezwa na Krizbeatz.
11 Eneka Laizer Classic Wimbo ambao mwenyewe aliutaja kama una ladha ya kimataifa baada ya kutoa ngoma nyingi za kinyumbani.
12 Fire Laizer Classic Tiwa Savage
13 Marry You Sheddy Clever Akiwa na Ne-Yo
14 Number One [Remix] Sheddy Clever Akiwa na Davido
15 Nana Nahreel Akiwa na Flavour
16 Kidogo Laizer Classic Akiwa na P-Square
17 Amanda Akiwa na Jah Prayzah
18 Far Away Laizer Classic na S2kizzy Akiwa na Vanessa Mdee

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]