Kidogo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Kidogo”
“Kidogo” cover
Kava ya Kidogo
Single ya Diamond Platnumz na P-Square
kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale
Imetolewa 12 Julai, 2016
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2016
Aina Bongo Flava, Afro-pop
Urefu 4:14
Studio Wasafi Records
Mtunzi Diamond Platnumz
P-Square
Mtayarishaji Shirko
V-Tek
Laizer Classic
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz na P-Square
"Make Me Sing"
"(2016)"
"Kidogo"
"(2016)"
"Salome"
(2016)

"Kidogo" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 12 Julai 2016 kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz akishirikisha kundi la P-Square kutoka nchini Nigeria.

Wimbo unatoka katika albamu ya A Boy From Tandale na wa tatu kutolewa kama single kutoka katika albamu hiyo. Wimbo umetayarishwa na watayarishaji watatu tofauti kabla kuja kumaliziwa mazima katika studio za Wasafi Records. Ndani yake kuna mkono wa Shirko (katengeneza biti), V-Tek (kaichanganya na kuiboresha zaidi) na mwisho kabisa akamalizia Laizer Classic aliyefanya marekebisho ya mwisho kabisa. Kazi ya kutunga wimbo huu ilianza tangu tarehe 10 Januari 2015 katika studio za Square Records, Lagos Nigeria kabla kuja kutia masauti.[1][2]

Video yake imefanywa jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini chini ya Godfather Productions mnamo tarehe 24 Aprili, 2016. Si muda mrefu hadi kuja kuachiwa. Hii ni video ya sita kufanya pamoja na Godfather tangu Mdogo Mdogo, Ntampata Wapi, Nana], Utanipenda, Make Me Sing na huu[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. VIDEO: Diamond Platnumz ft. PSquare – Kidogo Naija Vibes - 2016.
  2. Audio ya Kidogo na maelezo kiasi[dead link] The Choice-TZ - July 12, 2016.
  3. Harmonize – Kainama ft Burna Boy & Diamond Platnumz[dead link] 042cobed - 2019.