Nana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Nana”
“Nana” cover
Kava ya Nana
Single ya Diamond Platnumz na Mr. Flavour
kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale
Imetolewa 29 Mei, 2015[1]
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2015
Aina Bongo Flava, Afro-pop
Urefu 3:50
Studio The Industry
Mtunzi Diamond Platnumz
Mr. Flavour
Mtayarishaji Nahreel
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz na Mr. Flavour
"Nasema Nawe"
"(2015)"
"Nana"
"(2015)"
"Utanipenda"
(2015)

"Nana" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 29 Mei, 2015 kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz akimshirikisha Mr. Flavour kutoka nchini Nigeria. Mashairi na taarifa kuhusu Nana] wavuti ya All Howwe</ref> Huu ni wimbo wa 15 kutoka katika albamu ya A Boy From Tandale na wa pili kutolewa kama single kutoka katika albamu hiyo huku wa kwanza ukiwa Number One Remix. Wimbo ni sehemu ya mwendelezo wa mahusiano mazuri ya kimuziki kati ya Tanzania na Nigeria. Wimbo umetayarishwa na Nahreel chini ya studio ya The Industry. Video imeongozwa na Godfather kutoka Afrika Kusini.

Huu unaufanya kuwa wimbo wa tatu kufanya kazi pamoja na Godfather tangu Mdogo Mdogo na Utanipenda na kazi nyengine za baadaye. Chibu anaulezea wimbo kuwa una ladha ya afro-pop baada ya kusimama tangu Number One (2013-2014) kisha akatoa Bongo Flava tupu mbili (Nasema Nawe na Utanipenda). Chibu huwa na kawaida ya kuweka mizani ya wapenzi wa muziki wake. Kuna kipindi anakuwa Kiafrika nzima, kuna kipindi anarudi nyumbani tu, yaani, Bongo Flava. Nana ni wimbo wenye staili kali za uchezaji ambazo wengi walizirudia ukilinganisha na nyimbo zake za awali.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]