Nenda kwa yaliyomo

Gitaa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Luan Breva (kushoto) na Paco de Lucena (kulia) walikuwa wapiga gitaa mashuhuri wa aina ya flamenco mnamo 1880.
Paco de Lucía mpiga gitaa wa flamenco ya kisasa.

Gitaa (kutoka Kiingereza: guitar) ni ala ya muziki yenye nyuzi 4 hadi 12 zinazokazwa na kupigwa kwa kuzidonia kwa kidole au kucha.

Gitaa huwa na bodi yake ambayo ni sanduku la ubao na juu yake shingo ambako nyuzi zinafungwa na kukazwa. Gitaa la kawaida huwa na nyuzi 6. Bodi ya kawaida ina uwazi ndani yake inayopazia sauti ya nyuzi.

Vidole vya mkono mmoja vinakaza nyuzi sehemu za shingoni na kutawala sauti ya uzi kuwa juu au chini. Vidole vya mkono mwingine vinapiga nyuzi juu ya bodi na kuleta mipapatiko inayotoa sauti.

Kuna pia gitaa za umeme ambako kifaa kinachukua mipapatiko ya uzi na kuibadilisha katika umeme wa aina tofauti inayosikika kwenye kipazia sauti. Aina hii haihitaji bodi yenye uwazi ndani yake.

Gitaa hutumiwa kwa muziki wa mitindo mbalimbali kama klasiki, reggae, rumba, charanga, na rock. Ukulele pia ni chombo cha muziki kinachofanana na gitaa lakini huwa ni ndogo na yenye nyuzi nne pekee.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gitaa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.