Nenda kwa yaliyomo

African Beauty

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“African Beauty”
“African Beauty” cover
Kava ya African Beauty
Single ya Diamond Platnumz akiwa na Omarion
kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale
Imetolewa 15 Machi, 2018
Muundo Upakuzi wa mtandaoni
Imerekodiwa 2018
Aina Bongo Flava, Afro-pop
Urefu 3:57
Studio Wasafi Records
Mtunzi Diamond Platnumz
Omarion
Mtayarishaji Krizbeatz (biti)
Laizer Classic (sauti)
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz akiwa na Omarion
"Waka"
"(2017)"
"African Beauty"
"(2018)"
"Iyena"
(2018)

"African Beauty" ni jina la wimbo uliotoka tarehe 15 Machi, 2018 kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz akiwa na Omarion kutoka nchini Marekani. Wimbo unatoka katika albamu ya A Boy From Tandale na wa tisa kutolewa kama single kutoka katika albamu hiyo halkadhalika wa kwanza kutolewa baada ya albamu kutoka. Wimbo umetayarishwa na Laizer Classic kupitia studio za Wasafi Records wakati biti limetengenezwa na Krizbeatz. Sifa pekee ya wimbo huu ndio wa kwanza kwa Chibu kutumia tangazo la kuratibu umri wa mtazamaji katika Youtube. Hii inatokana na ukakasi wa video yenyewe ilivyo. Ikiwa hujajisajili Youtube ili itambue umri wako, video haifunguki hadi ujisajili. [1]

Vilevile ndio wimbo wa kwanza wa Chibu kuwa na matoleo mawili ya video, yenye umri wa kawaida na ya watu wazima. Diamond alipakia video ya wimbo huu mara mbili. Tarehe 15 Machi[2] alipakia yenye kuonesha sehemu kubwa ya utupu wa mwanamke, wakati ya tarehe 16 Machi 2018 imepungua kuonesha utupu.[3]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]