Nenda kwa yaliyomo

Hallelujah

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Hallelujah”
“Hallelujah” cover
Kasha la Hallelujah
Single ya Diamond Platnumz akiwa na Morgan Heritage
kutoka katika albamu ya A Boy From Tandale
Imetolewa 28 Septemba, 2017
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2017
Aina Bongo Flava, reggae, dancehall [1], muziki wa dunia
Urefu 3:42
Studio Wasafi Records
Mtunzi Diamond Platnumz
Morgan Heritage
Mtayarishaji Laizer Classic
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz akiwa na Morgan Heritage
Zilipendwa
(2017)
"Hallelujah"
(2017)
"Sikomi"
(2017)

'Hallelujah' ni wimbo ulioimbwa na kutungwa na Diamond Platnumz akiwa na kundi zima la muziki wa reggae kutoka nchini Marekani, Morgan Heritage. Wimbo umetolewa tarehe 28 Septemba, 2017. Huu ni wimbo wa pili wa Diamond Platnumz kushirikiana na wasanii kutoka nchini Marekani baada ya ule wa Marry You aliomba na Ne-Yo. Huu ndiyo wimbo wa kwanza Afrika kutazwama mara milioni 1 katika Youtube ndani ya masaa 15 tangu kutolewa kwake. Mtindo wa muziki ni tofauti kidogo na Bongo Flava ya kawaida, kuna mchanganyiko wa reggae, afro-pop, R&B, dancehall na muziki wa dunia.[2][3] Wimbo umetayarishwa na Laizer Classic kupitia Wasafi Records. Kazi ilikuwa kubwa kwa sababu wasanii hawa walikuwa nchi mbili tofauti. Ilikuwa lazima akina Morgan watume sauti kwa Laizer halafu yeye aingize na kuwatumia kwa masawazisho. Mapigo ya wimbo huu ni tofauti na nyimbo zote za awali zilizowahi kutayarishwa na Laizer.[4]

Mapokezi

[hariri | hariri chanzo]

Wimbo umepokelewa vizuri sana hata kwa wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania. Quick Rocka ameonesha hisa zake waziwazi juu ya wimbo huu kwa kusema wimbo umefanywa vizuri sana kuanzia Diamond mwenyewe hadi akina Morgan Heritage. Anaona ni kazi kubwa sana kuvunja rekodi ya kutazamwa mara milioni 1 ndani ya msaa 15, sio jambo dogo.[5]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]