Nenda kwa yaliyomo

Baila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Baila”
“Baila” cover
Kava ya Baila
Single ya Diamond Platnumz akiwa na Miri Ben-Ari
kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale
Imetolewa 12 Julai, 2018
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2018
Aina Bongo Flava, Afro-pop
Urefu 4:17
Studio Wasafi Records
Mtunzi Diamond Platnumz
Mtayarishaji Laizer Classic
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz akiwa na Miri Ben-Ari
"Iyena"
(2018)
"Baila"
"(2018)"

"Baila" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 12 Julai, 2018 kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz akiwa na Miri Ben-Ari kutoka nchini Marekani kwenye violin. Wimbo unatoka katika albamu ya A Boy From Tandale na wa 11 kutolewa kama singo kutoka katika albamu hiyo. Wimbo umetayarishwa na Laizer Classic kupitia studio za Wasafi Records.

Maswali juu ya video ya wimbo[hariri | hariri chanzo]

Chibu kwa mahaba yake kwa mwigizaji wa Bollywood "Shah Rukh Khan", akaona heri achukue japo sehemu ya vipande vya wimbo wake wa "Saans" uliotayarishwa na A. R. Rahman.[1] Baada ya kutoa wimbo, maneno yalikuwa mengi sana mtandaoni. Vurumai za maneno ya kejeli, ambayo Chibu mwenyewe aliyatolea maelezo.[2]

Sababu kubwa ya Kumpendea Sharuk Khan sio tu kuigiza bali ni Ufundi na kubobea kwake kwenye sekta ya Uigizaji wa Mapenzi katika Movie zake... Licha ya Vingi vinipavyo Furaha Lakini kuwa kwenye Mapenzi ama Kumpenda Mtu, ndio stareh yangu kubwa....Na kama ujuavyo, Unapokuwa na kajina Wengi wanakuwa wanakupenda, Wengine kwa dhati wengine kwa Matamanio...ila inapotokea anipendae nami nikampenda, basi huyo Hufaidi haswa Mapenzi yangu... na ndiomaana mara nyingi inakuwaga ni ngumu sana wengi Kunisahau pindi tutenganapo....kwani huwaga na Matendo Mengi Mazuri ya Kimahaba yanayoonekana na Yasiyoonekana gizani, kwasababu nayapenda Mapenzi, na ni Hodari sana kwenye kila taaluma ya kupetipeti... Kwa Machache nilojifunza kwenye Mahusiano nilisema, siku nikikutana na Mwanamke Mpya nitaetaka kuwa nae ...kabla ya Kuianza safari, sitomwambia neno, bali nitamuekea wimbo huu wa #BAILA kwani Maneno yote nitayotaka kumwambia Nimeshayaweka hum....Akisha sikia na Aka-afki, TuTutaianza Safari ya Mahab — Diamond Platnumz - 13 Julai, 2018

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Watiri, Sue, Zari Hassan reacts to Diamond looking for a new woman (kwa American English), iliwekwa mnamo 2018-07-16
  2. Milimo, Dennis, Diamond new video rocked with controversy hours after release [Video] (kwa American English), iliwekwa mnamo 2018-07-16

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]