Reggae
Mandhari
(Elekezwa kutoka Muziki wa reggae)
Reggae (tamka: "rege") ni aina ya muziki kutoka nchini Jamaika. Ilianzishwa mwaka 1968 na kuwa maarufu kimataifa kwa nyimbo za Bob Marley na kundi lake The Wailers. Pia watu kama Lucky Dube na John Tosh waliwezesha reggae kuwa maarufu.
Reggae hupendwa sana na watu wenye imani ya Rastafari lakini pia watu wa rika, imani na mataifa mbalimbali kote duniani.
Vifaa vya kawaida katika bendi ya Reggae ni ngoma, gitaa ya besi, gitaa na kibodi pamoja na sauti za waimbaji.
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Reggae kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |