Wikipedia ya Kiitalia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
![]() |
|
| Kisara | http://it.wikipedia.org/ |
|---|---|
| Ya kibiashara? | Hapana |
| Aina ya tovuti | Internet encyclopedia project |
| Kujisajiri | Hiari |
| Lugha asilia | Italian |
| Mmiliki | Wikimedia Foundation |
| Mwanzilishi | Jumuia ya wiki ya Kiitalia |
Wikipedia ya Kiitalia (Kiitalia: Wikipedia in italiano) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiitalia. Toleo hili lilianzishwa mnamo mwezi wa Januari katika mwaka wa 2002 na ina makala zaidi ya 527,000 na watu waliojisajiri ni zaidi ya 338,000 kwa tar. 5 Januari, 2009[1].
Mnamo mwezi wa Agosti 2005, Wikipedia ya Kiitalia imeipita toleo la Wikipedia ya Kihispania na Kireno, na kuifanya iwe Wikipedia ya 8 kwa ukubwa wa hesabu ya makala. Sababu za msingi zilizopelekea Wikipedia hii kuwa kubwa ni baada ya kuruka idadi ya makala kutoka 56,000 hadi 64,000. Ambazo zote zilifanywa na maroboti ambao walitengeneza makala za mbegu zaidi ya 8,000 kuhusu miji na maeneo ya Hispania.[2][3]
Mnamo tar. 8 Septemba, 2005, Wikipedia ya Kiitalia imeipita Wikipedia ya Kiholanzi na baada ya siku moja, mnamo Septemba 9, ikapita makala 100,000. Mnamo tar. 11 Septemba, imeipita Wikipedia ya Kiswidi, na kuifanya iwe toleo la Wikipedia ya tano kwa ukubwa. Tena, maboti yakafanya michango mizito kwa kuikuza Wikipedia hii. Kwa mfano, maboti yametunga zaidi ya makala 35,000 kuhusu manispaa za Ufaransa.[4]Hata hivyo, ilikuja kupitwa na Wikipedia ya Kipoland mnamo tar. [[23 Septemba, 2005.
[hariri] Marejeo
- ↑ Italian Wikipedia. Speciale:Statistics. Retrieved on 2009-01-05.
- ↑ Italian Wikipedia. Wikipedia:Ultime_notizie. Retrieved on 2008-02-23.
- ↑ Italian Wikipedia. Progetto:Geografia/Antropica/Comuni_spagnoli. Retrieved on 2008-02-23.
- ↑ Italian Wikipedia. Progetto:Comuni_della_Francia. Retrieved on 2008-02-23.
