Wikimedia Foundation
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wikimedia Foundation ni shirika lisilo la serikali katika Marekani linaloendesha wikipedia pamoja na miradi mingine.
Shabaha yake ni usambazaji wa elimu huria inayopatikana bure kwa watu wote kwa njia ya mtandao. Ilianzishwa na Jimmy Wales mwaka 2001. Shirika inaendeleza maendeleo ya programu huria za wikiwiki zinazomruhusu msomaji si kusoma tu bali kuandika na kuhariri vilevile.
Wikimedia Foundation kama miradi yake yote si kibiashara na yaliyomo yote yanatungwa na wachangiaji wengi wanaojitolea bila malipo.
Mapato ya shirika hutokana na michango ya watu binafsi. Makampuni na taasisi za elimu hujitolea pia kwa kutoa kompyuta na nafasi ya kutunza data kwenye server zao.
Kati ya miradi ya Wikimedia Foundation pamoja na wikipedia kuna Wiktionary, Wikiquote, Wikisource, Wikinews, Wikibooks, Wikiversity, Wikimedia Commons na Meta-Wiki.
Shirika hili haliangalii yaliyomo kama makala ya wikipedia ambayo hutungwa na jumuiya za watumiaji katika lugha zinazofikia karibu 200.
