Ntampata Wapi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“Ntapata Wapi?”
“Ntapata Wapi?” cover
Kasha ya singo ya Ntapata Wapi
Single ya Diamond Platnumz
Imetolewa 20 Novemba, 2014
Muundo CD, Pakuo la kidijitali
Imerekodiwa 2014
Aina Bongo Flava, Afro-Pop
Urefu 3:46
Studio Burn Records
Mtunzi Diamond Platnumz
Mtayarishaji Sheddy Clever
Mwenendo wa single za Diamond Platnumz
"Mdogomdogo"
(2014)
"Ntapata Wapi"
(2014)
"Nasema Nawe"
(2015)

Ntapata Wapi ni jina la kutaja wimbo uliotungwa na kuimbwa na Diamond Platnumz ikiwa kama single yake ya tatu kutolewa kwa mwaka wa 2014. Mwaka 2014, Diamond Platnumz amepata kutoa vibao vitatu ambavyo ni: Bumbum, Mdogomdogo na huu wa "Ntampata Wapi". Kama ilivyo nia ya msanii huyu, muziki wa video umeongozwa na Godfather kutoka Afrika Kusini na video haijapishana sana na maudhui ya video ya awali, yaani, Mdogomdogo.

Ndani ya wimbo, analalamika juu ya kuachwa na mpenzi wake ambaye awali walikuwa pamoja, ila tu kutokana na shida za pesa wenye mahela wakampora akabaki mpweke. Staili ya uimbaji ni mchanganyiko mkali na ladha za pwani. Huzuni iliyokithiri kuliko nyimbo za awali.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]