Waka
“Waka” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kava ya Waka
| |||||
Single ya Diamond Platnumz na Rick Ross kutoka katika albamu ya A Boy from Tandale | |||||
Imetolewa | 7 Desemba, 2017 | ||||
Muundo | Upakuzi wa mtandaoni | ||||
Imerekodiwa | 2017 | ||||
Aina | Bongo Flava | ||||
Urefu | 3:17 | ||||
Studio | Wasafi Records | ||||
Mtunzi | Diamond Platnumz Rick Ross | ||||
Mtayarishaji | WCB Wasafi | ||||
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz na Rick Ross | |||||
|
Waka ni jina la wimbo uliotoka tarehe 7 Desemba 2017 kutoka kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania - Diamond Platnumz akimshirikisha Rick Ross kutoka Marekani. Wimbo umetayarishwa na Laizer Classic kupitia studio za Wasafi Records na ni wimbo wa pili kutoka katika albamu ya A Boy From Tandale iliyotoka 2018. Wimbo huu ni wa tatu kushirikisha wasanii kutoka Marekani baada ya Marry You aliyomshirikisha Ne-Yo na Hallelujah aliowashirikisha Morgan Heritage. Vilevile wimbo wa pili kufungiwa (japo zilitajwa kwa wakati mmoja) na Hallelujah.[1] Kwa upande wa lugha, huu ni wimbo wa tatu kuimba sana Kiingereza baada ya Bum-Bum halafu Hallelujah. Japo alisikika akiimba Kiingereza kiasi kwenye wimbo wa Make Me Sing - lakini si sana kama huu na Hallelujah.