Wikipedia ya Kiafrikaans

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Favicon of Wikipedia Wikipedia ya Kiafrikaans
Kisarahttp://af.wikipedia.org/
Ya kibiashara?Hapana
Aina ya tovutiMradi wa Kamusi Elezo ya Internet
KujisajiriHiari
Lugha asiliaKiafrikaans
MmilikiWikimedia Foundation

Wikipedia ya Kiafrikaans (kwa Kiafrikaans: Afrikaanse Wikipedia) ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kiafrikaans. Mradi huu ulianzishwa tarehe 16 Novemba 2001, na ilikuwa Wikipedia ya 11 kuanzishwa.[1]

Tarehe 13 Mei 2009, toleo hili lilipita makala 12,000[2] na mwaka 2021 limezidi makala ya 100,000, likiwa toleo la 71 kwa ukubwa.

Awali lilikuwa toleo kubwa la Wikipedia katika lugha za Kiafrika, na pia lilikuwa toleo la kwanza la Wikipedia ya lugha za Kiafrika kupita makala zaidi 10,000[3]. Kwa sasa toleo la Kiarabu cha Misri linaongoza kwa mbali sana. Baada ya Kiafrikaans, zinafuata Wikipedia ya Kimalagasi na Wikipedia ya Kiswahili.

Mbali na Waafrika Kusini, Wikipedia pia uhaririwa na watu wa kule Uholanzi, Ubelgiji, Namibia, Ujerumani na baadhi yao kutoka nchi za Skandinavia.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikipedia
Wikipedia
Wikipedia ya Kiafrikaans ni toleo la Wikipedia, kamusi elezo huru